TANZIA Anne Rwigara afariki dunia. Ni dada wa Diane aliyejaribu kugombea Urais dhidi ya Kagame. Mama asema kifo hicho ni fumbo

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,525
10,762
63a52c10-a5ca-11ee-a15c-e9b847c42861.jpg

IMG_7350.jpeg


Anne Rwigara wa Rwanda amefariki dunia huku Mamake Anne alinukuliwa akisema kifo cha bintiye kilikuwa "fumbo" kwani hakuwa mgonjwa.

Vyanzo kadhaa vinashiriki maelezo ya kuhuzunisha ya kifo chake, vikidai kwamba baada ya masaa nane ya kulalamika kuhusu maumivu ya tumbo, viungo vingi vya mwili wake vilishindwa kifanya kazi. Hatua hiyo inachochea uvumi wa sumu kuwa huenda aliwekewa sumu

Huku uchaguzi wa Rwanda ukikaribia, Watumiaji wengi wa mitandao ya Kijamii wanaelezea wasiwasi wao kwamba kifo chake kinaweza kuwa jaribio la kuzima sauti za upinzani kabisa, hata kama Jumuiya ya Kimataifa inaangalia kwa karibu maendeleo katika nchi ya Rwanda

Hii Familia ya Rwigara iliingia kwenye mgogoro mkubwa zaidi na Rais Kagame baada ya Diane ambaye ni Dada wa Anne kutangaza nia ya Kumpinga kwenye uchaguzi. Kwanza walikamatwa na kuwekwa gerezani, walinyang’anywa utajiri wa familia yao ikiwa ni pamoja na Kiwanda chao cha Tumbaku. Na wakowa gerezani inadaiwa walikuwa wakipatiwa mateso

Historia Fupi

Baba yake inadaiwa aliuawa katika ‘ajali ya gari iliyotengenezwa’ Mwaka 2015, baadaye dada yake mkubwa Diane Rwigara aliingia katika siasa za Rwanda na kutangaza kugombea urais; kwa bahati mbaya aliwekwa gerezani na Kagame kwa kujaribu kumpinga; baadae Mama yake na Anne mwaka 2017 pia waliwekwa gerezani kwa kusema juu ya mateso ya familia yao na baada ya hapo Waliachiwa na kukimbilia uhamishoni, Marekani.

Mwenyezi Mungu aipe haki familia ya Rwigara na Wanyarwanda wote wanaoteseka mikononi mwa utawala wa Kagame Rwanda.

fbd2ff30-a5ca-11ee-beb5-e1400df560f2.jpg
 
Back
Top Bottom