Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

THE SPECIAL ONE...

12390989_1659324514107758_3226646624063560227_n.png

Mlikuwa na #Trophyless ikakata mnahamia kwenye EPL na tunachukua come to may

mtahamia UCL khe khe khe kheeeee
 
Sawasawa kabisa mkuu tunangoja hilo kabumbu, na vijana wapo imara kabisa.

Ikumbukwe tuna game nne muhimu baada ya hii game boxing day tunakutana na Southampton, na tarehe 28 tunacheza na vijana wa pwani ya Bournemouth,

Baada ya hapo tutaanza mzunguko wa pili kwa kuwakaribisha Newcastle tarehe 2 January.
 
Mimi mgeni wako leo jamani usinikimbie na nilivyo na machungu niandalie red win kabisa nicheki game kwa uzuri kabisa.....

Naomba kule kwako usiondoe turubai maana Britania sio sehemu salama kabisa hakika kabla ya kuanua matanga una msiba mwingine.
 
Habari za jioni wakuu.

Team news, bado hazijathibitishwa lakini kuna uwezekano mkubwa timu itakayoanza ikawa ni ile iloanza dhidi ya Aston Villa jumapili ilopita.

Yaani timu hio ilikuwa kama ifuatavyo.

Kipa Petr, beki kulia Berellin, beki kushoto- Monreal, mabeki wa kati ni Per Mertesacker na boss Coscielyn. Namba 6 Flamini,kiungo wa kati ni Aaron Ramsey, pembeni kulia Joel Campbell, pembeni kushoto ni Theo Walcott namba 10 ni Mesut Ozil na namba 9 ni Olivier Giroud.

Habari ingine ni kwamba Alexis Sanchez huenda akachukua nafasi ya Campbell au akaingia kipindi cha pili.

Man City nao Vincent Company bado ni majeruhi hivyo Otamendi na Mangala kundelea kuwa mabeki wa kati, huku Sergio Aguero akitegemea kuanza au kuingia kipindi cha pili.

Ngoja nimalizie Glass yangu ya Martell.

Merry Xmass!!
 
Masuala ya takwimu.

Arsenal wamepoteza mechi moja tu kati ya 18 za nyumbani dhidi ya Manchester City yaani wameshinda mechi 11 na kutoka sare mechi 6. Lakini wameshinda mechi 1 kati ya 6 walizocheza hivi karibuni.

Manchester City wamepoteza mechi 22 kati yake na Arsenal na hii rekodi wanachangia pamoja na Chelsea.

NB

Chanzo cha Takwimu hizi nio OPTA INDEX
 
arsenal leo kushinda itakua ngumu,sababu kiungo chake hakiwezi shindana na cha city,pia ramsey anapenda kufunga kuliko majukumu yake kama kiungo na kujisahau kule mbele kiasi kwamba hujikuta yupo nyuma ya mpira wakat tim inashambuliwa,sanchez ni bora asicheze,ataumia zaid na kufanya akose mechi nyingi..japo mpira hudunda
 
Official team news.

aaron-ramsey-heade_3528255b.jpg

Key man Aaron Ramsey.

Alexis Sanchez hayumo.

Arsenal ni ile iloanza na Aston Villa jumapili ilopita.

Arsenal

Cech; Bellerin, Koscielny, Mertesacker, Monreal; Flamini, Ramsey, Walcott, Ozil, Campbell; Giroud

Wachezaji wa akiba
 
arsenal leo kushinda itakua ngumu,sababu kiungo chake hakiwezi shindana na cha city,pia ramsey anapenda kufunga kuliko majukumu yake kama kiungo na kujisahau kule mbele kiasi kwamba hujikuta yupo nyuma ya mpira wakat tim inashambuliwa,sanchez ni bora asicheze,ataumia zaid na kufanya akose mechi nyingi..japo mpira hudunda

Sawasawa kabisa.

Lakini Ramsey amepewa majukumu ya kuhakikisha anacheza vizuri na Flamini na huku Walcott na Berrellin wakiwa wanawaweka nyuma mabeki wa Man City ndani ya eneo lao ili wasiende mbele.

Kama uliangalia mechi za Arsenal dhidi ya Olympiakos na Aston Villa utaelewa vizuri, Ramsey alikuwa anarudi nyuma kufanya defensive duties.
 
CWgHiVVW4AA8mLO.jpg

Smooth operator

Huyu na Ramsey wanatarajiwa kushirikiana sana.

Ozila ana utaalam wa kumiliki mpira.
 
Timu zaingia uwanjani.

Arsenal kama kawaida yao wamevaa jesi nyekundu na kaputula nyeupe
 
Timu zote zimejaribu na Giroud akapewa mpira katikati ya boksi.

Walcott ameanza upande wa kushoto na atakuwa akibadilishana na Joel Campbell.

Dakika inalwenda ya 5
 
Back
Top Bottom