Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

3000.jpg
 
Nimefurahi kuwafunga hawa wanoko wetu huwa wanatutesa sana hawa. Na ushindi huu utaongeza hamasa kubwa kwa wacheza katika siku za usoni kufanya vizuri zaidi. On top of that my prediction of 3-0 is 110% accurate lol!

Mana ndiyo naona sasa hivi watuma picha kwa fujo.
 
hahahahahah lol! haya kila la heri ila wakianza kukusumbua mie simoooooo, you know what I am talking about
Hawawezi aiseee........ .....mana humu wanapenda chura na mie kimbaumbau.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sijui Gundu ndo limeisha leo au ni linanukia kuisha... labda tutajua tutakapowagonga wale manyang'au wengine.. Back to 3rd.
 
Nimefurahi kuwafunga hawa wanoko wetu huwa wanatutesa sana hawa. Na ushindi huu utaongeza hamasa kubwa kwa wacheza katika siku za usoni kufanya vizuri zaidi. On top of that my prediction of 3-0 is 110% accurate lol!
Yani itabidi niwe nakutumia kwenye utabiri kwa kweli......
 
Mechi tuliyocheza vizuri off the ball kuliko zote msimu huu ni hii. Tungetumia nafasi (hasa Walcott) vizuri tungewagonga 4 au 5 leo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wako wapenda vimbau mbau wana sababu zao za kupenda vimbau mbau pia, ole wako uweke hapa.

Hawawezi aiseee........ .....mana humu wanapenda chura na mie kimbaumbau.
 
Ni kweli kabisa hatuna uchu wa magoli siye, tungeweza kabisa kushinda kwa goli 5.

Mechi tuliyocheza vizuri off the ball kuliko zote msimu huu ni hii. Tungetumia nafasi (hasa Walcott) vizuri tungewagonga 4 au 5 leo.
 
4148.jpg

A frustrated Diego Costa

Pretender katika ubora wake....and the Oscar goes to......
 
5568.jpg

Chelsea’s Marcos Alonso gets to grips with Arsenal’s Hector Bellerin.
 
5568.jpg

Chelsea’s Diego Costa tussles with Arsenal’s Shkodran Mustafi.
 
Kwa wale tuliokuwa tunahoji kwa nn Xhaka na Perez wasianze katika mechi ya leo:

Xhaka ni mchezaji mzuri hilo halina shaka. Tangu akiwa Bundesliga na hata ktk Euro 2016 amedhihirisha hilo. Perez pia amecheza vizuri sana dhidi ya N. Forest juzi ktk EFL Cup.

Lkn tukirejea katika partnership ya Carzola na Coquelin ndiyo bora kwa upande wa Arsenal kabla ya kuumia kwa Carzola karibu nusu ya msimu uliopita na pia Coquelin kuanza kuandamwa na majeruhi pia.

Kwa hivyo, Wenger kumuanzisha Coquelin na Carzola hakukosea kwa maana ya mafanikio wawili hao waliyomletea tangu waanze kucheza pamoja.

Kuna wakati Wenger alitaka kubadili kwa kumchezesha Ramsey na Coquelin na Carzola kumpeleka pembeni. Matokeo hayakuwa mazuri ikabidi arejee kulekule kwa Coquelin na Carzola.

Kubadili partnership ya wachezaji wanaofanya vizuri tena katika mechi muhimu ni sawa na kubet suala ambalo hakuna kocha aliye tayari kulifanya.

Vilevile, Xhaka na Perez bado wageninwa BPL wanahitaji muda wa kuifahamu na kuendana na kasi na fiziki ya ligi. Kingine ambacho ni cha muhimu pia Arsenal wana mechi nyingi tu za EFL Cup, FA, BPL na UCL na hapa ndiyo kwanza msimu umeanza.

Kadhalika, kuna wachezaji kuchoka na kushuka kiwango mechi zinapochanganya. Hivyo, kuwa na wachezaji wengi au kikosi kikubwa ni muhimu sana inapofika kipindi hicho.

Mfano mzuri ni sasa baada ya kuumia Coquelin ktk mechi dhidi ya Chelsea, Xhaka kaingizwa kuziba nafasi yake. Na kadri mchezo unavyokwenda kunaweza kutokea marekebisho yatakayo hitaji mabadiliko kwa wachezaji ambayo yatamlazimu mwalimu kuyafanya.
 
Back
Top Bottom