Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

arsenal anatabia ya kuvionea vitimu vidogo vidogo hvi, lakn nikikumbuka walivochukua hyo FA dhidi ya hull city msimu uliopita, mmmmmh game itakua ngumu, lets wait and see

Nakubaliana na wewe katika FA Cup tunabebaga ndoo baada ya kuonea vitimu vidogo kama Manchester United FA CUP final 2005, FA CUP QF 2015
 
Anyway, mniamshe tukishabeba kombe nimelewa shauku sasa hivi.
 
team news, Theo Walcott anaanza kama mshambuliaji na Olivier Giroud atakuwa bench.
 
Arsenal Team: Kipa Szczesny, Beki wa kulia Bellerin, kati namba4 ni Mertesacker na mkoba ni Koscielny. Kushoto kuna beki Monreal, namb sita ni Coquelin, namba nane Santiago Cazorla, namba saba Ramsey, namba nane ni Ozil,namba tisa ni Theo Walcott na namba 10 ni Alexis Sanchez.

Wacheaji wa akiba: Gibbs, Gabriel, Wilshere, Giroud, Ospina, Oxlade-Chamberlain, Flamini.


Aston Villa Team: Kipa Given, beki wa kulia ni Hutton, kati kuna Vlaar na Okore, beki wa kushoto ni Richardson, namba sita ni Westwood, saba ni nahodha Fabian Delph, namba nane ni Cleverley, kumi ni Grealish, namba 11 ni N'Zogbia, na namba tisa ni Christian Benteke.

Wachezaji wa akiba: Guzan, Baker, Bacuna, Sinclair, Agbonlahor, Cole, Sanchez.

Mwamuzi ni Jon Moss ambae ni mzaliwa wa Wilaya ya Yorkshire Magharibi. au West Yorkshire.
 
. Arsenal team to play Villa: Szczesny,
Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal,
Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil, Alexis, Walcott
 
Last edited by a moderator:
Mtazamo wa haraka maeneo ya shughuli pevu uwanjani.

Mabeki Per Mertescker na Coscielyn watakuwa na kazi ya kumchunga Chritian Benteke na kuhakikisha hapati nafasi ya kuwa pake yake. Kwahio ni kuhusu timing kwamba ukizubaa napiga goli na kosa moja goli moja.

Fabian Delph nae atakuwa na kazi ya kumchunga Santiago Cazorla ambae atakuwa na majukumu ya kutafuta vyumba kwa wenzie akina Walcott na Ramsey au hata yeye kufunga. lakini Kwa sababu Delph nae ni mjanja na ana kasi itabidi Cazorla asipande sana mbele bali kubakia kati kumsaidia Francis Coquelin.
 
Namuomba Mungu wangu tushinde hii game!!...hawa watoto wa mchangani huwa hawaaminiki.
 
Arsenal huwa haichezi vizuri ndani ya Wembley. Tusubiri tuone itakavyokuwa leo.
 
Wenger ameanza na Theo Walcott ili kutafuta magoli ya harakaharaka kwa kuwa Walcott anakimbia khasa.
 
Duh! Rosicky hayupo hata sub, sijui kwann Wenger hamkubali. Good lucky to theo i hope he will score
 
Moyo unadunda damu kama vile imeganda mishipani, nerves hazifanyikazi. Kaeni tayari kuita Ambulance.
 
Kikos kipo poa natumai leo sczeny hatazingua all in all kila la kheri kwa gunners woote. #COYG .
 
Back
Top Bottom