Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Kwa haya yanayoendelea!
Mwisho wa siku kila mtu ataelewa tu.
 
Karibu 5 trilioni imeondolewa kwenye mzunguko wa pesa nchini imelala pale BoT idle tu haifanyi kazi yoyote ile! wakati hii pesa ingekuwa kwenye mabenki ya biashara ingekuwa inazunguka kwa namna mbali mbali ikiwemo mikopo n.k. Hivyo benki za biashara zinafaidika na nchi pia inafaidika kwani watu wanakopa pesa wanafanya mambo mbali mbali ikiwemo kuinvest kwenye biashara mbali mbali, kufanya ujenzi etc. Wewe Rais hujik lolote kuhusu uchumi una washauru wa mambo ya uchumi lakini unakurupuka na kuondoa 5 trilioni shillings kwenye mzunguko wa pesa nchini.
Kama hakuwi nenda katuambie wapi serikali inafanya biashara na pesa yake ywnyewe? Umbulula mwingine mnajiaibisha. Kenya hapo tu wanafanya kama sisi mbona hakuna bank inaaumbuka.
 
CRDB walikuwa wanafanya biashara haramu na fedha za serikali....hii benki imetumika sana na mafisadi ...mafisadi wamebanwa ndio maana imefilisika
hata wakati manabii wanawaonya kuhusu bandari,hamkusikia,na kawaida kenge huwa "haelewi somo" mpaka aone damu imeanza kutoka masikioni.

hili na mabenki mnaonywa pia...ole wake asiyeisikia sauti hii
 
Namuunga Magufuli kwenye baadhi ya mambo, ila anafeli anapojaribu kucontrol pesa kwenye Mzunguko, cause kihualisia Bank binafsi na wananchi wanapesa nyingi kuliko fedha zilizopo Benki kuu
Magufuli anashauriwa na maprofesa. Z
Ila pamoja na dr yake hajajua tu kuwa u profesa siio kujua kila kitu. Hakuna watu wabaya kama maprof.
Kama maprof wangekuwa smart Lipumba tusimgemuona hivi alivyo leo hii..
 
Hapa kazi tu! Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu. Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession! Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
Taifa linarudi enzi za ujima lakini kuna watu wanashangilia Hapa Kazi tu!!!
 
Huelewi Mkuu, Serikali katika pesa hizo ilizoziondoa mabenki ya biashara ilikuwa inafaidika, sasa hivi haifadiki kwa hizo pesa nyingi kiasi hicho kukaa idle pale BoT. Mabenki ya biashara nayo yalikuwa yanafaidika, Watanzania nao walikuwa na wanafaidika na mwisho kuongeza mapato kwa Serikali kupitia TRA.
Serikali ilikiwa inafaidikaje na pesa zake huko kwenye mabenki? We umeambiwa serikali ilikuwa inakopa pesa zake kwa riba kubwa huko kwenye mabenki...sasa hivi pesa za serikali ziko BOT ikizitaka hakuna cha kukopa kwa riba
 
Tanzania bana.

Kila mtu ni mjuzi wa uchumi mpaka wengine wanapinga hata kinachoongewa na wataalam wa uchumi ambao wanafahamika kitaaluma.

Wale walisema half knowledge is worse than ignorance hawakukosea.
 
Basi nimekufananisha maana ID hii tumewahi jadili nayo mambo haya kwa kina sana!!

Anyway uchumi wetu unayumba kutokana na govt kupunguza sana matumizi coz chumi changa kama zetu zinahitaji sana kuwa boosted na govt expenditure kama serikali haitumii basi mzunguko unadorora na kuziathiri pia benki...

Nimemsikia Magufuli akijisifu kuwapa kazi nyingi TBA za serikali hii pia inaua uchumi coz TBA ni serikali so serikali inazungusha pesa mfukoni kwake badala ya kuwapa kazi makampuni watakaolipa kodi na kuajiri vijana wengi zaidi!

Hii ya CRDB kutoka kupata faida ya 30 billion mpaka hasara ya 2 billion ni msiba!! Hii si figisu ni kitu dhahiri kwani benki zote transactions zake pamoja na mitiririko yote ya fedha zao zipo monitored na BoT ni vigumu kudanganya!!

Jambo lingine lilichangia kuanguka huku ni hofu za wateja dhidi ya serikali!! Serikali ya JPM imeonesha dhahiri kutotabirika!! Hakuna mwekezaji au tajiri yeyote anayeweza wekeza pesa zake kusikotabirika!! So wengi waliondoa fedha zao benki ili kuondokana na hofu dhidi ya serikali isiyotabirika so benki zinakosa amana na mitaji....

Kingine ni madeni yasiyolipika kama vile mikopo ya watumishi hewa.... madeni ya biashara zilizoanguka kama hoteli n.k n.k

Katika ishu JPM anahitaji kuwa serious ni uchumi!! Hayo mengine anayohangaika nayo yatampotezea muda tu huku nchi ikielekea ilipo Zimbabwe... ni suala la muda tu utatuambia!!

CC Kobello Pohamba Richard
Mkuu, hawa jamaa wanaotupaka mafuta kwa mgongo wa chupa na kutudanganya kuwa uchumi wetu unapaa kwa kasi, je kipindi tutakapofikia kama ilipofikia uchumi wa Zimbabwe watatuambia nini? Watakua na majibu yoyote ya justify zile promo zao?
Hali ni mbaya kila sekta! Ila mkulu ndio hataki kabisa kushaurika.
 
hata wakati manabii wanawaonya kuhusu bandari,hamkusikia,na kawaida kenge huwa "haelewi somo" mpaka aone damu imeanza kutoka masikioni.

hili na mabenki mnaonywa pia...ole wake asiyeisikia sauti hii
Wanaolia lia ni CRDB tu kwa sababu ya mafisadi na wizi wao umebanwa...kuna benki nyingi tu zinapata faida nzuri
 
Serikali ilikiwa inafaidikaje na pesa zake huko kwenye mabenki? We umeambiwa serikali ilikuwa inakopa pesa zake kwa riba kubwa huko kwenye mabenki...sasa hivi pesa za serikali ziko BOT ikizitaka hakuna cha kukopa kwa riba
mwongo mkubwa......serikali inapokopa maana yake ina upungufu wa fedha...kwa hiyo hii serikali ni ya mazuzu ina hela halafu inakopa?

na mara nyingi serikali kuu ndiyo haina pesa,

mashirika kama ewura,sumatra,mashirika ya pensheni ndiyo yenye pesa nyingi ambazo kimsingi ni za kwao japo mashirika hayo yalikuwa yanamilikiwa na serikali.

serikali kuu haina haki yoyote juu ya pesa hizo za mashirika hayo.

kimsingi inayokopa kwenye mabenki ni serikali kuu ili ikalipe mishahara maafisa tarafa wake
 
Acha uongo wewe hayo mashirika sumatra, Tanapa Ewura ni mashirika ya serikali na pesa zao ni pesa za serikali na benki yao ni BOT tu...Walikuwa wanaweka pesa zao CRDB makusudi kwa ajili ya kupigia madili yao ya kifisadi na maafisa wa benki
 
Acha kuwa na fikra potofu Mkuu. Uchumi wa nchi unapokuwa Serikali haifaidiki kwa ongezeko la mapato kupitia kodi? Imagine kama hizi pesa zingekuwa zimekopeshwa kwa watu binafsi na makampuni ambayo yangeajiri Wafanyakazi wanaolipwa mishahara na wanalipa kodi na statutory deductions nyingine mbali mbali.

Serikali inahitaji more than 5 Trilioni ili kujiendesha hivyo itake isitake ni lazima ikope kwa sababu mapato yake ni madogo ukilinganisha na matumizi ya kwenye bajeti.

Serikali ilikiwa inafaidikaje na pesa zake huko kwenye mabenki? We umeambiwa serikali ilikuwa inakopa pesa zake kwa riba kubwa huko kwenye mabenki...sasa hivi pesa za serikali ziko BOT ikizitaka hakuna cha kukopa kwa riba
 
Acha kuwa na fikra potofu Mkuu. Uchumi wa nchi unapokuwa Serikali haifaidiki kwa ongezeko la mapato kupitia kodi? Imagine kama hizi pesa zingekuwa zimekopeshwa kwa watu binafsi na makampuni ambayo yangeajiri Wafanyakazi wanaolipwa mishahara na wanalipa kodi na statutory deductions nyingine mbali mbali.

Serikali inahitaji more than 5 Trilioni ili kujiendesha hivyo itake isitake ni lazima ikope kwa sababu mapato yake ni madogo ukilinganisha na matumizi ya kwenye bajeti.
Hizo trilioni tano sasa ziko BOT serikali ikizitaka itaenda kuzichukua bila kutoa riba....Unataka zipelekwe CRDB halafu wakazikope kwa riba kubwa? Kuna mabenki mengi serikali haikuwa inaweka pesa zake huko yako vizuri yanaendelea kufanya biashara halali na wananchi.....CRDB kuna shareholders wameweka fedha zao huko nashangaa wanalilia pesa za serikali.....hii benki ilikuwa inaendeshwa kijanja janja wacha ife
 
Acha uongo wewe hayo mashirika sumatra, Tanapa Ewura ni mashirika ya serikali na pesa zao ni pesa za serikali na benki yao ni BOT tu...Walikuwa wanaweka pesa zao CRDB makusudi kwa ajili ya kupigia madili yao ya kifisadi na maafisa wa benki
kwa busara za lumumba,nssf,pspf, lapf,bora hela zao zikaozee benki kuu mpaka mtumishi afikishe miaka 60 achukue pensheni?!!

zingekuwa na mchango kiasi gani kwenye uchumi kwa miaka japo 30!
 
Good People,

Hamna namna hizo financial statements ukazi-screenshot into two docs kisha ukazi-attach independently?! Hivyo ilivyo, sie tunaopenda kutumia reference tunashindwa kwavile haionekani vizuri hasa juu! So, if posible, ningeshauri doc ya kwanza iishie kwenye SELECTED FINANCIAL CONDITION INDICATORS na doc ya pili ianzie kwenye STATEMENT OF COMPREHENSIV INCOME FOR THE PERIOD ENDED 30TH SEPTEMBER, 2016. Nadhani ukiweka kwa hiyo staili, zinaweza kusomeka vizuri... nimecheki kwenye tovuti yao lakini bado hawajaweka!
 
Hizo trilioni tano sasa ziko BOT serikali ikizitaka itaenda kuzichukua bila kutoa riba....Unataka zipelekwe CRDB halafu wakazikope kwa riba kubwa? Kuna mabenki mengi serikali haikuwa inaweka pesa zake huko yako vizuri yanaendelea kufanya biashara halali na wananchi.....CRDB kuna shareholders wameweka fedha zao huko nashangaa wanalilia pesa za serikali.....hii benki ilikuwa inaendeshwa kijanja janja wacha ife
inazichukua tu eti eehh!!

kuna pesa nyingi za mashirika ya pensheni,ikitaka inazichukua tu eti? halafu wastaafu watalipwa na wajomba zako
kuna pesa za tanesco,ikitaka inazichukua tu eti eeh halafu tutatumia gesi ya tumboni kwako eehh
 
Back
Top Bottom