Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,484
- 4,821
Nadhani ni aina ya uondokaji wa wachezaji wenyewe ndo huwa inawaumiza wadau wenzangu wa Gunners,wengi huondoka kwa sababu ya maslahi duni ndani ya Arsenal(kitu ambacho kuna kipindi mimi huwa nawaunga mkono)...Hata ningekuwa mimi,najiona kabisa nina mchango kwa timu na ndiye injini ya timu(mfano Song) nalipwa Pauni elfu 50 wanakuja Barca na dau la elfu 80 kwa kweli siwezi kulaza damu.......Lazima nitaondoka maana mpira ndo kazi yangu nammfanyakazi yeyote yule huangalia wapi kuna maslahi mazuri....Tusiwaone wachezaji ni wasaliti kwa kukimbilia sehemu zenye maslahi mazuri na kuwaita majina ya ajabu ajabu.....Tukae chini na kuangalia tatizo liko wapi.....Tujiulize kwa nini kila siku/msimu ni Arsenal tu?, 'Why always Arsenal'?....Jirani mambo vipi.
Najua kabisa Walcott kiwango chake kimedumaa, hata mimi ningemwambia aondoke....Tatizo langu ni huu utamaduni unaojitokeza kwa baadhi ya washabiki especially wa Arsenal, wanakuwa wakali kupita kiasi kwa wachezaji walioondoka Arsenal. Utakuta mtu anaongelea mapungufu tu bila kuonyesha kwamba yule mchezaji alitoa mchango wowote alipokuwa Arsenal. Mapungufu haya hayasemwi wakati mchezaji hajaamua kuondoka. Kwanini tusijifunze kusema "ahsante kwa mchango wako kwenye club na tunakutakia mema huko uendako"....huu ndio ustaarabu. Kumbuka mchezji ni binadamu kama walivyo wengine, anazo haki zote za msingi ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi kuhusu career yake.
Kuna siku nilisema kwamba "Tatizo ni mfumo wa ulipaji mishahara uliopo Arsenal.....Wachezaji wengi wanaondoka Arsenal kwa sababu ya mishahara duni ukilinganisha na timu nyingine.......Bodi ya Arsenal inapaswa kubadilika na kubadili mfumo wa ulipaji mishahara,tofauti na hapo Arsenal itaendelea kuwa feeder club kila mwaka......Kazi yetu itakuwa ni kutengeneza wachezaji na kuwajengea umaarufu na kuwauza hivyo habari ya vikombe itabidi tusahau......
AW hapaswi kulalamikiwa katika hili la wachezaji kuondoka,anapaswa kuonewa tu huruma......Wa kulalamikiwa ni board wa Arsenal........
Najivunia kuwa Mshika Bunduki.........
Once a Gunner, always a Gunner......
Gunners for life...................No matter what....."