Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

HONGERA ALIYEANZISHA THREAD HII KWANI NI KICHWA KWELI KWELI AMEFANIKIWA KUWATOA WATU KWENYE MSTARI WA KUMFUATILIA KWA JAMBO LILE/ NA KUWASOGEZA HUKU,KWELI AKILI NI NYWELE
 
Tumekuelewa mheshimiwa Lusekelo,Ushauri wangu siasa unaiweza kama vipi ingia mazima mazima tu
 
Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ametoa ya moyoni kuhusiana na wanasiasa Kingunge Ngombare Mwiru na Edward Lowassa akitaka waombwe radhi.

Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amesema wanasiasa hao wamekosewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho amekitaka kiwapigie magoti Watanzania hao.
Mchungaji huyo amesema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam ametumia muda mwingi kueleza jinsi Lowassa na Kingunge walivyo muhimu kwa CCM.

Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, na Kingunge ambaye ni mwanasiasa mkongwe aliyefanya kazi kwa karibu na awamu zote nne za kwanza, walihama CCM wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka jana,
wakipinga uendeshaji mchakato wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

“Unawezaje kumuacha Mzee Kingunge na Lowassa wakaenda kwenye vyama vingine? Wale ni asset (mali). Ingekuwa mimi, ningerudi na kumpigia magoti Mzee Kingunge na kumwambia ‘Mzee chama kinakuhitaji rudi tukijenge,” amesema.

Mchungaji huyo maarufu amesema CCM imetumia muda mrefu kuwafinyanga viongozi hao, kwa hiyo ni hasara kwa chama kuwaacha.

“Mimi ninachojua ni kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri, ana ubinadamu. Katika watu ambao Mungu alitujalia kuwa viongozi, Lowassa yumo. Hata uniambie Lowassa mwizi, mimi sikubali,”amesema.

Lusekelo amemsifu Lowassa kuwa ndiye kiongozi pekee ambaye wakati akiwa Waziri wa Maji alithubutu kuvunja mkataba mbovu wa kampuni ya City Water iliyoingia mkataba wa kutoa huduma ya maji jijini Dar es Salaam.

“Unawezaje kumtukana mtu, sijui eti ni mgonjwa sijui nini. Hana kosa yule mtu. Amefanya nini, kwa nini kama Lowassa ni mwizi asikamatwe? Viongozi wa CCM wangapi ni wezi na ambao tayari wameshakamatwa, lakini Lowassa hakamatwi?” amehoji.

Chanzo: Mwananchi

 
Tatizo watu wamesahau kama lusekelo nae ni binadamu ana moyo kama ulivyo wewe,kisa ni mchunga basi ndo hasikwazike hata mtu akimkwaza?asinywe pindi anapojua na kiu?fuata mafundisho na s matendo yake,yaani mtu akuingize dole la macho hushindwe kuongea eti we mchungaji,huo utakuwa unafiki bora uongee na utoe hasira zako ,zen utatubu kwa nyakati yake,coz toba imewekwa kwa wadhambi,tusihukumu coz sisi s wakamilifu na hakuna mkamilifu dunia hii wote tuna dhambi,I wonder tunashabgaa madhambi ya lusekelo twashindwa safisha yetu,toa boriti kwa jicho lako kwanza
Mkuu umeongea pointi lakini ni wachache watakaokulewa maana wengi wanaongozwa na mihemko ya kisiasa.
 
CCM mdandio wakisikia neno Lowasa wana changanyikiwa na kuanza kutapatapa kama mgonjwa wa kifafa
 
Lusekelo haongeagi saana kuhusu mambo ya siasa ,sasa imekuaje !

Mtukufu usimjengee tena ile barabara uliomuahidi,mwambi wajengee haohao anaowasafisha. Aaalah!!!
 
Mzee wa upako mjanja, anajua Chadema hata kama unatuhuma kubwa kiasi gain ukiwa upande wao watakutetea Kwa nguvu zote.

Na ndio kinachoendelea hapa, tayari vijana wa bavicha wameanza kumsafisha Na kashfa ya ulevi.!

Hongera Mzee wa Upako Kwa kuwajulia hawa viumbe.!
Ulevi ni nini?

Ulevi ni kashfa?
 
b3e2db5a0ac99859fe3765c0a961577c.jpg
 
Hata Wayahudi Walimuita YESU kuwa ni MLAFI na MLEVI Lakini mwisho wa siku Walimpigia Magoti.

Tafadhali linganisha vinavyoweza kulinganishwa. Yesu hakulewa ila kwa vile alikaa na watu waliokuwa na historia ya dhambi na ulevi aliitwa kuwa naye mlevi na mwenye dhambi. Lakini wote walevi na wenye dhambi waliokaa na Yesu mwishoni waliokoka na kuacha ulevi na dhambi. Ni tofauti MNO na Lusekelo aliyeenda kwenye ulevi naye AKASHIRIKI ulevi halafu kutoka huko akaja kufanya matendo ya dhambi yaliyochajizwa na ulevi alioshiriki
 
Back
Top Bottom