Ardhi sio uwekezaji kwa mtu anayejitafuta

Mkuu kutafuta hela hakuna kituo maana tunaandika hapa kana kwamba mtu akipata hela yake kidogo basi atakuwa ameji-limit kwamba asiendelee kufanya kile alichofanya kikampa hiyo hela eg ajira,winga au udalali basi atoke akaanzishe biashara,ila tujue pia kwamba kwenye biashara kadiri mtaji unavyokuwa mdogo ndivyo inavyompa ugumu mmiliki kuiendesha na kuwa failed.

Hata wengi walionunua hizo ardhi na leo wanaziuza kwa bei kubwa hawakuwa na lengo la kuziuza au hawakujua zitakuja kuwa na thamani kubwa kiasi hiki sababu hawakuzinunua kibiashara,my point is mtu akipata hiyo mill 4,(sisemi 20mil sababu huo tayari ni mtaji japokuwa kama anahisi hana idea sahihi ya biashara bora na yenyewe akaitia kwenye ardhi) aiweke kwenye ardhi huku akiendelea kujazia mtaji siku akiona anaweza akafanya kitu akauze kiwanja ajazie afungue biashara kuliko kulazimisha biashara na mtaji mdogo.
- cha muhimu mimi naona ni kufanya diversification tu, yaani unanunua ardhi, unaweka kidogo Utt, unakuwa pia na biashara like tigopesa/mpesa/airtel money,
 
Habari zenyu wana JF

Kwa mtazamo wangu naona ardhi sio kitu cha kukimbilia kununua kwa kijana anayejitafuta kwani ni kama kuzika hela ambayo kama ukiwekeza kwenye kitu kingine ingekuwa na tija zaidi.

Huo ni mtazamo wangu , wewe waonaje ?
Wewe umewekeza kwenye nini huko unapata faida
 
Mara nyingi huwa naamini wenye mawazo kama haya hawajawahi kufanya biashara kwani biashara ni ngumu sana,kuzungusha hela izae hela na iwe endelevu siyo kazi ndogo ni nusu uwendawazimu ndiyo maana watu huwa wanaamua kiasi fulani cha pesa wakiweke kwenye ardhi kama backup kwa sababu ndiyo kitu pekee kisichopungua thamani kiwepesi.

Ninapoishi jirani kuna mwenzangu tulinunua wote mwaka 2008 mimi nililipa Tsh 3mill na point yeye sijui ilikuwa bei gani but juzi Feb alinitangazia anauza offer yake ilikuwa 70mill mnunuzi aliyepatikana akampa Tsh 63mill,Goba nina jamaa yangu alinunua ardhi chini ya 4mill mwaka 2011 mwaka jana mwishoni akapauza kwa 50Mill,uwekezaji wa ardhi na nyumba unampa mtu guarantee ya kupata hela kesho wakati mwenye biashara anaweza akakosea kidogo hesabu akaamka na tra wakamfilisi akarudi zero.
2023 nimenunua ardhi shamba kwa tsh 33 Million asah hv nauza kwa kwa tsh 100 million mteja kapatikana

Kuna eneo nilinunua kwa tsh 40 million 2019 juzi hapa wachina wamefika kwa 250 million ila sijauza kwani nina project nalo

Ardhi ni uwekezaji mzuri kwa mtu ambaye hana muda wa kufanya biashara
Mfano mtumishi wa umma
 
Sahihi mkuu, mwaka huu nimekula hasara ya Milioni 8 kwenye biashara. Najiuliza hiyo pesa ningepeleka kwenye mashamba huko Songwe ndani ndani ningechungia hata ng'ombe.
 
2023 nimenunua ardhi shamba kwa tsh 33 Million asah hv nauza kwa kwa tsh 100 million mteja kapatikana

Kuna eneo nilinunua kwa tsh 40 million 2019 juzi hapa wachina wamefika kwa 250 million ila sijauza kwani nina project nalo

Ardhi ni uwekezaji mzuri kwa mtu ambaye hana muda wa kufanya biashara
Mfano mtumishi wa umma
Uko correct sn zaidi ya sn me naona ardhi kwa mtu ambae hana uzoefu wa biashara n nzuri sn na kama umebahatisha hela hujawah fanya biashara yyte n bora ukawekezavkwenye ardhi mana ukiingia kwenye biashara n ngumu kutoboa biashara inataka ile unaanza mdogo mdogo mwisho wa siku inakuwa sio leo hii umepata hela yako ya urithi ghaflauanzishe biashara hutoboi ndo mana wastaafu wengi wamefeli kwenye biashara
 
Mara nyingi huwa naamini wenye mawazo kama haya hawajawahi kufanya biashara kwani biashara ni ngumu sana,kuzungusha hela izae hela na iwe endelevu siyo kazi ndogo ni nusu uwendawazimu ndiyo maana watu huwa wanaamua kiasi fulani cha pesa wakiweke kwenye ardhi kama backup kwa sababu ndiyo kitu pekee kisichopungua thamani kiwepesi.

Ninapoishi jirani kuna mwenzangu tulinunua wote mwaka 2008 mimi nililipa Tsh 3mill na point yeye sijui ilikuwa bei gani but juzi Feb alinitangazia anauza offer yake ilikuwa 70mill mnunuzi aliyepatikana akampa Tsh 63mill,Goba nina jamaa yangu alinunua ardhi chini ya 4mill mwaka 2011 mwaka jana mwishoni akapauza kwa 50Mill,uwekezaji wa ardhi na nyumba unampa mtu guarantee ya kupata hela kesho wakati mwenye biashara anaweza akakosea kidogo hesabu akaamka na tra wakamfilisi akarudi zero.
Inategemea na sehemu ardhi ilipo na ukuaji wa mji pia ongezeko la watu.

Ukinunua ardhi Madongo kuinama na Nainjilinji hukoo, Hata ukae kwa miaka 100 thamani yake ni ileile tu.

Kwa Tanzania ardhi ina thamani sana kwenye baadhi ya mikoa tu ambako kuna ongezeko la watu.

Ardhi za huko vijijini labda ufanyie kilimo.

Ila uwekezaji wa makazi utasubiri sana.
 
Uko correct sn zaidi ya sn me naona ardhi kwa mtu ambae hana uzoefu wa biashara n nzuri sn na kama umebahatisha hela hujawah fanya biashara yyte n bora ukawekezavkwenye ardhi mana ukiingia kwenye biashara n ngumu kutoboa biashara inataka ile unaanza mdogo mdogo mwisho wa siku inakuwa sio leo hii umepata hela yako ya urithi ghaflauanzishe biashara hutoboi ndo mana wastaafu wengi wamefeli kwenye biashara

Cha msingi chukua taadhali kabla ya kununua ardhi
1. Fanya screening kujua matumizi yake mfano
makazi , shule au msikiti Hiyo kazi inafanya na surveyor mi huwa natoa hata 50,00 anachukua cordinate za enea na kwenda ardhi kucheki matumizi
2. Nunua eneo ambalo halina mgogoro
Huwa sinunue eneo la familia au urithi
3. Jitahidi uwe na documents halali baada ya kununua , mfano hati
 
ardhi ipi fafanua kwa maana shamba nalo ni ardhi
 
Cha msingi chukua taadhali kabla ya kununua ardhi
1. Fanya screening kujua matumizi yake mfano
makazi , shule au msikiti Hiyo kazi inafanya na surveyor mi huwa natoa hata 50,00 anachukua cordinate za enea na kwenda ardhi kucheki matumizi
2. Nunua eneo ambalo halina mgogoro
Huwa sinunue eneo la familia au urithi
3. Jitahidi uwe na documents halali baada ya kununua , mfano hati
Vipi suala la kununua ardhi mikoa tofauti na kujenga broh mfano nanunua dar najenga nanunua tabora najenga nanunua arusha ivo yaan au kununua sehem moja ukawekeza mm nna mpango huo wa kuwekeza kwenye ardhi biashara nimefeli sn
 
Habari zenyu wana JF

Kwa mtazamo wangu naona ardhi sio kitu cha kukimbilia kununua kwa kijana anayejitafuta kwani ni kama kuzika hela ambayo kama ukiwekeza kwenye kitu kingine ingekuwa na tija zaidi.

Huo ni mtazamo wangu , wewe waonaje ?
Kwa mtu yeyote,ni asset ambayo kwanza huwezi ibadili kuwa liquid Kwa haraka na ukilazimisha lazima uuze chini ya value yake.
 
Vipi suala la kununua ardhi mikoa tofauti na kujenga broh mfano nanunua dar najenga nanunua tabora najenga nanunua arusha ivo yaan au kununua sehem moja ukawekeza mm nna mpango huo wa kuwekeza kwenye ardhi biashara nimefeli sn
Hiyo ni nzuri kama utajenga sehemu ambayo ina
Vipi suala la kununua ardhi mikoa tofauti na kujenga broh mfano nanunua dar najenga nanunua tabora najenga nanunua arusha ivo yaan au kununua sehem moja ukawekeza mm nna mpango huo wa kuwekeza kwenye ardhi biashara nimefeli sn
well
Hiyo ni nzuri kama unajenga sehemu ambayo kuna hight demand ya nyumba ya wapangaji mfano kama gharama ya kujenga inarudi ndani ya miaka 5 sio mbaya

Kwani waweza jenga njumba kwa grarama kubwa then ukapanga kwa bei ndogo
Hela yako ina rudi baada ya miak mingi na nyumba isha anza kuchoka

Mfano kuna nyumba nimejenga kwa tsh 100 Million kodi yake nis sh 800,000
Maana yake hela inarudi baaday ya kama 10 years hv
Though kwa vizazi vyako vitanufaika
 
Ardhi sio uwekezaji kwa mtu anayejitafuta
Inategemea kazi ya mtu.
Kama upo kwenye ajira rasmi, uwekezaji kwenye ardhi ni chaguo bora zaidi, maana ukijiingiza kwenye biashara wakati huna muda wa kutosha kusimamia wala ujuzi juu ya biashara husika, watu utakaoweka kusimamia watakuliza vibaya.

Kwa ardhi unatakiwa tu kuwa makini wakati wa kununua usiingizwe mkenge. Ukifanikiwa kununua sehemu nzuri, ni suala la muda tu unapata pesa ndefu.

Vinginevyo kama huna ajira rasmi, jikite kwenye biashara
 
Uko sw ajira rasmi uwekezaji wake n kwenye ardhi tu hata wasanii siku izi unawaona wanawekeza sn kwenye ardhi biashara n kitu kinahitaji umakini sn na icho kitu kinahitaji ukianze ukiwa na umri mdogo ndo mana wenzetu wahindi na waarabu wanawarithisha watoto wao mapema leo hii mtu una miaka 35 au 40 uanze biashara kwenye 100 labda 10 tu ndo watafanikiwa biashara n process mtt wa bakhresa au wajaukuu wake n simple kutoboa ila sio mtu from no where uanzishe biashara unaweza pewa milion 100 ukafilisi zote halaf kuna mtu kapewa milion 5 akatoboa akazalisha iyo milion 100
 
Mara nyingi huwa naamini wenye mawazo kama haya hawajawahi kufanya biashara kwani biashara ni ngumu sana,kuzungusha hela izae hela na iwe endelevu siyo kazi ndogo ni nusu uwendawazimu ndiyo maana watu huwa wanaamua kiasi fulani cha pesa wakiweke kwenye ardhi kama backup kwa sababu ndiyo kitu pekee kisichopungua thamani kiwepesi.

Ninapoishi jirani kuna mwenzangu tulinunua wote mwaka 2008 mimi nililipa Tsh 3mill na point yeye sijui ilikuwa bei gani but juzi Feb alinitangazia anauza offer yake ilikuwa 70mill mnunuzi aliyepatikana akampa Tsh 63mill,Goba nina jamaa yangu alinunua ardhi chini ya 4mill mwaka 2011 mwaka jana mwishoni akapauza kwa 50Mill,uwekezaji wa ardhi na nyumba unampa mtu guarantee ya kupata hela kesho wakati mwenye biashara anaweza akakosea kidogo hesabu akaamka na tra wakamfilisi akarudi zero.
Wewe una akili sana. Nunua ardhi kwa kadri uwezavyo. Jitese miaka minne, mwaka wa tano utafurahia maisha.
 
Habari zenyu wana JF

Kwa mtazamo wangu naona ardhi sio kitu cha kukimbilia kununua kwa kijana anayejitafuta kwani ni kama kuzika hela ambayo kama ukiwekeza kwenye kitu kingine ingekuwa na tija zaidi.

Huo ni mtazamo wangu , wewe waonaje ?
Mi huwa, naamini, katika kuwekeza katika ardhi, nyumba, chakula, idadi ya watu inaongezeka, ardhi itahitajika Sana, cha msingi ni kuangalia unanunua wapi,
Ukinunua heka moja bukoba kwa laki, 5,na, ukanunua heka, moja Dodoma kwa milioni tatu, baada ya mwaka mmoja,heka ya Dodoma Ina thamani Mara 20,ya, ile ya Bukoba,
Hv unasemaje ardhi sio kitu cha maana,eti ni kuzika pesa,kama upo Dar, ukipita njia ya, Goba, au, madale Yale maflemu, maduka, apartments zilizojaa, zimejengwa hewani!?
Huyu IGP, wa sasa, nasikia amejenga apartment kibao Goba, za, ghorofa moja moja, alinunua kabla rami haijajengwa! Leo Je! Wenye akili ndogo ndio, huamini ardhi ni kupoteza pesa, sasa unataka vijana wakauze simu na cover sake kariakoo, au, nguo mwenge? Au,
 
-afande IGP alinunua zamani lakini, alikuwa na position nzuri sana kwa sababu alikuwa ofisa,
 
Mimi nakuunga mkono,asilimia mia moja,
sababu zangu hizi hapa
1.Watu wanaangalia thamani ya pesa unayopata baada ya hiyo ardhi kukaa miaka kadhaa,wakati huo kama huna mtu wa uhakika kukuangalizia hiyo ardhi kama ipo mbali nawe unapigwa na matapeli na kuikomboa kama utafanikiwa ni gharama kuliko pesa uliyonunulia hapa naongelea mahakama za ardhi ni majipu matupu.

Ikitokea ukaweka mtu wa kukuangalizia uwe tayari kumlipa kiasi chochote cha pesakwa mwezi,kwa bahati mbaya tukiuza kiwanja hizo pesa tulizotumia kutunza huo uwanja huwa hatukumbuki kizitoa ndipo tuhesabu faida.Hapo sijataja gharama za kwenda kutembelea kiwanja chako na kurudi ukiwa na chupa ya maji mkononi.

2. Sehemu za mashamba .ukiacha suala la matapeli,kuna matumizi ya ardhi,wewe unanunua ili ulime wakati unasubiria bei ipande,unakutana na mgogoro wa wakulima na wafugaji,hii ilinicost hata kwenye upandaji wa miti.

Ushauri wangu kwa anayejitafuta
ni heri hizo pesa weka UTT,faida yao ni ndogo lakini ni stress free.
Wewe kila siku unaangalia ongezeko kwa kutumia App yao.
Hapa naongelea wale ambao hawana elimu ya biashara,wenye elimu ya biashara wanaweza kuzalisha zaidi.

Kama umeamua kuwekeza kwenye ardi au nyumba za kupangisha .tafuta sehemu zenye mzunguko mzuri wa pesa siyo viwanja vya uswenkeni hapa unaweza kusema umewekeza.
Nami ni maoni yangu. Naongea kutokea kwenye uzoefu
Mimi nimeishavuka umri wa kujitafuta,nimeona nilichokiona kiwe postive au negative.
 
Ardhi ni uwekezaji mkubwa sana Mkuu ngoja nikupe mfano mdogo ndio maana bank huwa wanakubali bond ya ardhi kuliko mali nyingine yoyote.

Ila ipo hivi kama unataka kuhifadhi hela basi ihifadhi kupitia ardhi, elewa neno kuhifadhi, sababu hiyo hela itakuwa inaongezeka kupitia kuongezeka kwa thamani ya hiyo ardhi.

Pia, usinunue ardhi ukajenga nyumba ya kuishi wewe mapema, ujenzi ndio kitu kinarudisha watu wengi nyuma au kubaki pale pale. Hiyo hela ya kujenga sasa ndio nitakubaliana na wewe uipeleke kwenye biashara au hata bora ukanunulie ardhi nyingine utakazoziuza baada ya hata miaka 5.

Ardhi ni hazina kweli ila ujenzi wa nyumba ya kuishi kwa kijana ni upotevu wa hela.

Nunua ardhi uzifanyie mambo mengine sio ununue ardhi ujenge nyumba ya kuishi chapu chapu na huko ndio kuzika hela kwenyewe.
 
Back
Top Bottom