Anthony Lusekelo: Lowassa mtu safi

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,379
2,533
Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ametoa ya moyoni kuhusiana na wanasiasa Kingunge Ngombare Mwiru na Edward Lowassa akitaka waombwe radhi.

Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amesema wanasiasa hao wamekosewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho amekitaka kiwapigie magoti Watanzania hao.
Mchungaji huyo amesema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam ametumia muda mwingi kueleza jinsi Lowassa na Kingunge walivyo muhimu kwa CCM.

Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, na Kingunge ambaye ni mwanasiasa mkongwe aliyefanya kazi kwa karibu na awamu zote nne za kwanza, walihama CCM wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka jana,
wakipinga uendeshaji mchakato wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

“Unawezaje kumuacha Mzee Kingunge na Lowassa wakaenda kwenye vyama vingine? Wale ni asset (mali). Ingekuwa mimi, ningerudi na kumpigia magoti Mzee Kingunge na kumwambia ‘Mzee chama kinakuhitaji rudi tukijenge,” amesema.

Mchungaji huyo maarufu amesema CCM imetumia muda mrefu kuwafinyanga viongozi hao, kwa hiyo ni hasara kwa chama kuwaacha.

“Mimi ninachojua ni kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri, ana ubinadamu. Katika watu ambao Mungu alitujalia kuwa viongozi, Lowassa yumo. Hata uniambie Lowassa mwizi, mimi sikubali,”amesema.

Lusekelo amemsifu Lowassa kuwa ndiye kiongozi pekee ambaye wakati akiwa Waziri wa Maji alithubutu kuvunja mkataba mbovu wa kampuni ya City Water iliyoingia mkataba wa kutoa huduma ya maji jijini Dar es Salaam.

“Unawezaje kumtukana mtu, sijui eti ni mgonjwa sijui nini. Hana kosa yule mtu. Amefanya nini, kwa nini kama Lowassa ni mwizi asikamatwe? Viongozi wa CCM wangapi ni wezi na ambao tayari wameshakamatwa, lakini Lowassa hakamatwi?” amehoji.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu ni bwege kweli? Anamtafuta Lowasa leo? Aache kupiga dili alifikiri siku ile JPM alienda kusali bure na zile sifa ,, sasa ni wakati wa kulipa yale madhambi yake
 
Back
Top Bottom