Umeona eeh!
Cheka bas NC wamepata la 2
Hahahahahahah lol! umefurahi au umenuna HC wanashuka daraja?
Yaani nimenuna mpaka nataka kupasuka acha tu nitumie Pepsi baridi nishushe hasira.........naona umefurahi sana.
Haya banaaa pole kwa kununa ila usipasuke bado unahitajika kwa miaka mingi tu ijayo. Kitu kingine
sikutaka wale NC washuke nadhani ndio timu pekee EPL yenye wacheza wengi toka Africa ukilinganisha na timu yoyote ile.
Hahahaha!! Hiyo sababu ya mwisho imenifanya nitabasamu nipotezee machungu..... Mbona hatualikani tarehe 30 au unahisi Villa atakuchapa?
Unakaribishwa sana kama unakuja kutushangilia tukiwachapa wale Aston Villa lakini kama unataka kuja kutunanga 🙂🙂 cheza mbali na hili jukwaa 🙂🙂 chungulia kwa mbali tu. Nimeambiwa nawe ulikuwa damu damu ni Arsenal lakini kukosekana kwa makombe ndiyo ukahamia nanihii, makombe sasa yameanza kurudi karibu tena nyumbani binti mpotevu 🙂🙂
Hahahahahahaha!!!! Ninepe Everlenk mie eti unasemaje!!!!......bila hiyana nitakuja kuwashangilia sana tu tena sana si unanijua eeh!!....lakini nakuhaidi niko kama kinyonga mkifungwa nitawaruka fasta kama siwajui 😀😀😀😀
Hilo la kufungwa sahau kabisa timu iko bomba sana lakini ukija kwa nia ya kutunanga huku tunamchapa mtu ni bora tu uondoke, mie sitatia neno lakini kuna Gunners wengine utakoma ubishi mwenyewe wakianza kukuita majina mabaya yote ya humu ndani hahahahahaha ikiwemo #msagasumu, #mburukenge n.k. lakini aisee kuna wakati huwa nacheka sana watu wakianza kuchachurana huku kwenye sports dah!