Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

lol!!! Wacha wasikie tu halafu namuona huyo Defoe anafunga viatu vizuri kuja kujaribu bahati yake...huyu ni mbaya sana anapokuwa maeneo ya hatari.

BAK .....Wasikusikie Watu wa Man Utd
 
Tottenham wamemwingiza Jermain Defoe badala ya Moussa Dembele na wanarudi kucheza mtindo wa 4-4-2 hivyo Defoe anacheza mbele na Soldado.
 
Ni kweli Mkuu...lakini Mhhhh! Si umeona hilo shambulizi la nguvu golini kwetu...mie moyo karibu usimame 🙂

Hahahaha.....
Kanauma japo kamoja!
 
Monreaaaaaaal ambae anaingia anakosa goli la wazi kabisa!
 
Nacho Monreal ameingia kuchukua nafasi ya Thomas Rosicky na atacheza mbele ya Kieran Gibbs kumdhibiti Sandro upande wa kushoto.
 
Sie bwana hatununui wachezaji ovyo ovyo, or we should we say ki "tots tots...."....
 
Olivier Giroud anaonekana amechoka na huenda akatoka.

Wenger amuingize Yaya Sanogo.
 
Dakika 5 zimeongezwa juu ya zile 90

Na Theo Walcott anatoka na Bacary Sagna anaingia.

Sagna anakwenda kucheza nafasi yake ya beki wa kulia na Jekinson anaziba nafasi ya Theo walcott na anakuwa mshambuliaji.
 
Tutanunua lakini sio kiholela namna hii...jamaa wako kama ndio wameonana leo, hakuna balance kabisa kwenye team yao...

Hata wakipata draw ni bahati kabisa.

Hiko kikosi thamani yake ni karibia £110....Unbelievable
 
Back
Top Bottom