Anne Makinda: Sitogombea tena ubunge 2015

Kwanini asifanye kujiuzulu kabisa sasa hivi ili tujaribu kuhisi anauchungu na nchi yake ambayo chama chake kimeinyonya mpaka imekuwa masikini kama nchi ambayo iko vitani
 
Mh. Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano amesema kuwa hato gombea ubunge chaguzi mkuu ujao. Amesema anataka kukopa pesa arudi kujenga nyumba.

Sorce: ITV, HABARI YA SAA MBILI

Huu ujenzi wa nyumba inamaanisha MRADI WA NYUMBA (real estate) au yakwake kuishi?
 
Hana jipya!
Amechoka akili na mwili, na anaelewa wazi kuwa changamoto za Bunge la sasa hatakaa aziweze!...Watu kama akina Tundu Lisu ni mwiba sana kwake, na anajua kuwa 2015 wataingia vijana matata zaidi na wabishi mno!
Namsifu kwa kuona zaidi ya pua yake!

Naona wengi mnakosa point anayo iongea makinda.
Kasema hata gombea tena ubunge,............Kauli kama hii alisha itoa Sitta pia.

Wote hawa wana maanisha kwamba watakuwa kwenye mchakato na mchanyato
wa kuingia Ikulu,.........subirini watakavyo kwaruzana huko............
 
bungeni ni eneo la kumfanya mtu kuwa maskini na sio tajiri na yeye amekopa pesa benki ili jange nyumba by spika makinda chanzo ITV & TBC 1 na pia metangaza kustafaa 2015

Duu kama makinda ni maskini basi hatari,nikianza kuorodhesha mali zake ni aibu,kwani lile ghorofa alilojenga akazuia na njia kashahamia?
Zile Shule zake za secondary kashaanza usajiri wa wanafunzi?
 
Nikiwa primary sch. miaka ya 1980, huyu mama tayari alishakuwa mbunge! Leo hii eti akakope pesa ya kujengea nyumba! Alikuwa wapi muda wote? Na hizo fedha za ubunge alikuwa anapeleka wapi?

Alikuwa anapeleka kwa Serengeti Boyz!
 
Mh. Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano amesema kuwa hato gombea ubunge chaguzi mkuu ujao. Amesema anataka kukopa pesa arudi kujenga nyumba.

Sorce: ITV, HABARI YA SAA MBILI
nyumba ipi... Ile ya knyama aliyofunga barabara kauza?
 
Akiongea na wananch wake hko jimbon kwake anne mkinda(mb) ambaye pia ni sipika wa bunge ametoa tamko tena kuhusiana na tatzo la posho za wabunge(sitting allawance),amesema kuwa zile posho watalipwa wale tu watakao hudhuria vikao vya bunge na ni kwa siku 9 tu baada ya hapo hakuna posho wala nin!! Sasa hapo wabunge miatatu na nazaidi mara kila mbunge 330000 kwa siku tisa ni shilingi ngapi? Na kuna miradi mingapi ya muhimu inakosa pesa ya kuendeshea kwa kisingzio kuwa serikali haina pesa? Tunakwenda wapi watanzania!
 
wabunge wana mpango wa kufua posho zote kama kisasi ..mother anataka azifute ndio aondoke zake..aende zake
 
Naona wengi mnakosa point anayo iongea makinda.
Kasema hata gombea tena ubunge,............Kauli kama hii alisha itoa Sitta pia.

Wote hawa wana maanisha kwamba watakuwa kwenye mchakato na mchanyato
wa kuingia Ikulu,.........subirini watakavyo kwaruzana huko............

unamaanisha huyu naye anataka kugombea? kwa kigezo gani? cha uanamke kama alivyoukwaa u spika? ...nitaingia msituni huyu maama akipewa
 
unamaanisha huyu naye anataka kugombea? kwa kigezo gani? cha uanamke kama alivyoukwaa u spika? ...nitaingia msituni huyu maama akipewa

Ndiyo maana yake,............
Haujasikia zamu ijayo iwe ya mwanamke ?haha
 
huyu ni muongo yale mabasi ya SUPER FEO DAR- SONGEA NI YAKE PESA KAZIONA WAPI?
Nakusanya ushahidi kuhusu mali zake nikiukamilisha nitaumwaga hapa jamvini.
 
Unajua wakati mwingine ni kama watawala wetu wanatufikiria kuwa sisi ni mazezeta wa aina fulani hivi; sasa kama mtu analia umaskini na kuwa ni Bungeni ni sehemu ya umaskini wa "kutupwa" kwanini anataka kusubiri hadi 2015? Kwanini asiamue - katika jitihada za kuukwepa umaskini - kuachia ngazi sasa hivi akaende kufanya shughuli zake binafsi?
 
Makinda ni janga kubwa sana la Taifa. Unfortunately watu wa aina ya Makinda wapo wengi sana kwenye madaraka yanawapa mamlaka ya kufanya maamuzi yanayohusu mstakhabari wa taifa hili; ndiyo maana Taifa hili linapiga maktaimu tu, wakati mataifa ya wenzetu yakisonga mbele.
 
Mbon sijakielewa mkuu. Siku 9 za nini? Kwani vikao vya bunge huwa ni siku 9 au alikuwa na maana gani?
Fafanua ili tupate muktadha wa bandiko lako.
 
Back
Top Bottom