Anime

Anime

Binafsi Anime yangu pendwa ni Ippo Hajime Makonouchi hii hata week iliyoosha nimetoka kuiludia ...

Japo sidhani kama watatoa mwendelezo wake nipo nasikiliza watoe manga ya mwezi huu hapa niliishia sehemu nzuri sana

Baada ya hapo Attack On Titan ipo kwenye ratiba zangu nikiboeka tuu naangalia namkubali sana mwamba wangu Levi Ackerman na kichaa wake HangeView attachment 3411213

Solo Leveling Mwaka huu walijua kutushika Season 2 imekuwa ya moto mno...

Nipo nangojea Kaiju No 8 niliambiwa mwezi huu wataachia
mkuu right now nipo naingalia conny kamkuta maza wake kawa titan ila hajamjua. Hii series imenifanya nilale saa kumi za usiku miaka ya 2022.
Ps.
Nitajie anime kali ulizotazama nitafuatilia mojamoja
 
mkuu right now nipo naingalia conny kamkuta maza wake kawa titan ila hajamjua. Hii series imenifanya nilale saa kumi za usiku miaka ya 2022.
Ps.
Nitajie anime kali ulizotazama nitafuatilia mojamoja
Kwa haraka haraka nitakuambia Solo Leveling na Demon Slayer humu pia walitulia



Umenikumbusha niangalie hata season moja AOT kama ambavyo wewe huwa huichoki GOT😃😃😃


Recommendations nyingine zipate kwa mkuu Mwananchi B yeye ameangalia nyingi kuniliko na hata zangu kuangalia natoa kwake
 
Lord of Mysteries
Screenshot_2025-09-19-17-33-43-536_com.google.android.googlequicksearchbox.png
 
Duh hawa jamaa wanapiga pesa. Hivi na Africa tukitengeneza Anime ya Demon Hunting ambapo demons walikuwa wanaattack African villagers miaka 800BC, kukawa na demons wana majina ya Kibantu na kuwe na superheroes wa jadi ambao wanawinda hao demons, na ikawa kali. Itauza kweli huko mambele 🤔 au ndo itakuwa ni kuambulia hasara tu 😅
 
Duh hawa jamaa wanapiga pesa. Hivi na Africa tukitengeneza Anime ya Demon Hunting ambapo demons walikuwa wanaattack African villagers miaka 800BC, kukawa na demons wana majina ya Kibantu na kuwe na superheroes wa jadi ambao wanawinda hao demons, na ikawa kali. Itauza kweli huko mambele 🤔 au ndo itakuwa ni kuambulia hasara tu 😅
Ha ha ha inawezekana, inshu ni idea nzuri, mpangilio Mzuri wa Stori, uniqueness ya dialogue bila kusahau technology nzuri.
 
Habari wana Jamii Forums!
Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala hapa JF, na nimegundua kuna uhaba wa mada kuhusu Anime na Manga, hususan zile za Kijapani.

Mimi ni mgeni kwenye ulimwengu huu, nimeanza kuangalia Anime mwaka 2024 na nimezipenda sana! Nilishangaa sana kuona hakuna mada rasmi kuhusu hili hapa JF hadi leo.

Kwa wale ambao hamjui, Anime ni filamu za katuni zinazotengenezwa nchini Japani. Zina mtindo wa kipekee wa michoro na hadithi mbalimbali, kuanzia vichekesho, kusisimua, mapenzi, hadi sayansi. Manga kwa upande mwingine, ni vitabu vya katuni au riwaya za picha za Kijapani ambazo mara nyingi huwa ndio chimbuko la hadithi za Anime.

Kwanini Anime Inavutia?
Kuna mambo mengi yanayofanya Anime ivutie:

Hadithi Pekee: Zina hadithi za kusisimua na zenye undani, zinazokuvuta na kukuweka mtegoni.

Wahusika Wenye Undani: Wahusika wake huwa na maisha halisi, matatizo, na ndoto, unajikuta unaelewana nao kirahisi.

Ubunifu wa Michoro: Michoro ni ya kipekee na yenye ubunifu wa hali ya juu, inakupa picha halisi ya matukio.

Maadili na Mafunzo: Mara nyingi zinafundisha maadili na masomo muhimu ya maisha.

Mifano ya Anime Maarufu Zilizoshinda Tuzo

Kuna Anime nyingi zilizofanya vizuri na kutambulika kimataifa. Baadhi ya hizo ni pamoja na:

Spirited Away: Imeshinda tuzo ya Oscar kwa Filamu Bora ya Uhuishaji.

Your Name. (Kimi no Na wa.): Imepokea tuzo nyingi na kuvunja rekodi za mapato duniani.

Demon Slayer: Kimetsu no Yaiba: Imeshinda tuzo mbalimbali ikiwemo "Anime of the Year."

Attack on Titan: Maarufu sana kwa hadithi yake tata na yenye kusisimua.

Nimeona inafaa kufungua mada hii ili tupate nafasi ya kujadili na kushiriki uzoefu wetu kuhusu Anime na Manga. Karibuni sana tushiriki mawazo, tuulizane maswali, na kupendekeza Anime/Manga nzuri!

Je, kuna wengine hapa mnaopenda Anime
? Tuanze mjadala!
View attachment 3411124View attachment 3411125View attachment 3411126View attachment 3411127View attachment 3411128
Kuna anime (hentai) za kikubwa (pilau). Niliziangallia sana miaka kama 20 iliyopita. Bahati nzuri sasa nimezeeka na najaribu kumrudia Mungu.
 
Imeisha vibaya sema ila ile battle ya Kira na light ni noma sana.
Angalia na steins gate pia
Sijapenda kabisa walichomfanyia L, mshikaji aliteleza kidogo tu. Wanasema muandishi wa Death Note alitaka kumaliza Anime baada ya kufa L, ila baada ya kuona imekuwa well received wakaamua kuindeleza na kumkabidhi mikoba dogo Near. Na sitaki kuamini kwamba amemdhidi L akili.

Mwisho wa Light Yagami ni well deserved, wanasema usifunge mkataba na shetani, hasa kama ni Shinigami mtoa roho.

Ngoja niitafute hiyo Steins Gate, nasikia nayo ni kali.
 
Back
Top Bottom