Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Huyu mzee wa upako mjanja sana, hapo badala ya watu kuendeleza mjadala wa ulevi wake kitakachofuata ni matamshi yake kuhusu Lowassa ndio yatakayojadiliwa, kausoma mchezo vizuri anajua kucheza na mind za watu!
Kwa kuwa idadi kubwa wanamsapoti Lowassa anajua ili kufuta ile aibu ni kugusa pale ambapo wengi watasapoti!!
Chezea bapa wewe, Bapa inaongeza I.Q...
 
WATU WENYE AKILI DUNI HUWEZA KUDHANI,RAIS MAGUFULI NI ADUI KWA LOWASSA,HILO HALIPO HAWA NI MARAFIKI WAKUBWA KWELI KWELI../ BALI MIFUMO ILIYOPO NDIYO INASABABISHA WATU KUKAA MBALI-/ LAKINI IKUMBUKWE MTU MZIMA HAPANGIWI RAFIKI,WALA ADUI.
•mf.ukiniambia mbowe ni adui na rais magufuli hakika NITAKUCHEKA SANA.
USILOLIJUA USIKU WA KIZA.
UADUI MKUBWA NA MBAYA ZAIDI UPO NDANI YA CHAMA KONGWE...
"TIME WILL TELL"
 
Maneno hata kwenye kanga yapo. hii ndo sababu kubwa Cdm kumpokea lowasa Kwa sababu ni msafi tulijiridhisha hizo tuhuma ni za kubumba kama kweli mwizi ccm wampeleke mahaksmani.

na akipelekwa akashindwa basi yesu atarudi kabla ya siku ya mwisho.

kwakuwa tunajua hakuna kitu kama hicho lowasa baba karibu Cdm na marafiki wote walokufata wakaribie milele .

na wale waliobaki ccm ile mwaka Jana kwenye mkutano mkuu walishindwa kuzuia hisia zao wakaamua waimbe ule wimbo pendwa "tuna imani na lowasa" nao tunatambua uwepo wao indirect. kwenye siasa lowasa ni dhahabu huu ndo ukweli.
 
Mlimuhoji muda gani? hebu rudini tena mida ya usiku saa mbili mbili hivi kama hata atakumbuka hayo yote.
 
Hili lilevi nalo vipi.
77d0cf3f6d8cd680c88148ea43e214a9.jpg
 
Mtumishi wa Mungu hasemwi vibaya ila unaacha Mungu atafanya atakavyo. It's advisable not to talk ill of Pastors as God knows how to handle them.
 
Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ametoa ya moyoni kuhusiana na wanasiasa Kingunge Ngombare Mwiru na Edward Lowassa akitaka waombwe radhi.

Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amesema wanasiasa hao wamekosewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho amekitaka kiwapigie magoti Watanzania hao.
Mchungaji huyo amesema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam ametumia muda mwingi kueleza jinsi Lowassa na Kingunge walivyo muhimu kwa CCM.

Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, na Kingunge ambaye ni mwanasiasa mkongwe aliyefanya kazi kwa karibu na awamu zote nne za kwanza, walihama CCM wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka jana,
wakipinga uendeshaji mchakato wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

“Unawezaje kumuacha Mzee Kingunge na Lowassa wakaenda kwenye vyama vingine? Wale ni asset (mali). Ingekuwa mimi, ningerudi na kumpigia magoti Mzee Kingunge na kumwambia ‘Mzee chama kinakuhitaji rudi tukijenge,” amesema.

Mchungaji huyo maarufu amesema CCM imetumia muda mrefu kuwafinyanga viongozi hao, kwa hiyo ni hasara kwa chama kuwaacha.

“Mimi ninachojua ni kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri, ana ubinadamu. Katika watu ambao Mungu alitujalia kuwa viongozi, Lowassa yumo. Hata uniambie Lowassa mwizi, mimi sikubali,”amesema.

Lusekelo amemsifu Lowassa kuwa ndiye kiongozi pekee ambaye wakati akiwa Waziri wa Maji alithubutu kuvunja mkataba mbovu wa kampuni ya City Water iliyoingia mkataba wa kutoa huduma ya maji jijini Dar es Salaam.

“Unawezaje kumtukana mtu, sijui eti ni mgonjwa sijui nini. Hana kosa yule mtu. Amefanya nini, kwa nini kama Lowassa ni mwizi asikamatwe? Viongozi wa CCM wangapi ni wezi na ambao tayari wameshakamatwa, lakini Lowassa hakamatwi?” amehoji.

Chanzo: Mwananchi
Alikuwa amekunywa ngapi wakati anaongea utumbo huu!!
 
Alikuwa amekunywa ngapi wakati anaongea utumbo huu!!
Rais Magufuli atembelea kanisa la mch. Lusekelo.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, kwa hiyo nataka kukuthibitishia ninakupenda sana.

“Ndio maana kuna siku moja, ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi nitafute mbinu za namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi, nikamtuma meneja wa barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu changamoto zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu, nataka kukuthibitishia kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo” Alisema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na waumini.
 
Maneno hata kwenye kanga yapo. hii ndo sababu kubwa Cdm kumpokea lowasa Kwa sababu ni msafi tulijiridhisha hizo tuhuma ni za kubumba kama kweli mwizi ccm wampeleke mahaksmani.

na akipelekwa akashindwa basi yesu atarudi kabla ya siku ya mwisho.

kwakuwa tunajua hakuna kitu kama hicho lowasa baba karibu Cdm na marafiki wote walokufata wakaribie milele .

na wale waliobaki ccm ile mwaka Jana kwenye mkutano mkuu walishindwa kuzuia hisia zao wakaamua waimbe ule wimbo pendwa "tuna imani na lowasa" nao tunatambua uwepo wao indirect. kwenye siasa lowasa ni dhahabu huu ndo ukweli.
Ni zaidi ya dhahabu. Lowassa ni mfano wa kuigwa
 
Back
Top Bottom