Sisi sote ni watu wa Mungu kwa maana Biblia yatuambia tumeumbwa kwa mfano wake! Anthony Lusekelo hana tofauti na Kibwetere au Kakobe na wengine wa namna hiyo! Dini ni imani inayoweza kukufanya kuwa huru na mambo ya kidunia au kukufanya mtumwa wa mambo hayo! Kwa imani hiyo hiyo tumwombe Mungu atupe hekima na busara ya kuweza kumjua,kumtumikia na kumwabudu.
Mungu hana shida ya majumba ya kifahari au magari ya kifahari wala sadaka au fungu la kumi. Mungu hali wala hanywi. Inasikitisha kuwa tumekosa hekima na busara ya kuitambua na kuijua kweli! Matendo mema ya mtu ndiyo yakayomfanya kuwa karibu na Mungu na hata kuuona ufalme wa Mungu na wala si kwa kutoa sadaka kwa kumpa nabii au mtume wa uwongo.
Biblia inatuambia tukeshe tukiomba na wala tusikeshe tukidanganya watu na kujinufaisha kwa sadaka kwani saa ya kuja mwana wa mtu haijulikani,atakuja kama mwizi na kuwachukua walio wake! Makanisa ni sehemu ambazo zilitakiwa kuonekana takatifu kwa kuabudia,lakini zimegeuzwa na kuwa ni sehemu za kufanyia biashara ama mapango ya wanyang'anyi!