Anime

Anime

Wazee wa anime kuna hii iitwayo BUNGO STRAY DOGS Ina season 5

BungoStrayDogsKYS3.jpg
 
SPOILER ALERT.

Leo tupige story kidogo kuhusu ONE PIECE.

Wengi tunakumbuka zile Movies za Pirates of Carribbean za mtaalam Jack Sparrow? Naam najua wengi tunakumbuka.

Sasa hizi movies zilinifanya nivutiwe sana na Ulimwengu wa Pirates na Kile kilichooneshwa kwenye zile Movies kilifanya niwe na kiu zaidi ya kutaka kujua hasa kuhusu ulimwengu huu wa ajabu.

Sasa ONE PIECE ilikuja kukata kiu kabisa ya Ulimwengu huu, karibia kila kitu kilikuwa on Point.

Kwanza matukio yake ni Very unpredictable, huwezi jua what comes next.

Leo tutaona vitu vichache kuhusu ONE PIECE.

ULIMWENGU WA ONE PIECE.

Aisee kile tulichokiona kwenye season one ya Netflix ya ONE PIECE ni kipande Kidogo saaaaana cha Ulimwengu wa One Piece na Kwa mwendo ule wa Netflix sijui watachukua miaka Mingapi kufikia sehemu ilipo sasa kwenye ANIME.

Kwanza katika Ulimwengu wa ONE PIECE Bahari imegawanyika katika sehemu kuu saba zinazoonekana.( Zingatia zinazoonekana sababu nyingine hazionekani kwenye ramani)

Kuna EAST BLUE (Hii ndio sehemu tuliyoiona wengi kwenye Season one). Matukio karibia yote ya Season 1 yalikuwa EAST BLUE.

Kuna WEST BLUE, NORTH BLUE na SOUTH BLUE.

Sasa ukitoka hapo kuna sehemu nyingine tatu ambazo ni RED LINE, CALM BELT na GRAND LINE.

images (1) (19).jpeg


Sasa ndoto kubwa ya Luffy ambapo baadae walikuja kupata jina maarufu na linaloogopeka la STRAW HAT PIRATES, ilikuwa ni kupata ile treasure ya ONE PIECE ambayo ilikuwa inapatikana Grand Line.

Sasa Kuingia GRAND LINE ilikuwa sio kazi ndogo maana ni asilimia chache mno wanaoweza kuingia kule achia ku survive kwenye GRAND LINE.

Maana ili uingie grand line kuna njia mbili tu.

1. Upitie REVERSE MOUNTAIN

Ambapo at the mountain bottom kuna strong currents ambapo a very small mistake itafanya Ship yako I crash kwenye RED LINE na kuwa totally wrecked hapo ndipo inakuwa mwisho wa Safari ya Kuingia GRAND LINE.

Au
2. Upitie CALM BELT sasa.

CALM BELT

Hili ni Eneo hatari sana la bahari ambalo kwanza halina upepo kabisa yaani ni Zero Wind na tunajua umuhimu wa Upepo kwenye Usafiri wa baharini, mbili ni makazi ya viumbe vya ajabu vikubwaaa saaaana ambavyo kwenye ONE PIECE vinaitwa SEA KINGS, Hivyo meli yoyote ikijikuta ipo kwenye Calm Belt either kwa Makusudi au bahati mbaya basi ndio Mwisho wake hapo. Hakuna mtu anarudi yupo hai.

Lage_der_Grandline.jpg


Hivyo kuingia GRAND LINE kupitia CALM BELT ni almost impossible.

Hivyo njia pekee inayobaki ni ya kwanza kupitia REVERSE MOUNTAIN.

Ambapo hapa Maji yanapanda mlima (Ndio yanapanda Mlima) halafu yakifika juu ya Mlima ndipo sasa yanashuka kwa spidi ya ajabu kuingia GRAND LINE.

images (1) (20).jpeg


Sasa huko GRAND LINE Kuna balaa zito.

Kuanzia
1. Navy waliopo huko ni hatari, kuna wajuba hawafai.

2. Pirates waliopo huko ni Kisanga.

Tunakumbuka Luffy Ali Battle na Leader wa Arlong Pirates ( Arlong) ambaye ndio alikuwa na Bounty kubwa Zaidi kuliko Pirates wote kule East Blue Yaani Bounty ya Berries 20,000,000 si Ndio.

Sasa hiyo ni chamtoto mnooooo, maana Kule kuna Wapuuzi Wana Bounty za 4 BILLION Berries. Sasa unaweza kuimagine How strong and notorious are those Pirates.

images (1) (21).jpeg



3. Visiwa vyenyewe vilivyopo huko ni balaa.

4. Hali ya hewa yenyewe ya GRAND LINE ni Fujo tupu. Hali ya Hewa inakuwa Harsh in matter of Seconds.

Hivyo Survival rate ya GRAND LINE Hasa ukiwa Pirate ni ZERO na ndio maana palikuwa Panaitwa PIRATES GRAVEYARD yaani hii ni The Most Dangerous Place in the World.


Wataalam naskia Kaiju No 8 Season 2 episode ya 1 ipo hewani. Ni Kweli?
 
Back
Top Bottom