Anne Semamba Makinda's Profile!

Sikutegemea huyu mama kusema maneno haya kwa wakati huu, hasa akiwa amechaguliwa kama speaker wa bunge. Hili linanipa shaka katika ufanisi wake wa kazi, kwani ameanza vibaya kwa kutumia siasa za maji taka.

Wote tunajua kuwa suala la kuongelea kuhusu 'wizi wa mke wa mtu' ni nini na linamlenga nani. Ni maji taka hayohayo ambayo yalitumiwa na viongozi wa ccm dhidi ya Dr. Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi. Kwa hili tunaweza kusema kwel kama atafanya kazi yake vizuri? Leo hii hakuna haja ya kutafuta maana ya neno 'fisadi'. Kila mtu anajua hata mtoto wa darasa la 3 anajua.

Kwa kutamka hivyo hadharani, ameuhakikishia umma wa Kitanzania kuwa amewekwa pale kuetetea hoja za mafisadi, hakuna mjadala zaidi. Kama yeye alikuwa halijui hilo, basi imeliwa kwake!
 


Mkuu kama kuchaguliwa kwa Anne Makinda kuwa spika kuna mkono wa Ikulu basi kwa lugha nyepesi kabisa bila kuzungusha mdomo ni kusema kuchaguliwa kwake kuna mkono wa mafisadi.
Kila mmoja anafahamu jinsi JK alivyo na mafungamano na mafisadi papa sasa tena unatuzuga eti mafisadi walimtaka Anna Abdallah? hapana bana acha hizo. As long uchaguzi wa spika Makinda ulikuwa na mkono wa ikulu basi uchaguzi wa spika ulikuwa na mkono wa mafisadi, wala hatuhitaji longo longo juu ya hilo pamoja na kwamba uko karibu na ikulu.
 


mkuu sijakusoma vizuri hapo unaweza kutoa ufafanuzi kidogo? i mean ufisadi na Butiku na Warioba inakuwaje hapo?
 

- Mkuu siko karibu na mahali popote isipokuwa niliyoyasema ni mtizamo wangu kuhusu matokeo ya uchaguzi kuanzia wa taifa mpaka huu wa Spika, na wewe uko entitled na mtizamo wako, wangu uko based only na facts za matokeo ya uchaguzi na understanding siasa zetu bongo kwamba Spika hawezi kuchaguliwa toka chama tawala bila ridhaa ya Ikulu,

- Otherwise wako pia ni mtizamo wako on the ishu at hand na wala hakuna tatizo ni wananchi wanaosoma ndio wataamua upi unaweza kuwa muelekeo halisi wa kinachoendelea.


William.
 
uyo mama SIYO MNYALU, msiharibu kabila la watu bure. huyo mama ni MBENA yaani from bena tribe. wabena wanatoka wilaya ya njombe, wilaya ya iringa mjini na vijijini na kilolo ndo kuna wahehe, wilaya ya Ludewa wapo WAPANGWA, wilaya ya Makete wapo wakinga na wawanji...Mufindi wapo wahehe. huyu mama ni mbena na ni mkabila vibaya mno...anapendelea sana wabena. katika list yao, wapo yeye, Luhanjo, Deo yule mbunge aliyekuwa lawyer wa Barick, mkuu wa mainjinia hapa tz, kina makweta etc. kuna siku nilishawai kuhudhuria graduation moja hivi waliifanya pale mabibo mimi nilijifanya mbena mwenzao, nilichoshuhudia ni kwamba tz ukabila upo mkubwa sana underground.

Huyo mama ndiye aliyeipigania sana njombe hadi kuomba kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Njoluma/njombe ili kujing'oa kwenye mkoa wa wahehe, hivyo yeye hatoki tena iringa, anatoka mkoa wa njoluma/njombe. kama kuna mtu mwenye swali uliza.
 

Mkuu umechukua dhamana kubwa sana hapo. Kwa kweli naomba uhai na afya njema tu nishuhudie huo "muujiza". Manake wengine imani ilishatutoka kitambo sana.
 

Mtanganyika
Mimi siku zote nimekuwa naeleza kuhusu huyu opportunist Sitta na ninakubaliana na wewe kabisa, na kwa huyu mama, again hamna cha maana zaidi ya party politics atakazofanya bungeni, kamati na maamuzi ya kamati kwa kwenda mbele, nakuhakikishia atajitahidi tu kuhakikisha kuwa wapinzani hawaongei au kuuwa hoja zao bungeni na hakuna zaidi.
 

Ukitaka kumjua Sitta, fuatilia record yake CDA na TIC. Ni mwizi aliyevaa ngozi ya kondoo.

Mmesahau dawa za milioni mbili? Mmesahau ofisi ya Spika kule kwao?

Ni sawa alikuwa upande wa wananchi kwenye suala la ufisadi sio kwasababu yeye mwenyewe anapinga ufisadi kwa matendo bali kwasababu hao mafisadi walikuwa ni maadui zake kisiasa.
 

Writing style kama ya Field Marshal ES. Not implicating you though, kufanana siyo kosa.
 

Mheshimiwa boma;

Kuna magonjwa kwa mamia ambayo ni MORAL VALUE - BASED!! ..hata Ukimwi weneyewe ni moral value related.. Its very important kwa kiongozi ku observe moral supiriority kama mtindo wa maisha ..vingine atasimama vipi mbele ya majukwaa kwa kampeni mbalimbali?
 
Mtoto wa Anna atakuwa mkubwa kuliko huyo Neema. Neema atakuwa ni mtoto wa mke ambaye Prof alimuoa baada ya kuzaa na Anna. Watoto wa Prof kwa mke huyo wamesomea South Africa. I remain to be corrected .

uko sawa.
 
William asante kwa maelezo mengi uliyotoa kuhusu Anna, japo kuna maswali mengi watu bado yapo vichwani mwao na pengoine Anna will prove us wrong,
Lakini kwangu mimi ni kubwa ni moja na ambalo linanifanya nishindwe kuoanisha most of dots and details you have provided nalo ni kwamba Anna hakuwa chaguo la mafisadi na kwamba walipambana naye sana asirudi bungeni lakini wameshindwa. Swali langu mimi kubwa ni moja, mimi natoka Njombe na bahati nzuri najua kidogo upepo ulivyokuwa huko.
Anna alipita bila kupingwa katika mchakato wa ubunge na hivyo ilikuwa kazi rahisi kwake kusonga mbele, sasa hiyo nguvu ya ziada ilihitajika wapi naomba unieleweshe mkuu
 


- Kwenye siasa za kisasa hakuna kuchaguliwa bila kupingwa kama kweli unatokea jimboni kwake, then ulipaswa kujua mengi yaliyotokea huko katika kujaribu kumzuia asirudi bungeni, mtu anayechaguliwa bila kupingwa hawezi kutumia muda mwingi sana jimboni wakati wa uchaguz,hope nimekusaidia.


William.
 

Ana mtoto mwingine wa kiume....namfahamu fika mkuu lete data za uhakika.
 

Agreed!ni mbena na ukabila wanao ndio haohao pamoja na kina Makweta, Thomas Nyimbo wote ni wabena na sio wahehe!
 

Ndg William,

Ni wazi kabisa Tanzania ya mwaka 1961 sio Tanzania ya leo. Nakubaliana na wewe kabisa kwamba Mama Makinda ni spika wa CCM na amechaguliwa kuendeleza policy za CCM. Hapo kwa watu wenye ueleo tunafahamu kabisa kwamba kanzu ndio mpya lakini shekh ni yule yule. Ukweli ni kwamba hakuna kipya tutakacho kiona kwa huyu mama. Tusahau mchakato mzima wa kubadilisha vifungu kibao vya katiba na mambo mengine.

Mabishano yangu ni kwa wale wanao tetea kwamba huyu mama ni substantial leader. Kusema kweli hakuna hata mmoja aliyekuja hapa akasema kwamba wakati huyu mama akiwa body ya Mwatex alihoji matumizi mabaya ya xxx or wakati huyu mama akiwa naibu waziri fulani alihoji kadha wa kadha.

Mwisho kama huyu mama ameshindwa kufanya mabadiliko katika sekta zote alizofanya kwa miaka 35, jee atabadilisha mfumo wa bunge kwa miaka 5? I doubt.
 

Hiyo advanced diploma ilikuwa inachukua miaka minne au mitatu? Kuna repeat a year nini hapo?
 
sio uongo....huyo kijana jina lake aliitwa maurice ....ni mtoto wa anna makinda banaa alisomea arusha.

Anna Makinda ana mtoto mmoja tu wa kike, na ndiyo anavyojieleza mwenyewe. Hakuna mwanamke anayekana mwanae. Tungekuwa tunazungumzia mwanaume hapa ningefikiria mara mbili kuwa huenda kuna mahali alipitia na anataka iwe siri kwa mkewe, lakini wanawake huwa hawafichi wala kukataa watoto wao. Ana mtoto mmoja tu huyu mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…