Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Hao Citibank serikali haina akaunti huko lakini mbona wanajiendesha vizuri na wanapata faida...CRDB waende CitiBank wakafundishwe jinsi ya kujiendesha bila kutegemea pesa za serikali...
Citibank, especially kwa Tanzania ni Corporate Bank wakati CRDB ni Retail Bank na ndio maana huwezi kukuta Citibank wanaenda sehemu ambazo hazina corporate customers! Prediction ni kwamba, sooner or later hao Citibank wataingia ama Mtwara au Lindi au kote! Na wala hawataenda huko kwa ajili ya wafanyakazi au wafanyabiashara za maduka bali kwa ajili ya wawekezaji kwenye sekta ya mafuta na gas!!
 
Kama mzunguko wa hela mtaani umedorora na biashara nyingi zinakufa na uhakiki wa watumishi haufiki mwisho,hizi benki zitamkopesha nani na kama biashara zinayumba,wafanyabiashara hawa watalipaje mikopo hiyo?
Hayo ni maswali ambayo yanatakiwa yajibiwe sio na mtu mmoja, kuanzia gavana, shirikisho la mabenki, na wafanyabiashara kwa ujumla. Huwezi kupata jibu la haraka haraka lakini navyo ona mimi, hapa tz tuna mabenki mengi sana ambayo yanashindwa kubuni vivutio vya kuvutia wateja wao. Vitu kama punguzo la riba au hata ongezeko la riba ya akiba. Leo hii mtu huwezi ku take risk na ukajitosa benki kama riba ya mkopo ipo juu. Unajiuliza biashara ikigoma jee, sindio watanifilisi. Sasa wewe ukusema hivyo, na mwengine na mwingine, Matokeo yake mzunguko wa fedha unakuwa mdogo. Haya mambo ya riba yamekuepo tangu enzi za mkapa. Naona kipindi hichi cha JPM kama mabenki yasipo kuwa wabunifu uhai wao utakuwa ni wa utata.
 
wateja ambao citi bank anao crdb wala nmb hawezi kuwagusa..

jaribu kugoogle kwanza citi bank au wikipedia uijue vizuri balaa lake..

multinational companies karibu zote nchini zinaweka hela zao citi bank...

ni bank yenye mtaji zaidi ya mara 100 ya crdb au nmb na ipo dunia nzimaaaaa... hata baclays bank hagusi brand ya citi bank.

citi bank head office zipo usa wakati crdb head office zipo dsm..

hivi unafikiri makampuni ya gesi.. na kina vodacom, airtel, maersk, na multinational zinaweka hela zao nmb au crdb??

mzungu anaweka hela kwa mzungu mwenzake hataki ujanja ujanja


Hao Citibank serikali haina akaunti huko lakini mbona wanajiendesha vizuri na wanapata faida...CRDB waende CitiBank wakafundishwe jinsi ya kujiendesha bila kutegemea pesa za serikali...
 
Hapa kazi tu! Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu. Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession! Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"

Eti pesa zote kuwekwa benki kuu kumesababisha interest rate kupanda sana na wakopaji kushindwa kukopa.Kwani pesa zote za serikali zilipokuwa zinakaa mabenki ya biashara ni lini interest zilikuwa ndogo.Kila siku watu walikuwa wakipiga kelele mabenki shusheni riba na maskini wakope wakawa mabenki wameweka pamba masikioni wakati pesa wanayozungusha ni ya serikali! Sasa hivi ndio wanabweka.

Afadhali tu hizo pesa zimerudi tu BOT sababu kuwa kwenye mabenki ya biashara zilikuwa hazisaidii mnyonge na mtu wa chini kwa kumkopesha.Heri tu zikae tu zitulie tu.
 
Hapa kazi tu! Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu. Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession! Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
Mkuu wewe ni mmoja wa watanzania wanaojielewa sana na wanaojua kinachoendelea, nakupongeza kwa kutokua punguani kati ya mapunguani wanaoshabikia ovyo ovyo msemo wa kazi.tu bila kutafakari kwa kina mambo haya especially ya uchumi.
Napenda kuendelea kuongezea ulipoishia katika ufafanuzi wako kitaalamu lakini naona ntawapa watu stroke humu.
 
Vichaa wa lumumba wanasema ananyoosha mambo.wanasahau kuwa ni hao hao bado wako madarakani.
 
Below are some microeconomic indicators you may likely to see when economy is about to collapse:-

1. Local businesses shutting down in large numbers

2. Prominent local businessmen/ proprietors and leaders leaving the area/country or engaging in other business-related activities;
3.Grocery stores and big-box stores bereft of necessities and inventory
4. Increased layoffs and unemployment notices across the country.

5. Your local commercil bank beginning to institute forms of rationing (loans) or checks and controls; all aimed to limit you to borrow more money;
5. An increasing amount of social unrest such as Panyaroads;
6. Cessation or severe curtailment of regular shipments of goods (food, gasoline, medicine)
7. Supermarkets and other retail stores sell more necessity goods than luxury ones;
8. Increased number of ads selling their short term assets (household items , cars, plots etc);
.....
hizi zote zinaonekana Tanzania....tena kwa kila mtu hata kipofu
 
Rais afanye ziara ya kushtukiza huko kwenye UCHUMI kuweza kutumbua
anatafuta mlango hauoni......mambo yamemchanganya kiasi kwamba zile swaga za kutuimbia kilomita za barabara zimekwama.

aimbe takwimu za mbongo a.k.a makuta,a.k.a shilingi
 
Acha kuwa na fikra potofu Mkuu. Uchumi wa nchi unapokuwa Serikali haifaidiki kwa ongezeko la mapato kupitia kodi? Imagine kama hizi pesa zingekuwa zimekopeshwa kwa watu binafsi na makampuni ambayo yangeajiri Wafanyakazi wanaolipwa mishahara na wanalipa kodi na statutory deductions nyingine mbali mbali.

Serikali inahitaji more than 5 Trilioni ili kujiendesha hivyo itake isitake ni lazima ikope kwa sababu mapato yake ni madogo ukilinganisha na matumizi ya kwenye bajeti.
Kaka napenda sana kusoma comments zako lakini leo unachemsha sana
 
Kwa ujumla katika Q3 pekee imepata faida ya 2.8 Billion.Kinachooneka (1.9)billion kama

Kwa ujumla katika Q3 pekee imepata faida ya 2.8 Billion.Kinachooneka (1.9)billion kama hasara ni ya Benki pekee bila kujumlisha subsidiaries companies zake. Hivyo Benki kwa ujumla katika Q3 imepata 2.8+ Billion.
Faida imekuwa ndogo kwa sababu ya provision ya bad loans of 38 Billion compared to 13 Billion during the same period 2015.
Lakini kwa ujumla katika kipindi cha miezi tisa Benki imepata faida ya 69 Billion.
Of course si ishara nzuri nzuri kwenye uchumi wetu kama madeni yanashindwa kulipika.
kipindi hichohicho mwaka jana walikuwa na faida zaidi ya bilioni 100, kwa hiyo ukisema 69,linganisha na mwaka jana

bado wana hasara kubwa sana tu
 
Kwa hiyo huaminin kama kweli wamepata hasara? Kumbuka CRDB walikuwa na fedha nyingi za serikali ambazo wamenyang'anywa na kuhamishiwa BOT, so mtaji wao pia umepungua....
Kinachosikitisha ni bank ya Twiga kuzama na mtaji wa karibu bilioni mia na moja, fedha za depositors...
Kwa hiyo depositer watazipataje
Nmekuelewa mkuu

BOT ineshidwa kufanya kazi yake ya kuwa mkopeshaji wa mabenkiya kibiashara na hivyo kufanya mikopo iwe ghali zaidi kutokana na gharama za amana ambazo benki hizi zinaingia kupata amana.
Pia kwa serikali kuhamisha pesa zote kwenye mabenki kumeatbiri ukopeshaji ili kuanzisha shughuli mpya za kiuchumi au kuendeleza zile za zamani. Importers wanategemea mikopo katika biashara zao huwezi kuangiza mzigo ukauuza same day i uweze kuagiza mwingine matokeo yake yanaenda kugusa sekta nyingine kama Bandari.
Kupata hasara katika mabenki kama nilivyosema hapo mwanzo biashara nyingi zimesimama uwezo wa kulipa mikopo ya wafanyabiashara hasa wadogo umekuwa mgumu hivyo mikopo imekuwa mibaya sheria za uendeshaji wa mabenki chini ya usimamizi wa BOT inazitaka benki kufuta mikopo mibaya kwenye vitabu vyake kupitia faida ili kuendelea kuwadai wakopaji wakati tayari wameifuta na pale wanalipa basi inaongezwa kwenye faida ya mwaka mkopaji huyu anapolipa.
Hii unaweza iona katika vitabu vya CRDB wamefuta mikopo mibaya ya almost 38billion ambayo ni wazi imepunguza faida kwa 38billion lakini hii inavifanya vitabu vyake kuwa safi na kutengeneza mkakati mpya. Jambo kama hili lilitikea miaka miwili iliyopita kwa NBC ambao walipata hasara ya kama 2billion kwa mwaka huo tofauti na Crdb wao bado kwa majumuisho ya kipindi cha robo tatu bado wanafaida ya zaidi ya 100 billion na uwezekano wa kupata faida zaidi kwa mwaka 2016 ni mkubwa kwasababu tayri sehemu kubwa ya mikopo yake mibaya ambayo inakula faida amekwisha ifuta kwenye vitabu vyake na kuwa deni la kawaida kwa wakopaji.

Ushauri:
1. Serikali kuzipa nafasi mabenki kutumia pesa wanazokusanya kutoka a maduhuri ya serikali kubaki huko ili waweze kukopesha au

2. BOT kufanya kazi ya kuyakopesha manenki ili nayo yaweze kukopesha kwa riba nafuu kwa wananchi na kukuza uchumi.

Tahadhari;
Kwa mabenki kushindwa kuwa na amana za kutosha kwa serikali kukimbizia makusanyo yote (ambayo commericial benki ndo wakusanyaji) itaua uwezo wa mabenki na hivyo ukusanyaji wa mapato ya serikali ukawa mgumu kwa vile BOT hawana matawi nchi nzima.

Pia serikali itambue mabe ki ni mshirika wake katika kujenga uchumi na hatua zizote za kudhoofiisha sekta hii ni kuua uchumi.

Mwisho kodi inaongezeka kwa kuwa na uwekezaji mpya hivyo serikali inatakiwa kuhamasisha uwekezaji binafsi i kuweza kuvuna kodi la sivyo tukimaliza kukusanya hizi Tax arrears tunatabaki hatuna cha kukusanya (hili limeanza kujitokeza utaona malengo ya umusanyaji wa mwezi October yatavyofikiwa kwa mbinde)
 
Vitu vingine haviitaji ubabe bali akili na uwezo. Ukiaribu kimoja tu kinapelekea kwa kuaribika kwa vingine. Tusubili kuingia kwenye Recession then Depression kabisa miezi michache ijayo
 
Taasisi bhana wakiwa wana submit report zitakazotumika na m amlaka za kodi wanaonyesha wanapata hasara au faida kiduchu, lakini hao hao wakiwa wanataka mikopo wanaonyesha wanapata faida kubwa, ukitaka mwanao awe jizi la kutupwa mruhusu abobee kwenye hii kada
Hakuna cha ajabu. Benki ni wawezeshaji (facilitators) wa shughuli za kiuchumi/kibiashara. Shughuli za kiuchumi/kibiashara zikidorora lazima na benki zipate mdororo.
 
Serikali kutunza fedha zake BOT ni sahihi kabisa maana one and traditional function of BOT is a " banker of the Government". hapa kuna tatizo kwnye hizi commercial banks zetu.
Natamani kukuelekeza kitu hapa kiuchumi zaidi ila nimebanwa na majukumu, ila naimani ukipitia comments nyingi za wajuzi wa mambo ya uchumi hapa utaelewa. Hiyo ni kazi moja wapo ya BOT ila kumbuka pia ni banker of commercial banks pia. Na kazi yake kubwa ni kumonita monetary activities zote ndani ya nchi kwa kutunga sera za kifedha na kuzisimamia.
 
Serikali kutunza fedha zake BOT ni sahihi kabisa maana one and traditional function of BOT is a " banker of the Government". hapa kuna tatizo kwny hzi commercial banks zetu.
Hii "traditional" si ndio "mazoea" au kidhungu hiki hakina ithibati!?
Iko haja ya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
 
Basi nimekufananisha maana ID hii tumewahi jadili nayo mambo haya kwa kina sana!!

Anyway uchumi wetu unayumba kutokana na govt kupunguza sana matumizi coz chumi changa kama zetu zinahitaji sana kuwa boosted na govt expenditure kama serikali haitumii basi mzunguko unadorora na kuziathiri pia benki...

Nimemsikia Magufuli akijisifu kuwapa kazi nyingi TBA za serikali hii pia inaua uchumi coz TBA ni serikali so serikali inazungusha pesa mfukoni kwake badala ya kuwapa kazi makampuni watakaolipa kodi na kuajiri vijana wengi zaidi!

Hii ya CRDB kutoka kupata faida ya 30 billion mpaka hasara ya 2 billion ni msiba!! Hii si figisu ni kitu dhahiri kwani benki zote transactions zake pamoja na mitiririko yote ya fedha zao zipo monitored na BoT ni vigumu kudanganya!!

Jambo lingine lilichangia kuanguka huku ni hofu za wateja dhidi ya serikali!! Serikali ya JPM imeonesha dhahiri kutotabirika!! Hakuna mwekezaji au tajiri yeyote anayeweza wekeza pesa zake kusikotabirika!! So wengi waliondoa fedha zao benki ili kuondokana na hofu dhidi ya serikali isiyotabirika so benki zinakosa amana na mitaji....

Kingine ni madeni yasiyolipika kama vile mikopo ya watumishi hewa.... madeni ya biashara zilizoanguka kama hoteli n.k n.k

Katika ishu JPM anahitaji kuwa serious ni uchumi!! Hayo mengine anayohangaika nayo yatampotezea muda tu huku nchi ikielekea ilipo Zimbabwe... ni suala la muda tu utatuambia!!

CC Kobello Pohamba Richard
Hili la kutotabirika limenikumba hata mm mwenyewe nilikuwa nataka kufanya biashara, nikaomba kushirikiana na mwenzangu, nikiwa numeshafuata taratibu zote, lakini mwenzangu kajitoa pamoja na kufuata taratibu simply bcoz serikali haiaminiki tusubiri kwanza, unaweza kuagiza mzigo ukifika Bongo sheria zimebadilika!
 
Tunajenga Tanzania moja lakini serikali inagombania fito,eti inasema benki zilikuwa zinatumia fedha za serikali kukopesha wananchi na kupata faida.

Ebbo!!, sasa na bakhresa,mengi,mohamed dewji na matajiri wengine wanaoweka fedha benki nao wazitoe kwa hoja kwamba benki huwa wanatumia hela zao kukopesha?

je wakishakopesha, serikali ikienda kuangalia balansi,au ikienda kuzichukua huwa inaambiwa "fedha zenu hazipo,tumezikopesha"....si huwa wanazikuta!!tena zikiwa na riba!!

je wanaokopa ni akina nani? si hawa akina hawa,asha,mwajuma,abdallah,masanja.....watanzania wenzetu ili wakaanzishe biashara zao ndogo ndogo wajikomboe na umasikini!,

sasa serikali imeona hawa watanzania.wanakopa fedha benki wanazifaidi(na inaamini eti zinazokopwa ni za serikali tu),ikaamua izitoe,sasa inamkomoa nani? inazikomoa benki au wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao sasa hawapati mikopo na wanalia hali ngumu!

halafu unapokusanya pesa na kwenda "kuzificha" benki kuu unazuia mzunguko,benki kuu itayahifadhi malundo kwa malundo ya pesa tu,haiwezi kwenda tandale kumkopesha mama ntilie,haiwezi kwenda mtaa wa kongo kumkopesha mjasiliamali,

kwa maana nyingine,"unakomba"hela zoote za nchi,"unazificha,halafu unataka watu wafanyeje? manake huku ni kuficha hela.

kingine,hiyo CRDB ni benki ya nani?si ni benki ya mtanzania? kama kwa.miaka zaidi ya 20wameonyesha uaminifu kwa kutopoteza hata senti ya umma iliyohifadhiwa pale,kwa nini wewe ukae mwezi tu serikalini eti uwazidi akili mwinyi,mkapa na kikwete!!

tunagombania fito,na kwa kuwa tunagombania fito,hakika nyumba haitaisha,ukishika fito unanyanganywa,na mimk ukishika fito nakunyanganya......tutagombana weee mwishowe akija aliyetupa kazi (mtanzania)kutaka akabidhiwe nyumba,tutakoma 2020

Umeandika ngonjera ndefu ila haina maana. Inaonyesha dhahiri una uelewa Mdogo sana wa mambo ya fedha na uchumi. Mawazo yako yapo ki layman zaidi na siwezi kukulaumu.

Unaposema CRDB inakopesha pesa ya serikali kwa watu na bado serikali ikiomba pesa yake inapewa unajua unachozungumza kweli? Unajua ni mara ngapi CRDB wameshindwa kurudisha pesa waliozopewa na serikali? Au unadhani serikali na CRDB zinafanya transactions za 100mil?

Haya mambo ya uchumi watu kama nyie kaeni pembeni msikilize msilete ujuaji kwenye kila kitu wakati hamjui kitu.
 
kipindi hichohicho mwaka jana walikuwa na faida zaidi ya bilioni 100, kwa hiyo ukisema 69,linganisha na mwaka jana

bado wana hasara kubwa sana tu
Rafiki yangu iparamasa,kwenye Financials zote za 2015 na 2016,kinachoonekana kuleta tofauti kubwa hapo ni "provision for bad and doubtful debt".
kipindi hichohicho mwaka jana walikuwa na faida zaidi ya bilioni 100, kwa hiyo ukisema 69,linganisha na mwaka jana

bado wana hasara kubwa sana tu
Rafiki yangu iparamasa,kwenye Financials zote za 2015 na 2016,kinachoonekana kuleta tofauti kubwa hapo ni "provision for bad and doubtful debt". Kwenye 2015 during the same period provision ilikuwa 35 Bil wakati 2016 during the same period provision iko 78 Billion (angalia).Tofauti ya 43 Billion.Maana yake,ukiondoa suala ya Provision for bad loans the performance is less or equal the same.
Kwa hiyo,kitu kilicho wazi ni kuwa economic activities za watu haziendi vizuri kama ilivyotarajiwa!
 
Back
Top Bottom