Antony Lusekelo; Ni mtu wa Mungu? real Christian?

Antony Lusekelo; Ni mtu wa Mungu? real Christian?

mmmmmhhh.......nalo neno ngoja niendelee kukomaa pale pale nilipo mweee.........:disapointed:
 
Usishangae hilo tu, account ya michango ya kanisa kupitia M pesa inapitia kwenye NO yake mwenyewe ya simu ya mkononi.Mimi Ni Mkristo lakini kamwe sitajiunga na makanisa haya ya wokovu, wachungaji Hawa ni watu wabaya sana wamekimbia kwenye Makanisa Mazuri yenye kumuabudu Mungu kwa sababu ya uroho wa madaraka na fedha na kuanzisha makanisa yao binafsi.
Makanisa ya namna hii yamejikita kwenye kuhubiri utajiri na kusahau kabisa kuwafundisha waumini wake wamjue mungu, yawapasa kuwafundisha watu wamfahamu mungu na kuhusu utajiri mungu mwenyewe ataamua kukupa utajiri au la.

Hujui ulisemalo! Dini zenu zenyewe ndo balaa zaidi. Hakuna neno la uzima! Ni kujifunza yaleyale yaliyo kwenye litrugia dunia nzima! Wachungaji wenu wakiendesha magari halali kwao, lakini wengine wakiendesha magari nongwa. Ndo udhihirisho kuwa mna roho ya namna nyingine!
 
Wanaotoa pesa ni wengine ww povu linakutoka huo wote ni wivu tu,mtu anakwenda kumtunza kwa kuwa jamaa anaongea point za maana na hata kichwa kinafunguka unawaza mambo ya maana ndo maana kama unafuatilia kipindi huwezi ona mtu analala kila mtu anachangamka na kuimba
 
Nilizaliwa mkatoliki na ntafia kwenye ukatoliki. I wanna know less about these other mushrooming churches. Kinachoendelea humo anakijua huyo anayejiita nabii, mtume, askofu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Huyu ni tapeli kama matapeli wengine. Kwa Lusekelo watu wanaenda Showroom ya magari. Hiyo ni dini ya magari. Naulizia, ili nipate Benz nimtuze Lusekelo sh ngapi?
 
Lusekelo Ni mtumishi wa mungu, lakini kutunzwa pesa walianzisha waumini Wenyewe miaka ya 2007 hivi nasikia ,sasa mzee wa upako akaona isiwe tabu wacha azipokee. Swala hapo ni utaratibu, maana maandiko yanashauri utaratibu tukiwa Ibadani pamoja ili ata asiyeamini aamini mungu Yu katikati. Kwa kuwa Mungu si Mungu wa machafuko. Kutoatoa pesa wakati mtumishi anaongea kunapotesa umakini kwa wanaosikiliza,Mimi pia nisingependa wakati message inaniingia najenga hoja halafu watu watatu wanapeleka hela itabidi asite kwanza. Ata madarasani ,nondo zinashuka alafu mtu anaenda kwa lecturer anaomba kwenda kukojoa inaharibu flow
 
Nilikuwa sehemu muda si mrefu,
Kulikuwa kuna kipindi kwenye runinga showing kipindi cha dini..

Nimeshangaa sana kuona aina ya dini inayofanywa na huyu jamaa!

Mnaoabudu pale huu utaratibu wakumtunza jamaa pale mbele kama
Mpo kwenye shoo za tangwa inakuwaje?
Tuelimishane

Intelijensia ya polisi inabidi ihamie kwake kwani ni mchumia tumbo.
 
Utaratibu gani tena mkuu? Utaratibu ndio huo yani unanyanyuka kwenye kiti unaenda mbele kumpa kaisar kilichochake kisha unarudi kukaa usibirie miti yako izae hela.

mkuu lusokelo ni tapeli wa akili za watu,anacheza na saikolojia tu hana lolote.
 
Wanaotoa pesa ni wengine ww povu linakutoka huo wote ni wivu tu,mtu anakwenda kumtunza kwa kuwa jamaa anaongea point za maana na hata kichwa kinafunguka unawaza mambo ya maana ndo maana kama unafuatilia kipindi huwezi ona mtu analala kila mtu anachangamka na kuimba

Inaelekea nawe ni mmojawapo wa waumini wa Lusekelo. Pole, inaelekea umekamatwa ki sawa sawa. Itachukua muda kutoka ktk usingizi mzito uliolala!
 
...nooo, mimi si mshirika wake lakini, sioni dhambi kumtuza mtu kama moyo wako umefurahi. mbona huko kwenye disco mnatoa au na huko ni wajinga..? anyway mtazamo mpana kwanini mkiambiwa kupeleka mbuzi kuku na hata kitu cha thamani kwa waganga/wachawi wa kienyeji mnatii bila maswali, je si zaidi kuwapa watumishi wa Mungu....???!!

Kanisani kuna muda wa sadaka,kwanini utoe katikati ya mafundisho.Usilinganishe mambo ya dunia na mambo ya Mungu
 
Wengi wanaochangia hapa ni mafarisayo na masadukayo,wamejihesabia haki na wanasimama mahali pa mwenye kuhukumu!bila shaka hawajui kumteta mtumishi wa Mungu ni kujitakia laana isiyo na sababu,sijui wamekosa kitu cha kujadili!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Nyie watu mnatumia neno la Mungu kuwapumbaza watu ole wenu
 
Hujui ulisemalo! Dini zenu zenyewe ndo balaa zaidi. Hakuna neno la uzima! Ni kujifunza yaleyale yaliyo kwenye litrugia dunia nzima! Wachungaji wenu wakiendesha magari halali kwao, lakini wengine wakiendesha magari nongwa. Ndo udhihirisho kuwa mna roho ya namna nyingine!

nafikiri hapa tunajadili utaratibu wa ibada zake sio wanavyomiliki au sivyo ndugu
 
Yesu alikuwa mwema hakuwa na dhambi hivyo ilikuwa ruhsa kwake kunyooshea wengine vidole hadharani; tena kumbuka alifanya hivyo ana kwa ana kitu ambacho hata wewe hukatazwi kumtokea Lusekelo ana kwa ana na kumuonya kwa upole mkiwa wawili peke yenu lakini si vyema kutangaza hadharani ubaya wake wakati unajua hata wewe si mwema; kwa maana hii hatutakiwi kuhukumu mtu juu ya neno lolote. Kama shida yako ni kuponya wanaopotoka kwa mahubiri yake toa neno pekee usimtaje mtu.

watu wengi wakikosolewa wanajikinga na msemo wa 'usihukumu' hapa hahukumiwi mtu bali tunakosoa mfumo wa uendeshaji wa ibado.kukosoa sio kuhukumu
 
Muombe mungu akupe macho ya rohoni kiwatengu ili uweze kumtambua yuko real au fake!!
 
Nilikuwa sehemu muda si mrefu,
Kulikuwa kuna kipindi kwenye runinga showing kipindi cha dini..

Nimeshangaa sana kuona aina ya dini inayofanywa na huyu jamaa!


Mnaoabudu pale huu utaratibu wakumtunza jamaa pale mbele kama

Mpo kwenye shoo za tangwa inakuwaje?
Tuelimishane

Mchungaji huwa anatunzwa kama ameongea point. Kama wewe unavyomtunza DIAMOND sasa pale mimi naona halazimishwi mtu kutunza.Soma biblia
 
Back
Top Bottom