Mkuu FFP Haizuii timu lununua wachezaji so kwa timu kama Chelsea au Man City kununua wachezaji hao wote kwa msimu mmoja siyo tatizo, tatizo ni kwamba hizo pesa zimetoka wapi??
FFP Inataka timu inunue wachezaji kwa kutumia pesa ambayo inatokana na mzunguko wa mapato mbalimbali katika timu yaani kama vile pesa ya matangazo, mauzo ya jezi, mikataba mbalimbali n.k inachokataza FFP kwa mtu binafsi kuja kutoa pesa zake kununua wachezaji kama ilivyo kwa kina Sheikh Mansour wanavyotoa pesa zao walizozichuma kwenye mafuta na kuziingiza katika timu na kuanza kulangua wachezaji.
Hivyo ndivyo ninavyoilewa FFP.