Antony Lusekelo; Ni mtu wa Mungu? real Christian?

akili ku mkichwa
wajinga ndio waliwao.
watu bado na akili zao wanaenda mule
hebu aulizwe avue pete lake analovaa kama atafanya muujiza wowote.
 
Kwahiyo basi na sisi nyendo zetu zifanane na hao mataifa? kwamba na sisi tuwapende marafiki na kuwachukia adui zetu?

....jitahidi kupanua ufahamu wako mkuu, ninachomaanisha ni kuwa Mungu anastahili zazidi ya wachawi na waganga. Akili yako na hekima za kiroho lazima zikujulishe hili na wala si suala la kuwachukia watu...
 
Mkuu mimi mwenyewe huwa nashangaa sana hawa binadamu
Wanaofananisha neno la Mungu na Huduma za Baa au kwa
waganga..huu ni udhaifu mkubwa sana hasa kama ni wakristo...
 
Ndugu yangu Salimkabora, nakusalimu na nakutakia amani na upendo. Sisi wanadamu ni viumbe wa ajabu sana! Familia nyingi ambazo zinafaidika kwa namna moja au nyingine kutokana na vipato visivyo halali toka kwa ndugu na jamaa zao, mara nyingi huwa mstari wa mbele kuwatetea na kuwalilia ndugu au jamaa zao wanaposemwa kuwa ni wezi,kukamatwa na kufungwa au hata wanapouawa katika matukio ya wizi!

Kwa nini tunene yaliyo mema ya watu na kuacha mabaya yao gizani? Yesu alipoingia hekaluni na kukuta hekalu limegeuzwa sehemu ya kufanyia biashara na kuwa pango la wezi alikasirika,akapindua meza na kuwafungulia wanyama na ndege kisha akawafukuza wafanyabiashara nje ya hekalu! Kwa maana hekalu ni mahali patakatifu na si sehemu ya kufanyia biashara!

Malengo ya uanzishwaji wa makanisa mengi yamebadilika au kubadilishwa kwa makusudi ili kuwanufaisha wajanja wachache kwa kujifanya wanatoa huduma za kiroho kwa waumini wao huku wakijilimbikizia mali zitokanazo na sadaka,fungu la kumi na michango mingine!
Yesu alikuwa mwema hakuwa na dhambi hivyo ilikuwa ruhsa kwake kunyooshea wengine vidole hadharani; tena kumbuka alifanya hivyo ana kwa ana kitu ambacho hata wewe hukatazwi kumtokea Lusekelo ana kwa ana na kumuonya kwa upole mkiwa wawili peke yenu lakini si vyema kutangaza hadharani ubaya wake wakati unajua hata wewe si mwema; kwa maana hii hatutakiwi kuhukumu mtu juu ya neno lolote. Kama shida yako ni kuponya wanaopotoka kwa mahubiri yake toa neno pekee usimtaje mtu.
 
....jitahidi kupanua ufahamu wako mkuu, ninachomaanisha ni kuwa Mungu anastahili zazidi ya wachawi na waganga. Akili yako na hekima za kiroho lazima zikujulishe hili na wala si suala la kuwachukia watu...

Mimi nakupa maandiko wewe unacheua mapovu; tumetakiwa matendo yetu kutofanana na ya mataifa ndio mana hata uchezaji kwaya ni tofauti na bolingo za kawaida ninapoongea habari ya chuki na upendo kwa adui ni upana wa fikra ambazo wewe huna ndio mana hukuelewa namaanisha nini. Mataifa watawachukia adui lakini sisi tutakuwa tofauti kwa kuwapenda; mataifa watavaa vimini lakini sisi tutakuwa tofauti kwa kuvaa sketi zenye staha; waganga wanataka kuku na vyura lakini mungu anataka rehema na wala si sadaka. Ukilielewa neno hilo utakuwa umeelewa naongelea nini.
 
Wakati mwingine anatumia lugha kali mfano utasikia akisema wanawake ni 'washeji' na bahati mbaya sana nao utaona wanashangilia na akiwaambia sema EIMEEEN! wanajibu hivyo. Anajiona ndiye muhubiri sahihi na bora kuliko wahubiri wote na anawaponda sana wenzake kuhusiana na majina wanayotumia kujitambulisha kama mitume na manabii. Sijui anauhakika gani kuwa yeye ndiye yuko sahihi kujiita mchungaji, mzee wa upako mara tinga tinga, transfoma nk. Wakati mwingine unamwona kabisa anahubiri kwa ajili ya kumlenga mhubiri fulani na akionesha wazi kuwa na chuki na hasira na yeye. Nadhani mafanikio ya utajiri alionao kutoka kwa waumini wake ndiyo yanayompa kiburi cha kujiona yeye ni bora na sahihi zaidi
 
Nilikuwa sehemu muda si mrefu,
Kulikuwa kuna kipindi kwenye runinga showing kipindi cha dini..

Nimeshangaa sana kuona aina ya dini inayofanywa na huyu jamaa!

Mnaoabudu pale huu utaratibu wakumtunza jamaa pale mbele kama
Mpo kwenye shoo za tangwa inakuwaje?
Tuelimishane

Kwani kuna watu wa Mungu siku hizi?dini siku hizi imeshakuwa ni biashara kama biashara nyingine ndio maana tuna viongozi /wenye makanisa mabilionia na wakiishi masiha ya kama mfalme wa Brunei au masheikh wa uarabuni,shauri yenu mnaoenda kuwaabudu hao mashetani
 
unaruhusiwa kusimama katikati ya mafundisho na kupeleka pesa mikononi mwake! what is this men!!
wafundishwaji wataelewa nini na mfundishaji concentration yake lazima iwaze nani analeta tena! badala ya kuendelea na somo..
Tena mkuu ukimpa lazima aitazame kwanza, nafikiri ikiwa ni mia tano lazima akurushie tu, lakini ikiwa Wekundu wa msimbazi utasikia, "Ahsante braza au Ahsante mama".
 
Yesu alikuwa mwema hakuwa na dhambi hivyo ilikuwa ruhsa kwake kunyooshea wengine vidole hadharani; tena kumbuka alifanya hivyo ana kwa ana kitu ambacho hata wewe hukatazwi kumtokea Lusekelo ana kwa ana na kumuonya kwa upole mkiwa wawili peke yenu lakini si vyema kutangaza hadharani ubaya wake wakati unajua hata wewe si mwema; kwa maana hii hatutakiwi kuhukumu mtu juu ya neno lolote. Kama shida yako ni kuponya wanaopotoka kwa mahubiri yake toa neno pekee usimtaje mtu.

We preach what we can not practice!
 
...nooo, mimi si mshirika wake lakini, sioni dhambi kumtuza mtu kama moyo wako umefurahi. mbona huko kwenye disco mnatoa au na huko ni wajinga..? anyway mtazamo mpana kwanini mkiambiwa kupeleka mbuzi kuku na hata kitu cha thamani kwa waganga/wachawi wa kienyeji mnatii bila maswali, je si zaidi kuwapa watumishi wa Mungu....???!!
Ama kweli wewe ni mshirika,hii ni mara ya kwanza kusikia staili ya aina hiyo duuu!!!na wewe unaitetea???nami ni mpetekoste yaani unajaribu kulinganisha na mganga wa kienyeji!!!!tafakari kwanza usiende pupa,mwisho wa siku utakuja yasema mengi hapa,hizo ni taarabu tuu.
 
mdogo wangu kuwa makini na viongozi wa ki'imani...itakughalimu; kama kitu unashaka nacho mara... nyingi huwa wanaweka namba zao za simu mpigie moja kwa moja muwasiliane nae na utapata jibu la uhakika kuliko kumuanika humu huwezi jua mawazo ya wengine yatakuwaje pengine anaweza kukashfiwa kitu ambacho hakitakuwa chema kwa maisha yako kwa siku za usoni.
 
Ngoja nitoe copy kidogo..
Mr Rocky, Arushaone, Mamndenyi.....
magari yenu mliyapataje?

Wengi wanamfuata kwasababu ya imani au zile nguvu za Nigeria? Kakobe kawachukulia hadi kawa tajiri.
Wajinga ndo waliwao siku zote,,endeleeni kumchangia sadaka mjanja wenu abadilishe Hummer kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Wengi wanamfuata kwasababu ya imani au zile nguvu za Nigeria? Kakobe kawachukulia hadi kawa tajiri.
Wajinga ndo waliwao siku zote,,endeleeni kumchangia sadaka mjanja wenu abadilishe Hummer kila siku.

na wenyewe si huwa wanashuhudia kuwa wameyapata hayo ma hammer
 
mdogo wangu kuwa makini na viongozi wa ki'imani...itakughalimu; kama kitu unashaka nacho mara... nyingi huwa wanaweka namba zao za simu mpigie moja kwa moja muwasiliane nae na utapata jibu la uhakika kuliko kumuanika humu huwezi jua mawazo ya wengine yatakuwaje pengine anaweza kukashfiwa kitu ambacho hakitakuwa chema kwa maisha yako kwa siku za usoni.

sidhani kama ni mimi hapa
 
Back
Top Bottom