Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Mtafutieni supu, hangover huwa inasumbua sana, hasa kama ni ya Konyagi.
 
Kuna muda nawaza hawa jamaa ni spin doctors na wanatumika na serikali kwa malengo yao fulani
 
Mh.Lowassa , Tupo pamoja nawe Mungu Anakupenda nasi tunakupenda Tunazidi kukuombea Na wote waliokusingizia waliokuombea mabaya Malipo hapa hapa Duniani
 
Mzee wa Upako aliwekwa ndani kwa ajili ya ugomvi kati yake na jirani yake.
Very sad. Mzee wa Upako nadhani ndie anamiliki Wapo Radio. Ile radio siisikii siku hizi.
Wakati fulani ilipewa tuzo na Polisi kwa kazi nzuri-Polisi sasa ambao wamemkamata Mzee wa Upako.
 
Lowasa ni Jembe hata sisiem wanamjua mwacheni aijenge CDM 2020 aingie state house aondoe huu umaskini unaoikabili nchi maana alisma mwenyewe anauchukia umasikini
 
Umesema kweli. Kwanza kupiga kinywaji hata Nuhu ambaye alikuwa anazungumza na Mungu directly alikuwa atakamata masanga na bado Mungu hakumuacha.
Hata akipolewa na kukaa uchi tunaona lililompata mwanae aliyemchungulia na kucheka baada ya kuona kende za mzee.
Kulewa siku moja kwa mzee wa upako is not a big deal kiasi cha maneno ya maana kuhusu ccm na kina Lowasa na Kingunge kutotiliwa maanani
Duuuuuu hivi hata upumbavu wa huyu mchungaji Lusekelo mmeanza kuangalia kisiasa, hatari sana.
 
Alipimwa kiwango cha kilevi kichwani kabla ya interview?

Ukiona umeanza kutetewa na watu wenye questionable images kwenye jamii jua hakuna kitu.
 
Mzee wa Upako anasema ukweli tupu lakini ni vigunu sana wachumia tumbo wa CCM kumuelewa.
 
He has a point.
Huyu 'mwizi' kwa nini hakamatwi? Miaka inaenda, wimbo wa fisadi unachuja, hakamatwi, why?!!

KADA
 
Mzee wa upako ana busara sana kuliko hata kardinali pengo


Huyu Lusekelo hana uadilifu wa kumtathmini mtu. Yeye ni mchafu kuliko hao CCM anaowasema. Halafu jambo jingine kati ya Lowassa au KLungunge kwa upande mmoja na CCM kwa upande mwingine, ni nani aliyemkosea mwenzake? Lowassa na Kingunge waliondoka CCM. Sasa hapo ndio CCM iwaombe msamaha? Au CCM kutompitisha Lowassa kugombea urais ndio kosa la kuombwa msamaha?? Nina uhakika Lusekelo sasa anahaha juu chini ili asifikishwe mahakamani. Na kwa nchi hii sitashangaa akitoa kityu kidogo ukasikia hakuna ushahidi japo video yote iko wazi. Nakumbuka mtu anayeitwa Aveva alihamisha pesa ya taasisi akaweka kwenye private account yake polisi wakadai wanachunguza ila hadi leo imeshasahaulika. Nchi hii bhana
 
Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ametoa ya moyoni kuhusiana na wanasiasa Kingunge Ngombare Mwiru na Edward Lowassa akitaka waombwe radhi.

Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amesema wanasiasa hao wamekosewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho amekitaka kiwapigie magoti Watanzania hao.
Mchungaji huyo amesema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam ametumia muda mwingi kueleza jinsi Lowassa na Kingunge walivyo muhimu kwa CCM.

Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, na Kingunge ambaye ni mwanasiasa mkongwe aliyefanya kazi kwa karibu na awamu zote nne za kwanza, walihama CCM wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka jana,
wakipinga uendeshaji mchakato wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

“Unawezaje kumuacha Mzee Kingunge na Lowassa wakaenda kwenye vyama vingine? Wale ni asset (mali). Ingekuwa mimi, ningerudi na kumpigia magoti Mzee Kingunge na kumwambia ‘Mzee chama kinakuhitaji rudi tukijenge,” amesema.

Mchungaji huyo maarufu amesema CCM imetumia muda mrefu kuwafinyanga viongozi hao, kwa hiyo ni hasara kwa chama kuwaacha.

“Mimi ninachojua ni kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri, ana ubinadamu. Katika watu ambao Mungu alitujalia kuwa viongozi, Lowassa yumo. Hata uniambie Lowassa mwizi, mimi sikubali,”amesema.

Lusekelo amemsifu Lowassa kuwa ndiye kiongozi pekee ambaye wakati akiwa Waziri wa Maji alithubutu kuvunja mkataba mbovu wa kampuni ya City Water iliyoingia mkataba wa kutoa huduma ya maji jijini Dar es Salaam.

“Unawezaje kumtukana mtu, sijui eti ni mgonjwa sijui nini. Hana kosa yule mtu. Amefanya nini, kwa nini kama Lowassa ni mwizi asikamatwe? Viongozi wa CCM wangapi ni wezi na ambao tayari wameshakamatwa, lakini Lowassa hakamatwi?” amehoji.

Chanzo: Mwananchi
Mlevi tu huyu. Kwanza awaeleze watu juzi anarejea kwake alfajiri kumekucha na kuzua ugomvi kutukana watu barabarani hadi kuwekwa ndani ilikua kisa gani. Sasa anaingia siasa sijui biashara ya kanisa inamshinda?
 
Back
Top Bottom