Anne Kilango alazwa Hospitali Dodoma

Mkuu Sikonge,

Hapa UK kama uko NHS hakuna grades, huyo aliyekuambia labda alikuwa anaongelea kitu kingine.

Mtu asikudanganye kama wewe ni maskini UK ni best kwa huduma ya afya, hakuna cha insurance au nini, kila mtu ana haki ya kutibiwa. Hata USA wanatuonea wivu kwa hilo.

Operation kama yake hiyo ilitakiwa hata atoke hapo hapo kama tungekuwa tunafanya investment kubwa kwenye huduma za afya. Wanasiasa wa Tanzania ni wajinga mno, kuanzia CCM mpaka upinzani.

Mkuu hilo ndio swala ambalo wengi wetu hawajui bado. UK wanatumia system inaitwa public health system, yaani huduma ya afya inalipwa na serikali na western/continental Europe kama Uholanzi na nyingine wanatumia mfumo wa private wenye insurance, na serikali inasimamia ubora na tija ya huduma, lakini wamekubaliana kuwa kila mtu ana haki ya kupata huduma, alafu mashirika ya BIMA yanashindana kwa kutoa huduma Bora kwa pesa kidogo sana. USA ingawa wanahuduama nzuri ukilinganisha na mataifa mengi lakini wapo Nyuma sana ukilinganisha na nchi nyingi za ulaya. Kwa hiyo tanzania inatakiwa kufuata mfumo wa Ulaya au CUBA
 
Amesharuhusiwa kutoka hospitali leo na yuko home anaendelea vema. Hao wanaosema yu mahututi mh!!!!!!
 
Mkuu hilo ndio swala ambalo wengi wetu hawajui bado. UK wanatumia system inaitwa public health system, yaani huduma ya afya inalipwa na serikali na western/continental Europe kama Uholanzi na nyingine wanatumia mfumo wa private wenye insurance, na serikali inasimamia ubora na tija ya huduma, lakini wamekubaliana kuwa kila mtu ana haki ya kupata huduma, alafu mashirika ya BIMA yanashindana kwa kutoa huduma Bora kwa pesa kidogo sana. USA ingawa wanahuduama nzuri ukilinganisha na mataifa mengi lakini wapo Nyuma sana ukilinganisha na nchi nyingi za ulaya. Kwa hiyo tanzania inatakiwa kufuata mfumo wa Ulaya au CUBA
Mbogela,

Kwa kiasi ni kama ulivyoelezea. Nina experience na systems karibu zote za Europe. Scandinavia na Holland kwa mfano wanaongoza kwa ubora wa hospitali zao. Wagonjwa wengi wana vyumba vyao na huduma nzuri. Inatakiwa uwe na bima na hiyo ndio inalipia. Kwa wenyeji hata kama hana kazi bado kuna utaratibu wa bima yake kulipiwa na serikali. Tatizo ni watu wa kuja au wanaopita.

UK hakuna bima kwenye afya ila wengi wetu tunalipa national insurance kupitia kwenye mishahara. Lakini huduma ni bure kwa kila mtu hata mtu aliyetua leo toka TZ anatibiwa bure ili mradi sio ugonjwa wa muda mrefu au magonjwa makubwa kama cancer nk. Quality kwenye hospitali zetu sio nzuri sana, huwezi kulinganisha na Scandinavia, ila tu kila mtu anapata huduma sawa. Pia kuna vifaa muhimu na vya kisasa kwasababu ni pesa ya serikali na hospitali huwa hawajali sana kuzitumia. Hapa pia kuna private hospitals lakini hata kama una bima lazima kwanza upitie NHS ndio wakuruhusu kwenda huko, vinginevyo unalipa mwenyewe.

Hiyo ya USA ndio balaa kabisa labda kama una bima yako au ni tajiri.

Uzuri wa UK kama ni mwanasiasa inatakiwa utibiwe sawa na sisi walala hoi vinginevyo wewe sahau kuwa kwenye siasa kwa muda mrefu. Watoto wa Brown wamezaliwa kwenye hospitali hizi hizi na hata aliyekufa, alifia kwenye hospitali hizi hizi. Hivyo hivyo kwa huyo mwingine ambaye anategemea awe PM mwakani, yeye ni tajiri lakini bado mtoto wake aliyekuwa mgonjwa kahudumiwa muda wake wote na NHS mpaka anakufa.

Sisi Watanzania tumeruhusu wanasiasa wetu waue hospitali zetu halafu bado tunawachague. Huo ni ujinga uliozidi kikomo.
 
Mawazo mbadala ya KP!
Mbunge Kilango amekuwa ni mwiba mkali katika mapambano dhidi ya mafisadi hapa nchini.
Wiki iliyopita, Mbunge huyo aliitia kiwewe Wizara ya Mali Asili na Utalii baada ya kutoa kauli kuwa atawasilisha hoja bungeni ya kutaka kuundwa kwa kamati itakayochunguza wizi wa nyara za serikali zilizobainika nchini Vietnam na Ufilipino hivi karibuni iwapo hatapewa maelezo ya kuridhisha na Waziri wa wizara hiyo, Shamsa Mwangunga.
Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wengi ambapo wakati wa kujibu hoja za wabunge, Waziri Mwangunga alimsihi Mbunge huyo kutowasilisha hoja hiyo kwani tayari serikali ilikwishaanza kuchukua hatua juu ya suala hilo.
 
Mbogela,
Hiyo ya USA ndio balaa kabisa labda kama una bima yako au ni tajiri.

Uzuri wa UK kama ni mwanasiasa inatakiwa utibiwe sawa na sisi walala hoi vinginevyo wewe sahau kuwa kwenye siasa kwa muda mrefu. Watoto wa Brown wamezaliwa kwenye hospitali hizi hizi na hata aliyekufa, alifia kwenye hospitali hizi hizi. Hivyo hivyo kwa huyo mwingine ambaye anategemea awe PM mwakani, yeye ni tajiri lakini bado mtoto wake aliyekuwa mgonjwa kahudumiwa muda wake wote na NHS mpaka anakufa.

Sisi Watanzania tumeruhusu wanasiasa wetu waue hospitali zetu halafu bado tunawachague. Huo ni ujinga uliozidi kikomo.

Nchi Kama Cuba zina GDP ndogo na pia zina Expenditure ndogo lakini quality ya huduma yake ya afya ipo juu kuzishinda nchi nyingi karibu zote. Sasa Mtanzania hawezi kuona kuwa kwa wenzetu mtu ndani ya nchi yake mwenyewe hawezi kwanda kutibiwa katika hospitali ya binafsi (ingawa tofauti ni ndogo) Je hawa wanaoenda nje ya nchi kutoka nchini kwetu si ndio tuwapige marufuku kabisa???
 
Last edited:
Unaona ukiwa shujaa unavyoliliwa hata ukiugua mafua. Kuna wakati Zitto Kabwe aliugua nadhani ni kwa uchovu uliompata huko Tanga. Alipochukuliwa vipimo kwenye pale Muhimbili picha zilitawala magazeti na pole nyingi.

Shujaa mwingine Mwakyembe alipata ajali tumejaza page za pole hapa JF.

Leo Iron Lady (Nimbatize hivyo) Mama Malecela kasema mwenyewe ni kaugonjwa kadogo tumashajaza page tatu sasa.

Tuendelee kuwalinda (moral support) hao mashujaa wetu hata wakimuwa na sisimizi.

Tena tuombe mmoja wao asije akaporomoka toka kwenye jukwaa wakati anafunga kampeni kama ilivyotokea siku zinafungwa kampeni za mwaka 2005.
 
I love this mama kwa kweli, hebu angalia uzalendo wake angekuwa yule mama Fisadi Meghji lazima tungeambiwa amekimbizwa UK kama si US ama SA kwa matibabu!
 
I love this mama kwa kweli, hebu angalia uzalendo wake angekuwa yule mama Fisadi Meghji lazima tungeambiwa amekimbizwa UK kama si US ama SA kwa matibabu!

Hivi kuna ambaye angehangaika kutoa pole kama zinavyomiminika hapa?
 
Mbogela,
Nakwambia ukienda hospital ya mkoa wa Kagera pale Bukoba leo utasikitika na machozi yatakutoka tu. Hasa kama uliwahi kuiona miaka 7 iliyopita.

Hospitali hii kwa ajili ya mambo ya ukimwi Danida walitoa ufadhili wa kuijenga tena upya miaka kama 8 iliyopita.

Walibomoa majengo ya zamani karibu yote na kuyajenga upya tena kwa kisasa kabisa.

Wali furnish karibu kila jengo kama lilivyokuwa linatakiwa. Walijenga vyoo vya kisasa kila mahali na kwenye Wards nakwambia kila kitu kilikuwa utadhani ulaya vile, maji ya moto, vyoo safi sana n.k.

Mimi nilidhani labda wanajenga hili iwe mfano kwa serikali yetu maana xray, na vile vyumba vya upasuaji waliweka vitu vipya tena vya kisasa ambavyo si rahisi kuamini.

Walijenga jiko, nyumba ya kuhifadhi maiti na kote walikuwa waki equip na vifaa vya kisasa vilivyoletwa toka ulaya tena vipya si vizee.

Waliweka vitanda vipya na hata mashuka na mosquito nets vyote vipya.
Machine za kufulia nguo za wagonjwa.

Machine ya kuchoma takataka hatari kama viungo na sindano etc waliweka pia na mahabara ya kisasa iliyo equiped(recently wameikarabati zaidi), waliweka standaby generator kubwa sana mpya kama mbili vile.

sina la kusimulia kwa kweli maana hata mazingira waliyajenga. Fikiri mtu anakutengenezea mpaka garden ya nyasi na maua.

Sasa funga kazi, we nenda uangalie miaka kumi hata haijaisha uone kituko.

Vitu vingi havifanyi kazi tena kama kawaida. Net za madirisha kwa ajili ya kuzuia mbu zimechanika ovyo. Kuta chafu wala hazioshwi kabisa.
Wards kama si wagonjwa wenyewe kujitolea hakuna usafi kabisa maana hazidekiwi.

Mashuka yamechanika na hayafuliwi. Ukiwa admitted unapewa la marehemu fulani aliyekuwa kalala pale unapokwenda kulazwa.
Yaani ni aibu ni aibu ni aibu hatakusimulia.

Nashindwa kuamini kama watanzania hata kama mtu atatupatia nini kama tunaweza. Maana nikiangalia kituko cha hospitali hii nashindwa kuamini kama kuna serikali na kama inakwenda mbele au nyuma.

Sishangai kuona mama kilango kalala kwenye chumba kama hicho, lakini nashangaa kama kwa uweza wake kama mbunge ameridhika!

Nashangaa kuona asiporidhika anatoa pesa ya walipa kodi kwenda ulaya na India wakati hata tulivyojengewa bure hatuvithamini.

Mungu tusaidie. Tuondoe katika ujinga huu na tuondoe kwenye mikono ya hawa viongozi wabadhirifu na wezi tu.
ggggggggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Back
Top Bottom