Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Mzee wa Upako aliwekwa ndani kwa ajili ya ugomvi kati yake na jirani yake.
Very sad. Mzee wa Upako nadhani ndie anamiliki Wapo Radio. Ile radio siisikii siku hizi.
Wakati fulani ilipewa tuzo na Polisi kwa kazi nzuri-Polisi sasa ambao wamemkamata Mzee wa Upako.
Acha uongo mzee, kitu kama hukijui ni bora ukakaa kimya!
 
Mzee wa Upako aliwekwa ndani kwa ajili ya ugomvi kati yake na jirani yake.
Very sad. Mzee wa Upako nadhani ndie anamiliki Wapo Radio. Ile radio siisikii siku hizi.
Wakati fulani ilipewa tuzo na Polisi kwa kazi nzuri-Polisi sasa ambao wamemkamata Mzee wa Upako.
WapoRadio ni Gamanywa
 
Lusekelo bwana, ila kafanikiwa kwa hili, maana mbali na wafuasi wake naona bavicha wanamshangilia kwelikweli kwa kauli yake hiyo.

Sasa naamini kile kitambaa huwa unafuta jasho litokanalo na mchemko wa supu ya mawe au machozi ya Simba.
 
Anatafutia kiki kwa Lowasa baada ya kuulowanya kwa ulevi
 
Maneno hata kwenye kanga yapo. hii ndo sababu kubwa Cdm kumpokea lowasa Kwa sababu ni msafi tulijiridhisha hizo tuhuma ni za kubumba kama kweli mwizi ccm wampeleke mahaksmani.

na akipelekwa akashindwa basi yesu atarudi kabla ya siku ya mwisho.

kwakuwa tunajua hakuna kitu kama hicho lowasa baba karibu Cdm na marafiki wote walokufata wakaribie milele .

na wale waliobaki ccm ile mwaka Jana kwenye mkutano mkuu walishindwa kuzuia hisia zao wakaamua waimbe ule wimbo pendwa "tuna imani na lowasa" nao tunatambua uwepo wao indirect. kwenye siasa lowasa ni dhahabu huu ndo ukweli.
Waliomuita mwizi ni sisi CDM siyo CCM, Mpaka sasa nipo dilemma kuhusu chama sahihi cha upinzani wa dhati.
 
Mzee wa upako mjanja, anajua Chadema hata kama unatuhuma kubwa kiasi gain ukiwa upande wao watakutetea Kwa nguvu zote.

Na ndio kinachoendelea hapa, tayari vijana wa bavicha wameanza kumsafisha Na kashfa ya ulevi.!

Hongera Mzee wa Upako Kwa kuwajulia hawa viumbe.!
 
Cha pombe kaanza tena kuropoka ..mind his tongue
 
Tatizo ni la hawa wachungaji kutokuwa na misimamo inayoelewa. Mi namuoma kama Gwajima et al.
 
Jamaa ana akili sana kaona akiponda bavicha Na ndio wamejaa mtandaoni atapotea mapema
Saiv bavicha wanaoji " mna uhakika alikuwa amelewa?
Na EL ilikuwa hivyo hivyo walimuimba ni fisad alipokuwa ccm kaamia kwao wanakuja Na kauli za kuwa ni mtu safi.
Hongera sana Antony umecheza kama nemanja matic....
 
Tatizo watu wamesahau kama lusekelo nae ni binadamu ana moyo kama ulivyo wewe,kisa ni mchunga basi ndo hasikwazike hata mtu akimkwaza?asinywe pindi anapojua na kiu?fuata mafundisho na s matendo yake,yaani mtu akuingize dole la macho hushindwe kuongea eti we mchungaji,huo utakuwa unafiki bora uongee na utoe hasira zako ,zen utatubu kwa nyakati yake,coz toba imewekwa kwa wadhambi,tusihukumu coz sisi s wakamilifu na hakuna mkamilifu dunia hii wote tuna dhambi,I wonder tunashabgaa madhambi ya lusekelo twashindwa safisha yetu,toa boriti kwa jicho lako kwanza
 
Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ametoa ya moyoni kuhusiana na wanasiasa Kingunge Ngombare Mwiru na Edward Lowassa akitaka waombwe radhi.

Ni kama vile anafuata nyayo za Kakobe wa fgb. Mwisho wake unakaribia

Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amesema wanasiasa hao wamekosewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho amekitaka kiwapigie magoti Watanzania hao.
Mchungaji huyo amesema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam ametumia muda mwingi kueleza jinsi Lowassa na Kingunge walivyo muhimu kwa CCM.

Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, na Kingunge ambaye ni mwanasiasa mkongwe aliyefanya kazi kwa karibu na awamu zote nne za kwanza, walihama CCM wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka jana,
wakipinga uendeshaji mchakato wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

“Unawezaje kumuacha Mzee Kingunge na Lowassa wakaenda kwenye vyama vingine? Wale ni asset (mali). Ingekuwa mimi, ningerudi na kumpigia magoti Mzee Kingunge na kumwambia ‘Mzee chama kinakuhitaji rudi tukijenge,” amesema.

Mchungaji huyo maarufu amesema CCM imetumia muda mrefu kuwafinyanga viongozi hao, kwa hiyo ni hasara kwa chama kuwaacha.

“Mimi ninachojua ni kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri, ana ubinadamu. Katika watu ambao Mungu alitujalia kuwa viongozi, Lowassa yumo. Hata uniambie Lowassa mwizi, mimi sikubali,”amesema.

Lusekelo amemsifu Lowassa kuwa ndiye kiongozi pekee ambaye wakati akiwa Waziri wa Maji alithubutu kuvunja mkataba mbovu wa kampuni ya City Water iliyoingia mkataba wa kutoa huduma ya maji jijini Dar es Salaam.

“Unawezaje kumtukana mtu, sijui eti ni mgonjwa sijui nini. Hana kosa yule mtu. Amefanya nini, kwa nini kama Lowassa ni mwizi asikamatwe? Viongozi wa CCM wangapi ni wezi na ambao tayari wameshakamatwa, lakini Lowassa hakamatwi?” amehoji.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom