Another 'victim'? Malegesi Adaiwa Kunyeshwa Sumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Another 'victim'? Malegesi Adaiwa Kunyeshwa Sumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mafuchila, Feb 8, 2009.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Malegesi adaiwa kula kitu chenye sumu

  2009-02-08 11:03:00
  Na Mwandishi Wetu

  Mmoja wa watu muhimu anayeaminika kubeba siri nzito juu ya mmiliki halisi wa kampuni tata ya Kagoda, inayodaiwa kuchota Sh bilioni 40 kwenye akunti ya EPA, amelazwa katika Hospitali ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam, tangu Januari 26 mwaka huu, baada ya kula kitu kinachodaiwa kutiwa sumu.

  Huyu si mwingine bali ni Mwanasheria wa Jijini Dar es Salaam, Bered Malegesi (31), ambaye kampuni yake ilitoa mchango mkubwa katika kuzisajili baadhi ya kampuni zilizochota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  Malegesi alikuwa mshirika wa karibu wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu Daud Ballali.

  Tukio hilo lisilo la kawaida, limekuja miezi tisa tu tangu Dk. Ballal, alipofariki dunia katika mazingira ya kutatanisha nchini Marekani, baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu.

  ``Aliletwa hapa akiwa hajitambui...lakini baada ya kumfanyia vipimo vya kimaabara tulibaini kuwa amekula kitu chenye sumu``, alisema daktari mmoja wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa sababu zinazojulikana.

  Kumbukumbu za hospitali hiyo zinaonyesha kwamba, Maregesi, ametumia siku 11 akiwa amelazwa akipatiwa matibabu ya kuondolewa sumu inayodhaniwa alikula baada ya kutiwa kwenye chakula muda mfupi kabla hajaanza kuumwa.

  Muuguzi aliyekuwa akimhudumia mwanasheria huyo hospitalini hapo ambaye naye alikataa jina lake lisiandikwe gazetini kwa maelezo kuwa si msemaji wa hospitali hiyo, alieleza kuwa Maregesi alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa katika hali mbaya, akitapika mfululizo huku mwili ukiwa na joto kali.

  ``Hali yake ilitutisha sana...alikuwa hana uwezo wa kufanya chochote na timu nzima ya madaktari na wauguzi waliokuwa wakimhudumia walipata mshangao, tumeshawahi kupata matukio kama haya ya watu kuletwa wakiwa hawajitambui, lakini hili lilikuwa tofauti kabisa``.

  ``Tulikuwa tumemuweka katika uangalizi maalumu na wa karibu wakati wote, hata hivyo, hatuwezi kusema kama sumu hii imeingia mwilini baada ya kula chakula kilichotiwa sumu au hapana. Siku ya kwanza alipoletwa hali yake ilituchanganya sana, lakini sasa kadiri siku zinavyoenda anaanza kupata nafuu taratibu na hii ni faraja kwetu``, aliongeza kusema muuguzi huyo.

  Hata hivyo, maadili ya kazi ya udaktari yanakataza madaktari na wauguzi kutoa taarifa kwa umma za mgonjwa aliyechini yao, hivyo kutokana na hali hiyo walikataa kutoa maelezo zaidi kuhusiana na mambo yaliyogundulika kwenye vipimo vya kimaabara.

  ``Hatuwezi kutoa taarifa zozote kuhusu aina ya sumu au matokeo yoyote tuliyoyabaini kwenye vipimo vya kimaabara bila ya ruhusu ya mgonjwa mwenyewe``, alisema muuguzi mmoja mwandamizi ambaye alikataa kuandikwa jina lake.

  Inaelezwa kuwa daktari aliyechukua vipimo vya mgonjwa huyo ameshauri ufanyike uchunguzi zaidi wa kimaabara ili kuweza kubaini kiasi cha sumu kilichosambaa mwilini.

  Hata hivyo, daktari huyo ameshaandika dawa anazotakiwa kutumia mgonjwa huyo, vikiwemo vidonge vya kuzuia kutapika, dawa za kupunguza maumivu na za kunyonya sumu toka mwilini.

  Akizungumza na Nipashe Jumapili, baada ya kutoka hospitali juzi, Malegesi, alithibitisha kuwa alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mikocheni baada ya kula kitu chenye sumu.

  Alisema hawezi kuhukumu kama sumu hiyo atakuwa amewekewa kwa makusudi kwa lengo la kumdhuru au aliiinywa kwa bahati mbaya bila ya kujua.

  Malegesi aliongeza kusema kuwa ameruhusiwa kutoka hospitali, lakini madaktari wamemshauri akapate matibabu zaidi nje ya nchi kutokana na sumu hiyo kumuathiri vibaya.

  Hata hivyo, amesema kwa sasa hawezi kusafiri nje ya nchi kutokana na hati yake ya kusafiria kushikiliwa na Timu ya Rais iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza wizi uliotokea kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  * SOURCE: Nipashe
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sitashangaa huu ukiwa usanii mwingine kama ule wa Ballali.

  Kama hana uhakika kawekewa sumu si aende polisi ili wafanye uchunguzi?

  Dr. Slaa kwa kila alichofanyiwa katoa report polisi. Hata kama wengi haturidhiki na utendaji wa polisi lakini bado polisi ndio wana wajibu wa kuchunguza kama kuna foul yoyote kwenye maisha ya raia.

  Huyu jamaa sitashangaa akianza kuomba pasi yake ili aende nje kutibiwa kwa kisingizio cha kunyweshwa sumu.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  The saga continues..

  Hivi tumefikia Episode ya ngapi vile?
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  1. Tanzania, Tanzania Nakupenda kwa moyo wote Nchi yangu Tanzania Jina lako ni tamu sana Nilalapo nakuota wewe Niamkapo ni heri mama wee Tanzania, Tanzania Nakupenda kwa moyo wote

  2. Tanzania, Tanzania Ninapokwenda safarini Kutazama maajabu Biashara nayo makazi Sitaweza kusahau mimi Mambo mema ya kwetu kabisa Tanzania, Tanzania Nakupenda kwa moyo wote

  3. Tanzania, Tanzania Watu wako ni wema sana Nchi nyingi zakuota Nuru yako hakuna tena Na wageni wakukimbilia Ngome yako imara kweli wee Tanzania, Tanzania Heri yako kwa mataifa

  4. Nchi nzuri Tanzania Karibu kwa wasio kwao Wenye shida na taabu Kukimbizwa na walowezi Tanzania yawakaribisha Mpigane kiume chema wee Tanzania, Tanzania Mola awe nawe daima
   
 5. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #5
  Feb 8, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu kweli huu mchezo wa kuigiza tuko episod ya 5 hakuna tofauti na ile tamthilya ya LOST,tuendelee kuangalia
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  na mi mi nasema kama anaumwa kwanini katoka hospitali? asije akawa anataka kukimbia?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  August,
  Huyu hawezi kukimbia kwa sababu pasipoti yake imeshikiliwa na serikali. Hili la sumu sishangai kabisa. There is a pattern here. Wakishindwa kukumaliza kwa Fuso watakumaliza kwa sumu. Ninachojiuliza ni kwa nini hakukamatwa mapema kabisa walipokamatwa watuhumiwa wengine wa EPA? Jibu ni kwamba hawakutaka kumkamata.
   
 8. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2009
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Duh!!! Hivi malegesi ana miaka 31!!!!
   
 9. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2009
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa nathani watanzania wanaanza kuamini kwamba mambo ya usifadi Tanzania goes beyond our innocent belief. This is like Italian or south america mafia groups. Naomba mfikirie hii vitu

  1. Malegisi ni lawyer! ambaye alikuwa karibu na Balali
  2. Balali aliuwawa na sumu which sound very similar to hii ya Malagesi
  3. Malegesi ni mstakiwa wa EPA
  4. Siri kubwa ya EPA alikuwa nayo Balali

  Sasa maswali ya kujiuriza

  1. Huyu Malegesi ana infomation ambazo zinaweza kumtoa kwenye kesi ya EPA na kuwaweka the really mafisadi kwenye hukumu
  2. Je alikuwa lawyer wa Balali? anajua ukweli ambao Ulichukua maisha ya Balali?
  3. Nani yuko nyuma ya hizi sumu zinazotoa maisha ya watu ambao wana information kuhusu ufisadi?
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kukimbia kuna kuja ktk context ya kutaka kwenda kutibiwa nje ya nchi hivyo arudishiwe passport akatibiwe.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Ni ajabu watu hawa kuwa nje pamoja na kuhusika na wizi mkubwa. Wote walistahili wawe rumande ili kusaidia uchunguzi na kuwepo kwao uraiani kunawawezesha kuvuruga uchunguzi na pia haya ya kula sumu au kulishwa sumu wangekuwa rumande yasingetokea.
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Huyu tuliwahi kusema huko nyuma kuwa ndiye mwenye habari zote muhimu za Balali, la yeye kukimbia nchi siamini maana hana sababu, ila hapa kuna mtego mzito ambao either umetengenezwa na mafisadi au yeye huyu mkuu,

  - Ninaswali moja kwa wahusika wote wa hii sagga, Mkono yuko wapi katika all this?
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkono sijajua role yake, ila nakumbuka kuna wakati habari iliwekwa hapa JF kuwa Mkono alionana na Balali huko Washington DC kabla ya kifo chake, lakini kama kumwamini nadhani alimwamini Malegesi shemeji yake, rather than Mkono.
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Hawa mafisadi wa EPA unweza kudhani wana akili kumbe ni butu tu ni bahati na positions walizonazo na kubebana kimatabaka.

  Kutokana na kauli zake unaweza kuona kuwa ni famba tu. Na inawezekana ameongea na daktari ili aadikiwe ruhusa ya kwenda kutibiwa nje, at the same time hospital wameshamruhusu kutoka na daktari kasema wanataka watumie maabara kufanya uchunguzi zaidi ili kuweza kubaini kuwa ni sumu ya aina gani.

  Pia Malegesi mwenewe andhani kuwa anaweza akawa amjinywesha hiyo sumu yeye mwenyewe....Yani ni vituko tu.

  Kama ni kweli wanaaanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe tutajua kwani tulishatabiri hapa JF,na pia kama ni usanii tutajuwa tu maana naona Ballali amempa mchecheto...Assuming kwamba Ballali amepotea tu.
   
 15. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2009
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sasa hapa ndio questions zinakuja... wana JF inabidi tupige kelele humu kwa nguvu zote serikali iwajibike kumtafuta mtu aliye muua Balali, mwili wake ufukuliwe na ufanyiwe uchunguzi kuona kama sumu aliyokunywa/wekewa huyu Malegesi ni sawa na yake...

  Hii ndio only solution to know the truth
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Unaona sasa mkuu yote haya tuliyasema mapema, tukatukanwa sana hapa, sasa unaona yanaanza kujirudia tena kama tulivyotabiri, ninakumbuka mimi na Lunyungu ndio tulikuwa wa kwanza kutabiri haya, kwamba Malegesi ana siri nzito sana kuhusu kifo cha Balali.

  - Hapa ninaamini kwamba kuna one thing, mafisadi wameanza kwua na wasi wasi na huyu Malegesi kwamba hawawezi kumuamini hasa katika hii safari yao ya kutafuta urais, Mkono tayari mafisadi wamemuudhi kwenye uchaguzi wa wazazi na ukishamuudhi Mkono, sasa unamuuhdi na huyu Malegesi, sasa hapa kama mafisadi wana tatizo na huyu Malegesi, basi next on line ni Mkono,

  Sasa nina ombi moja kwa wale wote mnaowafahamu hawa Malegesi na Mkono, kwa karibu ni kwamba ni vyema wakatusaidia taifa kwa kututolea ukweli wote unaohusu ishu ya Balali, kwa sababu hawa wawili wanazo info zote na muwape ujumbe I hope wanaelewa what is next.....!

  Susuviri bravo mkuu kwa kumbu kumbu nzito, vipi mkuu na wewe unakunywa mafuta ya samaki kama mimi, maana ninafanya huuu mchezo toka nikiwa 2 years old, sijawahi kusahau kitu, bwa! ha! ha! ah!
   
 17. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #17
  Feb 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa ukishajua amekunywa ndio alinyeshwa utafanya nini ?
   
 18. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu, umenichekesha sana, mimi nafahamu memory yako ni kali sana na mimi pia napenda kunoa akili na kuwa na memory, kwani naamini inasaidia sana kusurvive katika environment yetu.
  Utafikiri tulikuwa wote wakati Mkono wanamsumbua katika wazazi! Nilisema na mimi, in my circle of trust: Jamani! Babu huyu atawa-change-ia na akishawageuzia kibao watalia wao, siyo Mkono!
  Malegesi ni mwoga sana hawezi kuongea lakini Mkono ndo ana spine of steel, na anaweza kuwatenda. Tatizo he has skeletons in his closet, nadhani hata hii CIS case atakuwemo, lakini hakuna atakayempata huyu mzee ni mjanja, he is like Edgar Hoover yule mkuu wa FBI, he has files on everyone. Nadhani mimi na wewe hatuhitaji kuendelea kuweka vitu vingine hapa lakini historia yake unaifahamu vizuri tangu enzi za akina Rajpa! Pia tunafahamu vyema kuwa he believes that JK is weak, na hamuogopi. That makes him a troublemaker na najua kuwa wanamtafutia sana angle. He is next on the list!
  Lakini Malegesi is a real wimp! Anadhani that he is safer if he keeps silent, kumbe hajui the only thing that will protect him is publicity. Anyway ataendelea kuficha evidence zake za Balali na uchafu wote lakini if the heat is too strong, he will pass the relay to Mkono.
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Future-T
  Swali lako la tatu ndilo nami pia linaninyima usingizi.
  August,
  Malegesi hana nia ya kukimbia nchi. Alikuwa tayari kufikishwa mahakamani.
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Jasusi, hapa tupo wote Malegesi kukimbia nchi ni kama kusema eti Mkono atakimbia nchi, no way! Hawa wana siri nzito sana ya mafisadi na huko BOT, kuna kiongozi mmoja mzito wa taifa aliniambia huko nyuma kua Malegesi ndiye mwenye mambo yote ya Balali, na wao serikali wanajua hilo na pia mafisadi wanajua, sasa hapa naona kuna marathon flani hivi, lakini nitawasifu sana mafisadi kama watakuwa na nguvu za kuweza kuzuia ukweli wa kifo cha Balali this time usitoke, ingawa pia huwezi jua nani ana interest zaidi na habari hizo kutotolewa nje betweeen hawa players wote wa hii picha. Unaweza kuta hata serikali haitaki habari hizo zitoke kwa sababu na wao wanaweza kwua implicated, kuna Mama Meghji, sidhani kama angependa hii habari itoke, I mean ni wengi sana hapa kwenye hiki chungu.

  -Kwa sababu sio siri sasa kwamba walipomuzia Mkono Wazazi, sielewi walikuwa wanaangalia kwa urefu gani, maana sasa hapa tunaweza kuishia kupata ukweli wa kifo cha Balali, ambacho binafsi ninaaamini zitasiaida sana kufungua mambo mengi sana yanayofichwa ingawa mengi pia yapo wazi lakini viongozi wetu hawataki ku-act.

  Lakini no matter what, sterling hapa kwenye hii picha ni Mkono na Malegesi tu!
   
Loading...