Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mapungufu ya mpila,refa anawez kuia timu na akakiri baadaye hakuona vizuri,lakini timu imeumia red card ya metersaker inautata mkubwa sana,hakuna mahari walipogusana
Ina maana kila cku refa awaonee nyie tu iwe nyumbani iwe ugenini !!
The Mandaz bhana..

Khekhekheeeeeeee
 
Sioni ni kwa namna gani aseno wanaweza kubadili haya matokeo. Sanasana watakuwa wakijilinda kupunguza magoli. Poleni fans wote wa aseno hongereni mashabiki wote mliopo leicheste kwa mkopo.
 
Mapungufu ya mpila,refa anawez kuia timu na akakiri baadaye hakuona vizuri,lakini timu imeumia red card ya metersaker inautata mkubwa sana,hakuna mahari walipogusana
Chifu, weka unazi pembeni. Ile ilikuwa straight red card bila wasiwasi wowote. Per alikuwa the last man, na alimgusa Diego. Ndiyo shida ya hiyo professional foul last man, beki inabidi awe makini sana katika kufanya tackling, kwani hata ukimgusa kidogo tu mchezaji wa timu pinzani, refa hasiti kukupa kadi nyekundu.
 
Timu zimerudi uwanjani na hakuna mabadiliko Zaidi ya Arsenal waliofanya mabadiliko kwa Gabby ambae aliingia badala ya Per Mertesacker.
 
mert_3557682b.jpg


Mabeki wa Arsenal walikuwa wmepanda sana na hivyo kumfanya Willian kutoa pasi ilopita katikati yao na kumkuta Costa.

Kwa hali hiyo ilitakiwa Mertesacker amwache tu Costa aende na kuomba Cech akabiiane nae na pengine hata Bellerinangeweza kumkuta Costa.

Ni about "decision making process", ukikosea tu mahali basi unaathiri mpango mzima.
Ndiyo maana uwa nakukubali sana chifu. Wewe ni shabiki wa soka kweli kweli. Penye ukweli unasema hata kama ukweli huo unaiumiza timu yako. Hivyo ndivyo shabiki anapaswa kuwa. Na siyo kuweka unazi tu hata kwa mambo ambayo yapo wazi.
 
Alexis Sanchez anajiandaa kuingia na ametoa suti yake ya mazoezi.
 
Kuna dalili zote za msiba leo ....The Mandaz komaeni bhana tumechoka kuwaona Chelsea fake (Leicester) na jezi zao za blue kileleni
Khekhekheeeeee
 
Dakika ya 57 Alexis Sanchez anaingia na Joel Campbell anapisha.
 
Mpira wa adhabu unapigwa kuelekea Chelsea na kunafanyika shughuli lakini mpira umetoka na unakuwa wa kupigwa na Chelsea.

Dakika inakwenda ya 64
 
Chelsea wanafanya mabadiliko na Diego Costa anatoka na Loic Remmy anaingia.
 
Theo Walcott anatoka na Oxlade Chamberlain anaingia dakika inakwenda ya 74
 
Doh! Yaani mkishindwa hata kupata droo kwenye hii mechi, mjilaumu sana. Hawa Rent boys hawana kitu kabisa sasa hivi...yaani wanacheza kama vile wao ndiyo wapo pungufu!
 
Arsenal hawawezi kabisa kutafuta nafasi za kufunga zimebakia dakika kama 4 hivi
 
That's it mpira umekwisha na hongera Chelsea kwa ushindi ulopatikana kipindi cha kwanza.

Timu imecheza mechi hii kwa dakika 70 ikiwa na wachezaji 10
 
Back
Top Bottom