Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Katika siku ambayo nimeshuhudia Arsenal ikicheza kwa kujituma na bidii kubwa ni leo dhidi ya hii timu ngumu ya Crystal Palace.

Lakini baada ya Olovier Giroud kufunga goli la kwanza kwenye dakika ya 16 ndipo mpira ukawa umeanza rasmi.

giroud-goal-rex_3409357b.jpg

Giroud akifunga goli la kwanza.

Arsenal leo walijipanga kama ilivyotarajiwa huku Berellin akimbadilisha Debuchy na Cazorla akiwa katikati, pembeni Ramsey na Ozil, kati Sanchez na Giroud kati, Arsenal ikarudi kuwa timu ya kawaida.

Lakini dakika ya 23 Joel Ward akapata mwanya na kupiga shuti umbali kama mita 25 hivi.
ward-goal_3409368b.jpg

Joel Ward akiifungia timu yake goli la kusawazisha.

Baada ya mapumziko Arsenal wakawa wanaendelea kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini C Palace nao wakawa wanataka kumtumia Francis Coquelin hasa Cabaye.

Dakika mbili baada ya kipindi cha pili kuanza Coqulin akaamua kuanza kumshughulikia Zaha ambae alikuwa anasumbua upande wa Nacho Monreal.
coquelin-yellow_3409381b.jpg

Lakini kuna wakati akaenda haraka na akapiga kiatu na mwamuzi Marson akampa kadi ya njano.

Coquelin akiwa anashughulika pale katikati akisaidiana na Ramsey akawa na kazi ya kuwachunga Zaha na McArthur.

Dakika ya 62 Coquelin akapiga kiatu kingine kwa McArthur na kila mwana Palace akawa anataka Coquelin apewe kadi nyekundu.

Per Mertesacker akamwashiria meneja Wenger amtoe Coquelin ili kuepusha balaa na baada ya mida kidogo Alex Chamberlain akaingia kuchukua nafasi yake.

Baada ya hapo Kieran Gibbs nae akaingia kuchukua nafasi ya Ozil na Arsenal wakaendelea na taratibu za kumaliza mchezo.

Kwa ujumla ni matokeo mazuri na yanaleta ahueni kwa kila mpenzi wa timu hii ambayo inatazamwa kwa jicho la husda na kila mwenye wivu.

Tunawakaribisha Liverpoo Emirates Jumatatu tarehe 24 August.

COYG!!
 
Mourinho anasema ni fake resurt!!!na mimi namsapoti kwa sababu ingekuwa original alitakiwa apigwe hata 6-0.....poleni wana darajani
 
Tumeanza ligi, vijana naona walifikiri bado wako pre-season, ole wao walio mbele yetu, ni kichapo cha kwenda mbele tu, hakuna masihara tena...
C O Y G..
 
Jamani, hivi Game Theory, muasisi wa huu uzi wa Arsenal yuko wapi? mara ya mwisho yeye kuwa active ilikuwa 2012, HOMEPAGE yetu IMEPOOZA sana kuliko HOMEPAGE zote za timu humu, inahitaji updates kibao! Yeye ndo mtu wa kui-update, kama vipi, Moderator, Invisible iunganisheni hii thread na thread ya mtu ambaye yuko active ktk uzi huu awe kama administrator ili awe anafanya updates, ningependekeza Wacha1 au rubaman.
 
Last edited by a moderator:
Jamani, hivi Game Theory, muasisi wa huu uzi wa Arsenal yuko wapi? mara ya mwisho yeye kuwa active ilikuwa 2012, HOMEPAGE yetu IMEPOOZA sana kuliko HOMEPAGE zote za timu humu, inahitaji updates kibao! Yeye ndo mtu wa kui-update, kama vipi, Moderator, Invisible iunganisheni hii thread na thread ya mtu ambaye yuko active ktk uzi huu awe kama administrator ili awe anafanya updates, ningependekeza Wacha1 au rubaman.

Ahsante kwa recommendations. But I'm not interested kuwa moderator.
 
Kuna reporter mmoja huwa anatweet mpaka unaweza chukia uwongo wake kuhusu usajiri hasa arsenal sjui anatachukuliaje arsenal fans
 
Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee nicheke mie niliweka pics kibao jana za ushindi wa Gunners naona imewauma wengi wameamua kuziondoa safi sana na mwaka huu watakonda tu khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom