Kwa hiyo mkuu unaamini kabisa ndugu Mbunge alipanga vyema vipaumbele hapo.wakati taifa linajadili ripoti nyeti yeye yupo Same!
Kazi za mbunge ni kujenga viwanda kweli!!hiyo inapatikana wapi katika majukumu ya kikatiba ya mbunge!Kwa mwendo huo hatashindwa kuwagawia wananchi kanga na chumvi!
Moja ya majukumu ya Kikatiba ya mwakilishi wa wananchi ni kuiwajibisha serikali..Kushiriki majadiliano juu ya ropoti ya CAG ni moja ya majukumu yake ya msingi kabisa.Sasa ana tofauti gani kimsingi na Mkulo kwenda Marekani wakati wizara yake inajadiliwa...wabunge wote wakiamua kuiga ubunifu wa Ndugu Kilango nani atabaki bungeni kuiwajibisha serikali!
Kuhusu msimamo wake kuhusu nafasi ya wakuu wa wilaya,ni kama alikuwa analenga kuwatetea wakuu wa wilaya na CCM na si wananchi.
Anaelewa ,nawe waelewa ,kuwa wengi wa wakuu wa wilaya ni makada wa CCM wasio na elimu wala uwezo wa kutosha kuongoza wananachi...Anajua ,kama nawe ujuavyo, kuwa wengi wa ma DED si makada wa CCM,wengi wao ni technocrats na wasioyumbishwa kirahisi na watawala.Siamini kama kweli alitenda haki kwa wananchi wa SAME katika hili.