Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

TRANSFER UPDATES

Wakuu goodmorning,

Habari za usajili wa mshambuliaji kwa timu yetu ya Arsenal zimepamba moto lakini maskauti wapo busy sana na Ivan Gazidis na mwenzie Dick Law ambao ndio wataalam wa kuzungumza biashara za usajili baada ya kuagizwa na mzee Wenger, bado wanazungumza na Real Madrid kuhusu Morata.

Kuna kila sababu kwamba deal la paundi milioni 2 linaweza kufanywa ili Morata aende Arsenal kwa miezi 6 ili apate uzoefu zaidi kutokana na Morata mwenyewe kupendelea option hiyo badala ya kuhama kabisa.
1000x7356.jpg

Alvaro Morata

Wapo nchini Spain na pia maskauti wameulizia kuhusu mshambuliaji mwingine Jackson Martines ambae ni mColombia kuhusu availability yake pale Porto nchini Ureno kama option endapo deal la Morata litashindwa.

Kuna kila dalili kwamba deal la Morata lina usumbufu ukizingatia pia habari kwamba baadhi ya timu za PL zimeingia kwenye mchakato wa kumsajili mchezaji huyo na moja ya timui hizo ni Liverpool.

Lakini "penye udhia penyeza rupia"

COYG!
 
TRANSFER UPDATES

Wakuu goodmorning,

Habari za usajili wa mshambualiaji kwa timu yetu ya Arsenal zimepamba moto lakini maskauti wapo busy sana na Ivan Gazidis na mwenzie Dick Law ambao ndio wataalam wa kuzungumza biashara za usajili baada ya kuagizwa na mzee Wenger, bado wanazungumza na Real Madrid kuhusu Morata.

Kuna kila sababu kwamba deal la paundi milioni 2 linaweza kufanywa ili Morata aende Arsenal kwa miezi 6 ili apate uzoefu zaidi kutokana na Morata mwenyewe kupendelea option hiyo badala ya kuhama kabisa.
1000x7356.jpg

Alvaro Morata

Wapo nchini Spain na pia maskauti wameulizia kuhusu mshambuliaji mwingine Jackson Martines ambae ni mColombia kuhusu availability yake pale Porto nchini Ureno kama option endapo deal la Morata litashindwa.

Kuna kila dalili kwamba deal la Morata lina usumbufu ukizingatia pia habari kwamba baadhi ya timu za PL zimeingia kwenye mchakato wa kumsajili mchezaji huyo na moja ya timui hizo ni Liverpool.

Lakini "penye udhia penyeza rupia"

COYG!

Tunashukuru kwa taarifa nzuri mkuu!
 
BREAKING NEWS

MORATA HUENDA AKAJA ARSENAL MWISHO WA MWEZI- NI KWA MKOPO TU HADI MWISHO WA MSIMU WA 2013/2014
AlvaroMorata1.jpg

ALVARO MORATA

Timu ya Real Madrid leo wameamua kusikiliza maombi ya wawakilishi wa Arsenal na kwamba huenda wakamruhusu mshambuliaji huyo kwenda Arsenal kwa mkopo tu na sio moja kwa moja.

Habari za uhakika kabisa kutoka mji mkuu wa Madrid zinasema kwamba wawakilishi wa mchezaji huyo na wale wa Real Madrid walimzunguzia Morata na kuona kwamba kuna umuhimu wa kumruhusu mchezaji huyo aende Arsenal kwa mkopo ili kuongeza uzoefu.

Baada ya hapo likazungumzwa suala la ada ya usajili wa muda na masharti ya mkataba huo wa muda na ikakubalika kwamba kama kila kitu kikienda sawa basi mchezaji huyo anaweza kuingia kwenye ndege (pipa) na kuwa London ndani ya saa mbili tu.

Arsenal wanahitaji mshambuliaji kutokana na Theo Walcott na Nicklas Bendtner kuumia hivyo kuwepo hitaji la mshambuliaji mwingine kama back up na pengine kuingia kabisa kwenye first X1.

Nae Morata amekuwa akidhoofika kisaikolojia kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kwenye timu yenye washambuliaji wengi wenye vipaji kama Ronaldo, Bale, Angel Di Maria na hususan Karim Benzema ambae sasa amekuwa akifungia magoli timu yake kwa ushirikiano mkubwa na Ronaldo na Di Maria.
 
kwa mtazamo wangu hii gemu ya leo ndiyo itakayoamua nani wa kuchukuliwa, ikiwa timu haitotetereka nahisi umuhimu wa kununua mchezaji hautokuwa mkubwa
mambo yote hayo ninayafikiria tu mwenye uamuzi wa mwisho ni Arsene Wenger
 
Wenger anaendeshwa kwa matukio....We angalia signings zake nyingi ni kwa baada ya panic na presha kubwa. Players like Arteta, Per Mertasacker, Ashavin, Ozil...yani baada ya matokeo mabaya ndio jamaa anasajili. Mi naona gemu hii tushinde lakini ile ya wiki moja before the window closing tupoteze....hata hii mechi tukipoteza si mbaya ila itampa presha Wenger ya kusajili.
 
Ungesema lipuli au ujenzi rukwa sawa we mbwa nani anakujua England?unahisa weweee?mbururaaq
 
Back
Top Bottom