Mbogela,
Hata West wana grade. Nina jamaa zangu wawili ma Dr. huko UK na wote wanasema wazi kabisa kuwa kuna classes.
Ila ukweli ni kuwa tofauti zao ni ndogo na si kubwa sana kama zetu. Sanasana anasema kuwa kule kuwaona wale Madr. bingwa ndiyo kimbembe. Sanasana utaishia huko kwa akina dr........... Yale majina makubwa yamewekwa kwa ajili ya watu wenye hela zao, majina yao na labda USUBIRI na tena kwa kipindi kirefu.
Ila ukweli ni kuwa heri utibiwe UK kwenye low class kuliko Tanzania kwenye high class. Hii ndiyo tofauti iliyopo..........
Mkuu Sikonge,
Hapa UK kama uko NHS hakuna grades, huyo aliyekuambia labda alikuwa anaongelea kitu kingine.
Kuna baadhi ya hospitali wana baadhi ya vyumba vichache kama unataka kulala chumba peke yako basi unalipia kidogo na unalala peke yako. Baadhi ya magonjwa unapewa chumba chako kwahiyo wala hata sio muhimu.
Pesa unayolipia ni ndogo sana kiasi kwamba hata sisi walala hoi tunaweza kama unataka kusiwe na usumbufu wa watu wengi.
Viongozi karibu wote wa serikali hapa wanatibiwa NHS, ni matajiri na wafanyabiashara ambao baadhi yao wanaenda private.
Katika miaka yangu yote ya kukaa hapa sijaona grades. Kingine kilichopo ni kwamba baadhi ya hospitali ni nzuri kuliko zingine. Kwa mfano ukiwa London kwasababu ya watu wengi huduma inaweza kuwa mbaya ukilinganisha na mikoani lakini hospitali kama ni mbaya inawahusu wote maskini mpaka matajiri.
Mtu asikudanganye kama wewe ni maskini UK ni best kwa huduma ya afya, hakuna cha insurance au nini, kila mtu ana haki ya kutibiwa. Hata USA wanatuonea wivu kwa hilo.
Hiyo ya Tanzania ni aibu tupu; hiyo mizee inaunguza mabilioni hapa UK na SA kwa matibabu fake huku hospitali zetu zinakufa. Hata huyo mama Kilango angelazwa tu kule kwa wengine ili labda waone kwamba hizo pesa wanazounguza Ulaya kwa kisingizio cha matibabu ndizo zingetakiwa kutengeneza hospitali zetu.
Operation kama yake hiyo ilitakiwa hata atoke hapo hapo kama tungekuwa tunafanya investment kubwa kwenye huduma za afya. Wanasiasa wa Tanzania ni wajinga mno, kuanzia CCM mpaka upinzani. Ambacho hawajui ni kwamba mpaka ukimbizwe kutibiwa Ulaya tayari ugonjwa unakuwa umeshazagaa na wanaishia kufa tu.