Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,199
MAUAJI YA RAIA NA HII SERIKALI YA KIKWETE WANANCHI TUNASEMA SASA TUMEFIKA MWISHO WA UVUMILIVU WETU WALA HATUTAKI KUSIKIA TEN!!!!!!!
Viongozi walioko madarakani pindi wanapotafsiriwa kuwasaliti wananchi 'tuliowachagua' hadi hapo wanafanya maisha kuwa ni hatari tupu hata kwa viongozi wastaafu ambao pen gine wao awamu zao walifanya kazi nzuri tu.
Kitendo cha viongozi wote hawa kunyamazi bila hatua zozote stahiki pindi polisi wanapoendelea na Mauaji ya Raia kila kona ya nchi, Umma wa Tanzania tumefika mahala tunasema SASA BASI HATUTAKI TENA KUSIKIA KITU WAZIRI PICHA HAPO MAMBO YA NDANI, MA-RPC MA-KADA WA CCM, MKUU WA MKOA WALA KITU GANI kutukaribia maana wameonyesha kuwa hawko kwa ajili yetu tena katika maisha haya!!!!!!!
Viongozi walioko madarakani pindi wanapotafsiriwa kuwasaliti wananchi 'tuliowachagua' hadi hapo wanafanya maisha kuwa ni hatari tupu hata kwa viongozi wastaafu ambao pen gine wao awamu zao walifanya kazi nzuri tu.
Kitendo cha viongozi wote hawa kunyamazi bila hatua zozote stahiki pindi polisi wanapoendelea na Mauaji ya Raia kila kona ya nchi, Umma wa Tanzania tumefika mahala tunasema SASA BASI HATUTAKI TENA KUSIKIA KITU WAZIRI PICHA HAPO MAMBO YA NDANI, MA-RPC MA-KADA WA CCM, MKUU WA MKOA WALA KITU GANI kutukaribia maana wameonyesha kuwa hawko kwa ajili yetu tena katika maisha haya!!!!!!!
KAMA VIONGOZI WETO WOTE WAMEAMUA KWA DHATI KUSALITI 'HAKI YA KUISHI NA USALAMA WA MALI ZETU' KIASI HIKI SASA SERIKALI YENYEWE INAKUA NA MAANA KWA VIONGOZI WENYEWE AU SISI WANANCHI WALIPA KODI???????
Kijana umeongea kwa uchungu wa hali ya juu sana na yote ulioyataja humu ni ROBO TU ya jinsi gani tunavyowaona zaidi ya asilimia 98 % ya mbegu ya viongozi tulionao hivi sasa katika nchi yetu.
Mpaka hapa hakika mjue ya kwamba pindi mnapoendelea hata kwa robo hatua kwa kutuambia eti mchote tena kodi zetu ziwe posho zaidi kwenu, eti maisha Tanzania hii sasa ni magumu tu kwa hawa viongozi wanaofilisi taifa letu ...,
... nasema tunapoendelea kusikia eti hata MAFISADI waliokubuhu nao bado wanaendelea kuonekana wakirandaranda mitaani kutaka wakatuongoze tena badala ya kujivua gamba ...,
... kwa uhakika pindi vijana wa taifa hili tunapoendelea kushuhudia eti wengine wakiagiza polisi watuue raia na kutubandika nembo za WAHUNI pindi tunapoandamana kudai HAKI YA KI-KATIBA NA JUKUMU NAMBA MOJA YA serikali kutulinda na mali zetu ...
Mpaka hapo wenzetu ni kama vile akili zinataka kuturuka vile, ni kama vile wengine tunatamani kwenda kuondoa kabisa uozo wa aina hii kwa mikono yetu bila kuendelea kuhesabu vifo zaidi nchini; mkoa baada ya mkoa. Rai Kikwete kwa uhakika, kachukuwe hatua za dharura KUKOMESHA hii hulka mpya ya DOLA kuwaua raia kinyama kiasi hiki.
Mpaka hapa ni kwamba tungependa ieleweke kwamba HATUTOPENDEZEWA kuona vifo zaidi ya raia hata mmoja wakati kodi zetu polisi na jeshi letu wakiendelea kulipwa kila mwezi.
Nasema kwamba wala haitusaidii kitu kuendelea kuwa na viongozi sanamu sawa na picha tu ukutani kwa jina la Vuai Nahodha, Saed Mwema, Mkuu wa Mkoa, Wilaya na RPC huko Ruvuma wakati raia tukiendelea kuchinjwa na waajiriwa wetu wenyewe kwa mtaji wa kodi zetu!!
a. Wanaharakati mko wapi au mnasubiri tu kuja kuandika mi-ripoti ndefu mara baada ya familia kadhaa nchini kupoteza zaidi y nusu ya ukoo wao?
b. UDASA huu ukimya wenu tafsiri yake ni kujiunga na mdhulumishi au tuwaelewe vipi?
c. Tangnyika Law Society ndio tuseme mpaka O'Campo awe ametoa neno ndio mtiririko wote huu wa mauaji katika mkoa mmoja baada ya nyingine ipate kuwagusa?
d. Akina Mama kwenye taasisi zenu zote kama vile UWT inamaana uchungu wa mtoto wa mke mwenzio wala haukuhusu kitu isipokua ni jukumu la Mama Nkya na Kijo Bisimba peke yao sio?
e. Enyi wanafunzi wa vyo vikuu nchini mliopata kua VIWAKILISHI VYA SAUTI YA HAKI KATIKA JAMII, mnaona ni vema hadi afe mtu wa ngapi tangu Mauaji ya raia Mwembechai, Pemba, Arusha, Igunga, Musoma, Uyole-Mbeya, na sasa Songea, ndio mpate hata kuguna tu juu ya mwenendo wote huu wa mambo?
f. Kamisheni na taasisi zote za haki za binadamu nchini, inamaana hata kukemea tu muaji haya yote ni mpaka kupatikane mfadhili kutoka nje ya nchi ndio akawape fedha ndio mpate kutekeleza majukumu yenu?
g. Vyombo vya maamuzi ya Juu nchini kama vile NEC-CHADEMA, NEC-CCM, Baraza la Mawaziri na Taasisi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi kweli vikao vya dharura mtaweza kuviitisha tu pindi mambo ya kisiasa yanapowaendeeni vibaya kwa njia moja au nyingine na wala si kule KUTOLEWA ROHO Mtanzania mwenzetu??
h. Hivi kweli Tanzania tumefika mahala ambapo uhai wa raia ni sawa tu na uhai wa inzi na wala halichukuliwi kwa uzito wake kama ambavyo tumewahi kusikia enzi hizo Mzee Mwinyi alipokua Waziri wa Mambo ya Ndani?
i. Wazee wetu tunaowaheshimu saaana katika taifa hili; Joseph Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Benjamin Mkapa, Edwin Mtei, Bob Makani, Mufti Mkuu Sheikh Simba, Mwashamu Askofu Polycarp Pengo, Jenerali Ulimwengu, Rejnald Mengi, Mzee Bahresa ...
... je ukimya wenu wote huu wakati Dola ikiendelea kuua mkoa hadi mkoa ndio tuseme ni usaliti au usahihi wa msimamo wenu kutetea jukumu mama kikatiba kulinda uhai wa kila Mtanzania na mali zake au mpaka vurugu zije zitukumbe ndio mje kuanza kukatisha kushoto kulia.
Kamati ya kutumu ya Bunge kuhusu ulinzi na usalama, tunaomba maelezo kuhusu mauaji yote haya huku Rais Kikwete yeye akiendelea tu na safari zake za huko na kule kama vile hakuna cha ajabu kinachotokea ndani ya nchi yetu.
Kwa kweli kwa jinsi mambo yanavyoeneda hivi sasa na kwa usahihi ambao huyu Ndugu KweleaKwelea wa JF ameweza kubainisha kero za ndani kabisa wa kila kijana ndani ya nchi hii, napenda kusema kwamba NAUNGA MKONO karipio kali kwenye hotuba ya Mhe Dr Slaa, alioitoa hapo jana jijini Dar es Salaam, neno kwa neno na nukta kwa nukta bila ajizi!!