Niwekeze wapi kati ya hisa au ardhi?

Niwekeze wapi kati ya hisa au ardhi?

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
358
Reaction score
708
Siku mmoja tulipa mgeni kutoka wataalamu wa mambo ya uwekezaji akatuma elimu juu y uwekezaji wa hisa, bond nk kwa kweli ilikuwa ni elimu nzuri na niliweza kujifunza kitu.

Kitu ambacho nilibaini kila unapoitaji kupata elimu hakikisha unapata elimu kila maeneo ili uweze kujifunza na kupata maarifa ambayo mwisho wa siju yatakusaidia kufany maamuzi sahihi

Mtazamo wangu leo kama nina fedha ya kuwekeza nikipewa nafasi ya kufanya maamuzi nitawekeza katika ardhi kwa sababu kadhaa

Sababu ya kwanza
Idadi ya watanzani kila mwaka inazidi kuongezeka wakati eneo la ardhi ya Tanzania haliongezeke

Thamani ya ardhi inakuwa kila siku na ukuwaji wake unategemea eneo uliloko lakni sio rahisi ukanunua shamba milioni moja baada ya mwaka ukaliuz milioni moja au pungufu

Ardhi ni bidhaa pekee ambayo haiathiriki na mfumuko wa bei, mfumuko wa bei ukipanda au kushuka bado bei ya ardhi inakuwa juu

Ardhi ni raisi kuuuza kuliko kitu chochote ukiwa na eneo lako muda wowote

Bei ya ardhi inaamuliwa na mmiliki na sio beo ya sako, wakati bidhaa nyingi zinategemea bei ya soko

Mkuu wa mkoa wa Njombe anasema miaka ya nyuma wakati Mhe kikweta akiwa raisi wa madini Geita ilikuwa ni wilaya ya Mwanza na alisema na watu wa Geita kwamba wanunue maeneo na kipindi kile ardhi bei ilikuwa ni chee. Miaka 25 imepita kiwanja cha Geita Mjini unapata kwa bilioni.

Binafsi naungana nahoja ya Rc miaka 15 niliyopita mkoa wa Geit viwanja ambavyo vilinunuliwa milioni moja leo hii vinauzwa milioni 200 hadi 300 milioni, wasatani wa mara 200 au 300 wa bei ya kununulia

Niambie leo ni nani anaweza kununua hisa za milioni 1 miaka 15 zikawa na thamani ya milioni 200 , hakuna , mimi binafsi nakushauri ni bora ununue hicho kiwanja cha milioni 1 kuliko hisa ya milioni 1 utakuja kunishukuru badae
 
Hilo suala mbona halihitaji hata elimu ya shule ya msingi kutambua. Ardhi haiwezi zidiwa na hisa kwa mazingira ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom