Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kumekucha, pamoja na kupata droo ktk mechi ya jana, kidogo nimefarijika maana tungekua na wakati mgumu zaidi iwapo tungepoteza hii mechi. Lazima tukubari kua tumekua na matokeo mabaya dhidi ya Man UTD kwa muda mrefu sana. Kuhusu ubingwa kweli bado itategemea mipango ya Mungu kwa maana timu ya ubingwa inatakiwa ishinde zile mechi ngumu hususani waliopo big four kwa kasi hii sidhani kama tutaweza kumpiga Chelsea au Man City.
We didnt spend "Big" in January...huenda ikawa ni sababu ya kuukosa ubingwa
 
article-2557998-1B706B1900000578-176_634x339.jpg
 
Mkuu una ushabiki wa ajabu!!!! Van persie aliwakosa mara tatu. Pamoja na kugongesha mwamba mara mbili, Bado tu huamini na nyie mliponea kwenye tundu la sindano?

Thanks Gunner.

what a terrible game!

Nilisema mapema kuwa, kuwakosa Aaron Ramsey na Theo Walcott ni pigo kubwa sana kwetu kwa sababu hawa walikuwa mpaka wanamfanya hata Olivier Giroud aonekane ni mshambuaji hatari wakati kiuharisia ni average player ambaye hawezi hata kwenda na playing style ya Arsenal. Slow, dreadful first touch, immobile....

Kukaa hapa na kusema tungeshinda hii mechi wakati hatujashinda ni kujifariji faraja ambayo haina impact yoyote katika uharisia.

Gosh, Sijawahi kuona timu mbovu kutokea katika viunga vya mitaa ya Sir Matt Busby Way, Old Trafford kwa muda mrefu kama hii Man United ya mwaka huu lakini cha kushangaza ndiyo imeondoka kwenye viunga vyetu vya Emirates Stadium na point moja kibindoni kitu ambacho kwa Man United hii ni ushindi.

Ukiangalia na kuchunguza utagundua kuwa tulikuwa tunacheza mpira with fear of the unknown kama vile tunapambana na Man United ya Sir Alex Ferguson wakati wachezaji wa Man United pia walikuwa na wasiwasi mkubwa wa kufungwa as a result, Man United were excellent defending deep and in numbers,

Let's forget and move on kwa sababu kuna makombora Jumapili yako mbioni tena kushuka Emirates kutoka Merseyside saa 16:00 GMT kwa ajiri ya mtifuano wa FA CUP fifth round. Hata hivyo, nina uhakika hiyo mechi tutashinda.

Tukutane tena kwenye kijiwe chetu hiki Jumapili.

Once a Gunner, Always a Gunner.
 
Chu, ande goshi ulenamakoye.

Nhamala, Ule mhola kwenuko!.

Hujakumbana na Msukuma aliyeendelea ambaye anafunga redio kwente baiskeli kama car redio kwenye car dashboard!

Mimi pia nimeendelea kwa kiwango cha kuingia kwenye mechi za mpira na kushuhudia kabumbu badala ya kushuhudia mashindano ya ngoma ja bhagalu na bhagika wakati wa kiangazi.

Unenhe nale ngika.


Sasa Umekosea! Ungeshabikia li Chelsea la Mourinho kuliko Hiyo timu ina ukame Wa makombe!
 
Sasa Umekosea! Ungeshabikia li Chelsea la Mourinho kuliko Hiyo timu ina ukame Wa makombe!
Sitaki hata kulisikia hilo Lichelsea.

Wewe endelea tu kulishabikia huku nalo likiendelea kununua vikombe mbali mbali.
 
Sitaki hata kulisikia hilo Lichelsea.

Wewe endelea tu kulishabikia huku nalo likiendelea kununua vikombe mbali mbali.


Sasa Wewe unashabikia li timu lenye jezi nyekundu badala ya ya buluu km zile nguo zetu za machungani!

Utapigwa radi ukivaa nguo nyekundu machungani!

Chelsea ndio bingwa!
 
Yaani haiingii akilini Manchester hii ambayo timu kama Stoke city na Fulham wameigeuza kichwa cha mwendawazimu kwa kujifunzia kunyoa eti inakutana na timu mzuri kama Arsenal tena tupo nyumbani alafu tunadroo!!? Kweli hii ni haki?
Kwa upuuzi huu ubingwa tutaendelea kuusikia na kuusubiria hadi masiyah aka Jesus atakaporudi Duniani(kama ni kweli)

its time wenger to correct his mistake he has to make sure this coming summer transfer he buy atleast one super striker whatver the cost otherwise ubingwa msahau mpk wenger atakapoondoka arsenal
 
Sasa Wewe unashabikia li timu lenye jezi nyekundu badala ya ya buluu km zile nguo zetu za machungani!

Utapigwa radi ukivaa nguo nyekundu machungani!

Chelsea ndio bingwa!
Hilo halina tatizo hata kidogo. Nikiyavaa sikai karibu na mti wakati nikiwa machungani!.

Litimu gani hilo lina kiwanja kwenye sehemu ya matajiri matajiri utadhani washabiki wake wote ni matajiri wakati wengine ni wakulima wa pamba na mahindi Kama kina Ntuzu
 
Last edited by a moderator:
Hilo halina tatizo hata kidogo. Nikiyavaa sikai karibu na mti wakati nikiwa machungani!.

Litimu gani hilo lina kiwanja kwenye sehemu ya matajiri matajiri utadhani washabiki wake wote ni matajiri wakati wengine ni wakulima wa pamba na mahindi Kama kina Ntuzu


Ha ha ha ha haaaaaa!

Bahebu ahene onepandeka sn!

Ndio timu Nzuri Hiyo! Ata mashabiki wake harufu ya hela inakua inawanukia!

Wewe timu yako eti lighala la silaha nawakati Ng'wamapalala kumejaa mishale tu!
 
Last edited by a moderator:
acha povu wewe,hujui kuwa hawa walibeba ndoo za kutosha?acha kujitoa fahamu

Ndoo za kutosha ukiwalinganisha na Gerrard ama? Kwa sababu, hata ukiwajumuisha hao wote bado hawamfikii Giggsy...infwakti, Giggsy amebeba makombe ya EPL sawa na yale ya goons katika historia ya goons...
 
Sasa Umekosea! Ungeshabikia li Chelsea la Mourinho kuliko Hiyo timu ina ukame Wa makombe!

Tulia wewe mnyantuzyu kule uliko wewe ni Genge tu la watu wenye interest ya aina 1 walijikusanya eti na wao wakajiita timu.
 
Mkuu una ushabiki wa ajabu!!!! Van persie aliwakosa mara tatu. Pamoja na kugongesha mwamba mara mbili, Bado tu huamini na nyie mliponea kwenye tundu la sindano?
Kutukosa mara tatu au saba hakuwezi kuondoa ukweli wa mchezo kwa jinsi ulivyokuwa umepangwa na mameneja wa timu mbili.

Hiyo hoja yako haisimami kwenye Man United ya zamani kabla ya Moyes. Hii ya sasa inacheza mpira wa smash-and-grab.

Kila timu haikutaka kupoteza point kwa maana nyingine kila timu ilikuwa inacheza kwa uwoga kutokana na matokeo ya weekend as a result, hata mechi ilikuwa hata haivutii kuiangalia. No movement.

Man United is terrible and is there for the taking while Arsenal team was playing with fear for unknown.
 
Vijana walicheza wakiwa na hand break mkononi haina shida ..... ...... ........... kitaeleweka tu huko mbeleni ..... ... .. COYG



article-2558750-1B77C14200000578-105_964x347.jpg



Morinyo ameanza kuweweseka .... .... ......



article-2558448-1B6F965E00000578-113_634x535.jpg


No way past: Wojciech Szczesny pulled off a stunning save
from Juda Iskariot on Wednesday





article-2558448-1B6FAD9D00000578-873_634x379.jpg



Point blank: The Arsenal keeper tipped a header
from Manure's striker onto the crossbar

 
Back
Top Bottom