William!
Usitake kudanganya wana jamvi. Mali ghafi ya kiwanda hiki cha Tangawizi hapa Mamba au kiwanda kingine? Kama ni kiwanda cha tangawizi hapa Mamba, wewe na Mh. Kilango ni waongo wakubwa. Kiwanda hiki kilishakufa siku nyingi. Kilicho baki ni kudanganya umma ambao haupo hapa Mamba kwamba eti kuna Kiwanda cha Tangawizi. Kwanza wakulima wa tangawizi wote tulisha wafukuza kwa kusababisha ukame usio na kipimo hapa Mamba. Na sasa wamehamia maeneo ya Gonja Mpirani, Maore ikiwa ni pamoja na kuchangia kuharibu msitu wa hifadhi unao tenganisha Mpirani na Maore. Na tayari kumeshaanza kutokuelewana kati ya wakulima wa mpunga na wa tangawizi kwa kile kinachoonekana ni ukosefu wa maji kwa ajili ya kilino cha mpunga. Na wapo mbioni kufukuzwa na wananchi wa vijiji tajwa. Hata hivyo, wanapo vuna tangawizi zao, wanapeleka moja kwa moja kwenye masoko yenye bei kubwa na si kudanganywa eti na kiwanda cha tangawizi kilicho jaa ufisadi unao simamiwa na yule mama.
Mwisho, ningekushauri uwe unafabya utafiti kabla ya kutolea majibu habari usiyo kuwa na uhakika nayo.