Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

everlenk njoo muone hii Nonda inaleta uchambuzi yake na huku kwa gunners. Hii ni mutu ya hatai sn..... Kule kwetu naondoka na chadomo......
Khe khe khe khe ngoya ile Wacha1 ije....

HahahAha tumpe pole jana amepata kimoko toka kwa L ooserfool......
 
Last edited by a moderator:
Mimi bado naamini kwamba tatizo la Arsenal ni Kocha,,Wenger ni tatizo.Baada ya kikosi chetu cha ushindi kutawanyika,huyu babu hajawawahi kuumiza kichwa kutengeneza kikosi zaidi ya kutuletea Adebayo,,bendtner,,Giroud,,Czech na vilaza wengine wengi.Huyu babu utashangaa akikosa ubingwa msimu huu bado kuna wazungu wataongeza imani yao juu ya huyu mzee asieenda likizo wala kupumzisha akili yake iliochoka.

Kuna Wenger humu anaitwa Wacha1 akikusikia atakutoa macho.
 
Last edited by a moderator:
J
Mimi bado naamini kwamba tatizo la Arsenal ni Kocha,,Wenger ni tatizo.Baada ya kikosi chetu cha ushindi kutawanyika,huyu babu hajawawahi kuumiza kichwa kutengeneza kikosi zaidi ya kutuletea Adebayo,,bendtner,,Giroud,,Czech na vilaza wengine wengi.Huyu babu utashangaa akikosa ubingwa msimu huu bado kuna wazungu wataongeza imani yao juu ya huyu mzee asieenda likizo wala kupumzisha akili yake iliochoka.

Arsenal bhana inafurahisha, wakishinda masuala ya Wenger hayaongelewi wanaongelea ubingwa tu, wakishindwa kocha mbaya hafai. Wenger anaonjesha tende mwezi moja unaofuatia shubiri vumilieni tu nafasi ya nne ni yenu. Teheteheteheee
 
Eti wanasema Arsenal hawawez kufika kileleni hadi wapelekwe kwa dr mwaka
 
Nani anashangaa Arsenal kupigwa nne na Soton. Tokea 2003 -2004 Arsenal haijawahi kuifunga Soton nyumbani.Sasa kupigwa arbaa sio jambo la ajabu.
 
Umetaja Ozil na sanchez tu peke yao

na point 36 hiz tumezipata kwa kumpiga na City huyu huyu na hao wengine wameshindwa kuzifikisha so far let's appreciate our team's efforts, na tukubali league ni ngumu kila timu ni beatable

Flamini inafahamika sio mtu wa kutuvusha mbali ila by next week dirisha litakuwa open NEW DM ni lazima

ila kauli yako kuwa wachezaji woote ni useless ispokuwa Ozil na sanchez ni kupanic tu na mshktuko wa matokeo hamna kingine

Ubingwa kuona nan anachukua Sio sasa ni hukooo march ndio unaona huyu na huyu wanabeba....

historia iko wazi walio na 35+ points by christmass ndo tittle conteders so far naona City na Arsenal mpaka mwisho

atakayekuwa consistent atakuwa bingwa next may 2016
Ni wapi nimesema Ozil na Sanchez pekee? Nimetaja wachezaji kama 5 to 6 hivi, na ndio ukweli.
 
Sasa Gibbs ndo world class au squad player tu!

Huwez kuwa na World class wawili number moja....tena hasa beki mmoja akikaa benchi atatafuta mlango wa kutokea tu

ukiangalia squad nyingi XI inakuwa na mchanganyiko wa World class wachache na wengine top class wanaokaa benchi mara nyingi ni Average

kumaintain mchezaji mzuri akiwa bench ni ngumu atataka tu KUHAMA na hakuna mtakachofanya mtauza, mfano upo wazi Matheu Debuchy anataka kukimbia maana anaona yeye hana hadhi ya kukaa Benchi wakati France national team yeye ni XI

na january hii atalazimisha kuuzwa kwa kuwa ana presha ya kucheza EURO16 katika kikosi cha france
 
kuna kicheko humu hua kinachekwa saana kheeee kheee kheeee lakini naona toka jana sijikiona kunani!!!
 
Huwez kuwa na World class wawili number moja....tena hasa beki mmoja akikaa benchi atatafuta mlango wa kutokea tu

ukiangalia squad nyingi XI inakuwa na mchanganyiko wa World class wachache na wengine top class wanaokaa benchi mara nyingi ni Average

kumaintain mchezaji mzuri akiwa bench ni ngumu atataka tu KUHAMA na hakuna mtakachofanya mtauza, mfano upo wazi Matheu Debuchy anataka kukimbia maana anaona yeye hana hadhi ya kukaa Benchi wakati France national team yeye ni XI

na january hii atalazimisha kuuzwa kwa kuwa ana presha ya kucheza EURO16 katika kikosi cha france

Mathieu Debuchy hana uwezo ambao Hctor Berrelin anao, is as simple as that.

Na magoli ya jana hayakupitia pembeni bali katikati na hapo tunazungumza uwezo wa Aaron Ramsey kurudi kusaidia namba 6 wake Mathieu Flamini.

Tofauti ya Wenger na watu kama Pepe Guardiola ni kuweza kuwa na Plan B pale unapoona timu kama Southampton watakuja na very physical game ambayo itavuruga plan A yako.

Unachofanya unajiandaa kutoka sare au kushinda ushindi mdogo.
 
Yaani wewe unamkosoa Wenger?Una utaalamu gani wa kujua kwamba Wenger ana mapungufu ambayo Guardiola hana? Guardiola ni kocha aliyekuta timu zipo ready made mifano ya Barca na Bayern inajieleza wazi. Nitamheshimu kama atajenga timu kama Wenger.Wenger aliikuta Arsenal inacheza butua butua Mungu yupo mpaka leo imekuwa timu inayocheza kandanda la kueleweka. Huwezi kujua thamani ya kitu au mtu kikamilifu mpaka umkose au ukikose. Mwisho football ni lazima timu ama ishinde, kutoka sare au kufungwa. Tatizo la mashabiki/makocha tunakosoa timu inapofungwa tunasahau kuna matokeo mengine.
 
Tena wakati timu ipo nafasi ya pili katika msimamo.
 
kos-ritchie_3536023b.jpg

Arsenal VS Bournemouth

Uwanja: Emirates

Baada ya kufungwa na Southampton goli 4-0 Arsenal ndani ya masaa 48 wanawakaribisha timu ya Bournemouth uwanjani EMIRATES.

Ni mechi itakayotoa mwelekeo wa timu yetu ambayo inalisaka kombe la ligi kuu ya Uingereza ikiwa inapewa nafasi ya kulitwaa kombe hilo ililolipoteza zaidi ya miaka 10 ilopita.

Katika mchezo wa jana baadhi ya wachezaii walionekana wanahitaji kupumzishwa Joel Campbell, Mathieu Flamini na Mertesacker walionekana wapo hoi.

Tusisahau kwamba ni wachezaji hawahawa pamoja na wenzao ndio wameivusha timu yetu hadi kufikia hapo tulipo ikizingatiwa kuna majeruhi kama Alexis Sanchez, Santiago Cazorla na wengine.

Nafikiri meneja Arsene Wenger bado anataka asilimia 100 kutoka kwa dream first II yake na ambayo ni juzijuzi tu waliifunga Man City.

Lakini jana Theo Walcott alionekana amepotea, Olivier Giroud akawa peke yake kule mbele na Mesut Ozil kwa kuwa amekuwa mpikaji na mtengenezaji mipira mizuri na kutoa msaada wa ushambulizi, Southampton wakaja na wazo la kumzuia kabisa asifanye yote hayo

Arsenal wakawa wamebanwa na Victor Wanyama akawa amemzidi Aaron Ramsey kwa nguvu, Southampton walikuwa wakicheza kama wapo kwenye fainali!

Sasa kwenye mechi ya kesho ningekuwa Wenger basi, Mertesacker, Ramsey na wangeanzia kwenye bench na nafasi zao zikazibwa na Gabby Calum Chambers na OX Chamberlain.

Hivyo timu itakuwa na wachezaji wapya kistamina na hivyo kutokusimama na kukaribisha mashambulizi ya mara kwa mara.

Hivyo timu ingekuwa kama ifuatavyo:

Cech, Monreal, Berrelin, Gabby na Koscielny, katikati namba 6 Calum Chambers namba 8 Aaron Ramsey, Kulia Theo Walcott Kushoto Ox Chamberlain namba 10 Ozila na namba 9 ni Giroud.

Wachezaji wa akiba- Ospina, Gibbs, Mertesacker, Campbell, Iwobi na Reine Adelaide.

Ila kuendelea kuchezesha wachezaji ambao wamechoka bila kuwapumzisha hakutaisadia timu yetu na kelele za wale mashabiki uchwara za "Wenger Out", zitarudi maana sasa hivi wapo kimya na yule mjinga wao Pierce Morgan.

COYGs!
 
Back
Top Bottom