nimesoma kwa tahadhari taarifa ya Mama Makinda kuhusu kutogombea tena ubunge huko kwake njombe, lakini hakuna mahali popote pale aliposema ataachana na siasa. wengi mwameanza kumpa hongera, lakini ukweli ni kuwa hatagombea tena ubunge wenye maslahi duni bali USPIKA
katiba ya nchi yetu inatamka wazi kuwa spika si lazima awe mbunge, na anajua kuwa anaweza kugombea uspika bila kugombea ubunge.
hii haitakuwa mara ya kwanza. mnamo mwaka 2000, piuce msekwa alitangaza kuwa asingegombea tena ubunge wa jimbo la ukerewe, na kweli hakugombea ubunge kiti kile akamwachia mama mongela getrude, yeye aligombea uspika na alikuwa spika kwa kipindi cha 2000-2005 bila kuwa mbunge.
nawsilisha