Another Joke from Kikwete: Every student to have computer in five years time

Another Joke from Kikwete: Every student to have computer in five years time

Childish!!!....Anyway, alikuwa anaongea na watoto, na hivyo labda ilikuwa ni ongea ya ki'dimbadimba zaidi, na ile michezo tulikuwa tukiita mdako au NAGE zamani!
kwa hiyo atakuwa alikuwa anatania tu!! kama kawa!
 
Juzi JK alipokuwa anaongea na watoto wa shule mbalimbali nchini aliahidi kuwa akichaguliwa miaka 5 ijayo, atahakikisha wanafunzi wote watakuwa wanasoma kwa mtandao na kila mwalimu atakuwa anakuwa na laptop yake...mnauonaje huu mtaji?


Amakweli, kama ulivyo sema ni ndoto. Serekali imeshindwa kujenga madarasa, mpaka sasa kuna shule majengo yake ni ya nyasi, wanafunzi wanakaa chini hamna madawati, nyumba za waalimu ndo usiseme. Leo ni wanafunzi kusoma kwa mtandao, na kila mwalimu kuwa na laptop?

Sipati picha KABISAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.
 
...................nasikia hao watoto walikuwa wamevaa mashati ya kijani na kuimba "sema baba..usiogope semaaa"!!! kwa kuwa anajua tulivyomkinai, wasaidizi wake wanamuandalia mikutano atakayopigiwa makofi ili wajifariji!!!!! huyo ndio mkwere zaidi umjuavyo!!!!
 
Mwacheni jamani si unajua story na watoto lazima akili yako ifanane na ya kwao? Mambo ya sungura akasema, urafiki wa simba na sungura nk. Lakini watoto walimpiga maswali ya kikubwa zaidi kama watoto wa kike wakipata ujauzito kuruhusiwa kuendelea na shule nk. akaona awapoze na toriiiiiiii za hapo zamani za kale
 
...................nasikia hao watoto walikuwa wamevaa mashati ya kijani na kuimba "sema baba..usiogope semaaa"!!! kwa kuwa anajua tulivyomkinai, wasaidizi wake wanamuandalia mikutano atakayopigiwa makofi ili wajifariji!!!!! huyo ndio mkwere zaidi umjuavyo!!!!
Eti wanafunzi wa University nao wanaipigania ccm!
 
Inategemea alikuwa anaongea laptop zinazotumia National panasonic!!! Kama madawati hakuna je huo umeme wakuchaji laptop utatoka wapi???Labuda alikuwa akimaanisha shule za Bunge,Olympio Oysterbay kwani nikitu kisichoingia akilini!!Sijui labda anatimiza maandishi ya wahenga kwamba Siasa ni Mchezo mchafu!!
 
mhhhhhh, amakweli watanzania nasi, sasa hata mwandishi wa rais hajui hata la kupeka kwenye public?
 
Nanena kwa kinywa pasipo na kufirkiriiiiiii, Uchumi wa nchi JK ameu......bu.
 
Vituko vya Mr President, It si possible in Tz only.

Nafikiri JK aendelee na safari zake za nje maana anaidalilisha Nchi na watanzania kwa ujumla. Dunia inaishangaa Tz kwa kuwa na rais mtoa ahadi isiyotekelezeka, ajabu zaidi anaposema hayo anapigiwa makofi. Udom wamshangilia na kumnunulia fomu ni vituko full. JK namwomba abadilike ili kuiondolea Tz aibu. Au tumwondoe hana jambo la msingi atakolotuambia kwa mwaka huu wa uchaguzi. Mie nimemchoka natamani watanzania washutuke,

Ni kwanini hatumsaidii Jk, tumnyime kura huu ni msaada tutakaompa JK kwani ni aibu kuwa na rais kama yeye. anaahidi yasiyowezekana. Vijana, wazee, kina mama mwaka huu nn muda wa kumsaidia Jk. Hata kama hujajiandikisha kupiga kura, bado una nafasi ya kumsaidia JK mfano akiaahidi ahadi za ajabu ajabu UMZOMEE, NUNA, SIYO yeye tu, ni pamoja na chama chake.

Tuhamasishane kumsaidia JK na CCM kumwangusha kupitia kura zetu
 
You can fool some people sometime but you cannot fool all people all the time. Na watoto hawapigi kura bwanaaaa ama! Hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ng'o.
 
Juzi JK alipokuwa anaongea na watoto wa shule mbalimbali nchini aliahidi kuwa akichaguliwa miaka 5 ijayo, atahakikisha wanafunzi wote watakuwa wanasoma kwa mtandao na kila mwalimu atakuwa anakuwa na laptop yake...mnauonaje huu mtaji?
Ni asilimia 13 tu ya watanzania wanapata umeme. Na ni asilimia 5 tu ya watanzania wote wanatumia computa. Na ni asilimia 8 tu ya watumia computer wote wana access ya internet Tanzania. Huko kusoma kwa mtandao anakokusema JK kutakujaje? Kwali hii ni ndoto, tena ya mchana.
 
Sina lakusema kwa hili ila, nafikiri alivyo huyu comedian na wanaomuunga mkono, ni watu wanaoniumiza kichwa. Mapambano bado ni magumu sana,kama wafuasi wapo hivi. KWELI TUNAHITAJI THE TIME MACHINE
 
Siku zote nasemaga kuwa hakuna mpuuzi wa mawazo na mtazamo kama rais kikwete
 
Asabuhi ya leo nilikua nikisikiliza news toka Radio WAPO, mojawapo ya taarifa ni kwamba eti Kiranja mkuu kawaambia wachaga kuwa miaka mitano ijayo shule elfu tatu zitakuwa zinafundisha kwa kutumia Tele-conferencing system hivyo tatizo la uhaba wa Walimu litapungua...na blah blah nyingi. Swali langu la wasiwasi ni kwamba,

Hapa UDSM achilia mbali huko primary na secondary, wameshindwa kutumia system hizo, huko kwa walimu wa watu wasiojua lolote si ndio kuwadangaya kweli? UDSM zipo room ALT A & B na SA & SB vyenye hii mifumo ambayo wala haifanyi kazi wala haitumiki...jamani kweli walimu wetu waweza kuyafanya haya ndani ya hiyo miaka mitano ya Kiranja mkuu huyu, ajabu ya Mungu wachaga wale wakapiga makofi na kufurahia kweli kweli.

Tunakoelekea tutakuja kuambiwa mabomba yatatoa maziwa tukubali. tuwaeleze wananchi vitu ambavyo vina mantiki na sio kuongea ili mradi umeongea

Hii ndiyo si hasa, kazi yake kubwa ni kucheza na akili za watu kwa kufuta previous memory about your past pledge to them and save new memory about your future so that they will vote for you. Is a game of convincing the unrealistic to the short memories of wadanganyika
 
Huyu jamaa sijui alijua anaongea na WAZEE WA DARESALAAM!!!
Umeme wenyewe tu taabu kwenye sekondari nyingi, hizo computer watawasha kwa mafuta ya taa?
Waziri wake mmoja aliwahi kuulizwa kama kuna mpango wa "a laptop per child" kama Rwanda, akajibu hakuna mpango kama huo kwa sasa!! huyu mjomba wenu anawaongopea.
 
Back
Top Bottom