Chifu, mimi siyo mchumi, ila naomba unielimishe hapa.
Man United ina utajiri kuliko Arsenal. In fact, ni klabu tajiri ya 3 duniani kwa vilabu vya soka. Na mwakani itaanza kufahudu a 75M Quid kit deal na Adidas (a world record breaker).
Sasa, kwa maelezo yako unaonyesha kuwa Arsenal wana purchasing powers kuliko United ama?
Akaunti ya Arsenal imetuna kuliko ya United?!
Nielemishe chifu.
Mkuu usije ukawa ulikuwa umewaza labda nimekimbia, la hasha nilikuwa nashughulikia mambo yangu ya ujasiri mali pamoja na kutfuta few facts kuhusu hizi timu mbili.
Hapana simaanishi kwamba kuna tofauti ya kutuna kwa akaunti kati ya timu hizi ila ni kiasi gani cha deni kinaweza kuathiri matumizi ya kwaida kama kununua wachezaji.
Pia ni kweli Man Utd ni klabu tajiri ya tatu duniani ni hiyo ni kutokana na jina lake na kwamba hiyo Corporation ni Asset yenye thamani kubwa.
Arsenal nao wana deal la paundi milioni 300 kutokana na ufadhili wa Puma ambazo wanaweza kumaliza kabisa matatizo madogomadogo.
Haya tuendelee.
Deni la uwanja ambalo Arsenal ilikopa benki ili kujenga uwanja likikuwa kwenye paundi milioni 300 hivi.
Niliposema Arsenal wana "disposable income" ni kwamba wana uwezo wa kutumia pesa ambayo iko kwenye "cash reserve" pesa ambayo imetokana na mapato makubwa ambayo ni jumla ya paundi milioni 298.7.
Katika hii milioni 298.7 kuna pesa inayotokana na mapato ya uwanjani milioni 100.2 kwa kila mechi na uwanja unapojaa yaani watu 60,000 na ushei hivi, pesa inayotokana na matangazo kwenye telly paundi milioni 120.8 na milioni 77.7 zinatokana na mauzo ya jezi na mambo mengine au tunaita "commercial revenue".
Arsenal inalipa mishahara jumla ya paundi milioni 166.4 ambayo ni asilimia 66 ya mapato yake.
Kwa hio mapato mazuri yanaziba deni kiasi cha kuweza kusajili wachezaji kama Mesut Ozil (42 milioni) na Alexis Sanchez (35 milioni)
Man Utd wana deni kiasi cha paundi milioni 342 ambazo familia ya Glazer ilikopa kwenye mabenki kwa niaba ya Man Utd yaani walikopa kwa kutumia Man utd kama Asset yao kujikinga na deni.
Mapato yote ya Red Devils ni jumla ya mlioni 433.1 , kila mechi moja inaingiza milioni 108.1, deals za telly ni 135.7 na commercial revenue ambayo ndio njia kuu ya mapato ni paundi milioni 189.3
Katika mapato hayo unatoa mishahara milioni 215 ambazo ni asilimia 50 ya hayo mapato na kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha mapato timu hii bado inaweza kusajili wachezaji kama Angel Di Maria ambae aligharimu paundi milioni 59.7.
Isitoshe Man Utd wanalipa mishahara mikubwa kwa Wayne Rooney na Robin Van Persie ambayo ni zaidi ya paundi milioni 250,000 kwa wiki.
Isitoshe wakati wa kiangazi mwaka jana walikwenda tena benki kuongeza deni kwa kuchukua paundi milioni 150 wazitumie kwenye usajili wa wachezaji unaowaona leo.
Arsenal waliandika tu hundi kwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez wasajiliwe, kwasababu wana "disposable income".
Kwahio "facts" ni kwamba Arsenal wana mapato mazuri yanayoziba madeni na kuweza kulimaliza mapema na pia kuweza kushindana kwenye usajili wa wachezaji, wakati Man Utd bado wana deni kubwa ( kumbuka akina Glazer wanaweza kusepa zao na kuachia Man Utd iuzwe kufidia madeni) na pia wanatumia asilimia 50 ya mapato yao kulipa mishahara.
Hizi Data nimezipata kutoka kwenye website ya Premier League.