Anguko la January Makamba

Anguko la January Makamba

Wana-ccm wote kabla ya 2014 wanaamini rushwa will secure their survival toward uchaguzu mkuu 2015
 
Acts 13:36 – “For when David had served God's purpose in his own generation, he fell asleep; he was buried with his fathers and his body decayed

Ni ukweli usiopingika kwamba kila kizazi kinahitaji kiongozi wake. Hiyo ni kwa sababu kila kizazi kina matatizo yake, maono yake, na matakwa yake. Ni ukweli usiopingika kwamba kizazi cha Tanzania leo hii kina kiu ya kiongozi wake.

Kwa muda ilionekana kama vile kuna vijana wawili – January Makamba and Zitto Kabwe, ambao walikuwa tayari kubeba jukumu la kusimama kama nyota ya uongozi wa kizazi kipya. Kili mmoja wetu anajua kilichojiri Bungeni hivi karibuni, hasa uamuzi wa January Makamba kupingana na hatua aliyoingoza Zitto Kabwe ya kudai uwajibikaji serikalini.

Ni dhahiri, ingawa wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti, kwamba January amejiweka katika wakati mgumu kisiasa, hasa mbele ya vijana waliomtegemea.

Kwa muda January Makamba aliweza kung’ara katika anga za siasa Tanzania kwa sababu ya uwezo wa kupambanua mambo. Lakini kilichotokea Bungeni kimedhihirisha kitu kimoja – uwezo wa January kupambanua mambo na kutoa kauli “zilizoenda shule” peke yake hakumfanyi mtu kuwa kiongozi na shujaa wa kizazi chake. Kuna wakati na mazingira yanamtaka kiongozi kudhihirisha mawazo na moyo wake ulipo.

Pale Bungeni, wakati huo ulitokea na bahati mbaya sana January akaugopa wakati huo.

Pale mjengoni, January Makamba alidhihirisha kwamba mawazo yake na moyo wake yako mbali kama Mashariki iliyo mbali na Magharibi. Na ndio maana dhana ya “unafiki” inamzonga January. Katika utetezi wake, January Makamba aliandika hiki hapa chini:

"I can disagree with Zittokabwe on methods to reach the same objectives, and we are still brothers"

Mpaka leo sijasikia chochote toka kwa January kuhusu njia mbadala (tofauti na njia aliyopendekeza Zitto Kabwe) ya kuleta uwajibikaji serikalini. Kwa mantiki hiyo, hiyo kauli yake hapo juu ilikuwa ni jitihada tu ya kuzima zengwe na jinamizi la kisiasa linalomkabili.

What a waste.

Ajipange, kaponzwa na Uccm wake........ktk hili ametanguliza zaidi maslahi ya chama kuliko waTz, wapiga kura wake. Si kitu kizuri alichofanya.
 
Nope but his party is, if he was in opposition he would say alot believe me!!

Je, ana tofauti gani na wabunge wenzake wa CCM ambao katika jambo kama hili na nyakati kama hizi, wana achana na siasa za vyama na kuweka maslahi ya taifa mbele? Unasema kwamba 'if he was in opposition he would say a lot and that i should believe you'. Naomba nikueleze tu kwamba maana ya opposition ni hii: "The action of opposing something that you disapprove or disagree with"; Je kwa mtazamo wako, January agrees and approves of what Zitto and other 70 or so Wabunge from various political parties, disapprove and disagree with? January ametuangusha vijana ambao tulikuwa tunamwamini sana. Sisi vijana mitaani ambao tumekuwa tunamtetea tunajificha wapi sasa. Angalau basi ange abstain kama wengine wengi walivyofanya kwani he had nothing to loose. But him being actively involved means anashindwa kutofautisha kati ya activity and productivity katika siasa za ushindani.
 
Mazingira kitu gani? Simtetei mtu wala simpingi mtu hapa. Hayo hayo mazingira?ya Makamba angewekwa mtu hapa angeanza kujinyea the same. Zitto yuko huru kwa kuwa yupo upande wa kukosoa. Hivi cdm ndio ingekuwa madarakan halafu ikawa inaborongai mnadhani haya makeke ya Zitto mngeyasikia? Mnadhani Makamba angechukua uamuzi sawa na Zitto? Sitaki kuamini kuwa JM hana uzalendo. Halafu kwa nini JM peke yake? Lazima mjiulize maswali kwanza kabla ya kuanza kuhukumu.

Bado JM ni kiongozi mzuri pale atakapopata mfumo mzuri. Anaweza kutofautiana na Zitto kwenye njia ya kufikia suluhu lakini wakawa na nia moja ya kufikia suluhu. Hii inadhihirisha kuwa hakuna njia moja ya kufikia suluhu. Ni jambo rahisi tu kuelewa kuwa si rahisi kiivyo kuanza kukosoa kwa uwazi kama Zitto mfumo uliokulea tangu mtoto hadi kuwa kiongozi ndani ya huo mfumo. Na badala ya kumlaumu mtu mmoja tena kupitia keyboard, tungeinngia mitaani kudhihirisha hili lakini hiyo courage hatuna! So let them disagree on methods but still have a common goal!

Alphaxard Kangi Lugola ni mbunge wa Mwibara - ccm
Deo Haule Filikunjombe ni mbunge wa Ludewa - ccm
Nimrodi Elirehema Mkono ni mbunge wa Musoma Vijijini - ccm

Kama wote hawa ni wabunge wa ccm na walisaini petition, Je unataka tukueleweje katika utetezi huu unaoleta hapa dhidi ya kijana mnafiki January Makamba? unapozungumzia upande unamaanisha nini? kanda ya ziwa vs Nyanda za juu kusini vs Kaskazini??

January Makamba hawezi kuwa kiongozi mzuri hadi atakapoacha unafiki wake!! kiongozi mzuri anaonekana hata kama yuko upande gani. Katika hili huwezi katu kulaumu mfumo, hapa january anabeba msalaba wake mwenyewe kwa unafiki wake.
 
hivi kuna ulazima gani wa watoto nao kuwa viongozi kama baba zao..hapo ndipo ninapopata kichefuchefu..kwani hakuna wengine wa kuongoza..tumejaa tele lakini kubaniana na kupeana nafasi kwa vilaza ndio kunaendelea..

Mkuu,hujui ukizaliwa na mkulima ni lazima na wewe utalima?
 
..mimi nadhani alichofanya January ni utoto tu ktk mambo serious.

..alikuwa pale kujaribu kumharibia tu Zitto Kabwe.

..kama angekuwa serious angependekeza njia mbadala ya kuhakikisha mawaziri mafisadi wanawajibishwa.

..kitendo cha kumpinga Zitto na kueneza uvumi kwamba hoja yake[Zitto] ni "publicity stunt" kimeniacha na maswali mengi sana kuhusu January.
 
Shida kubwa ya vyeo vya kupewa kindugu hawezi kuwa independent...ni mnafiki sana na hajui kama meli aliyopanda inazama
 
Nilichogundua ni kwamba huyu jamaa si mpiganaji wa kweli,ni zaid ya mnafiki,na zaidi ya unafiki ni mtu mwenye uchu wa madaraka. Inaonekana waz kwamba anajipendekeza ili awe ktk baraza la mawaziri lijalo kama lililopo. Sina iman nae tena
 
Na badala ya kumlaumu mtu mmoja tena kupitia keyboard, tungeinngia mitaani kudhihirisha hili lakini hiyo courage hatuna! So let them disagree on methods but still have a common goal!

Still that haiondoi dhana kuwa katika suala zima la mawaziri kujiuzulu alichemka.
Method aliyochagua failed miserably.
Claiming issue ya Zitto ilikuwa a publicity stunt alichemka sana.
Because now it is completely the opposite. Yeye ndiye anayeonekana kuchemka.
Alichokuwa anataka kufanya au kutegemea kutoka kwenye Caucus yao was publicity stunt.
Alisema tusubirie kwenye vyombo vya habari tutaona results lakini mpaka leo hola.
Bado ni mdogo sana kwenye uwanja wa siasa. Hajakomaa kisiasa bado.
He still has got a long way to go.
I hope atakuwa amejifunza kitu kwenye sakata la mawaziri kudaiwa kudaiwa kujiuzulu though the damage has already been done.
 
Acts 13:36 – “For when David had served God's purpose in his own generation, he fell asleep; he was buried with his fathers and his body decayed

Ni ukweli usiopingika kwamba kila kizazi kinahitaji kiongozi wake. Hiyo ni kwa sababu kila kizazi kina matatizo yake, maono yake, na matakwa yake. Ni ukweli usiopingika kwamba kizazi cha Tanzania leo hii kina kiu ya kiongozi wake.

Kwa muda ilionekana kama vile kuna vijana wawili – January Makamba and Zitto Kabwe, ambao walikuwa tayari kubeba jukumu la kusimama kama nyota ya uongozi wa kizazi kipya. Kili mmoja wetu anajua kilichojiri Bungeni hivi karibuni, hasa uamuzi wa January Makamba kupingana na hatua aliyoingoza Zitto Kabwe ya kudai uwajibikaji serikalini.

Ni dhahiri, ingawa wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti, kwamba January amejiweka katika wakati mgumu kisiasa, hasa mbele ya vijana waliomtegemea.

Kwa muda January Makamba aliweza kung’ara katika anga za siasa Tanzania kwa sababu ya uwezo wa kupambanua mambo. Lakini kilichotokea Bungeni kimedhihirisha kitu kimoja – uwezo wa January kupambanua mambo na kutoa kauli “zilizoenda shule” peke yake hakumfanyi mtu kuwa kiongozi na shujaa wa kizazi chake. Kuna wakati na mazingira yanamtaka kiongozi kudhihirisha mawazo na moyo wake ulipo.

Pale Bungeni, wakati huo ulitokea na bahati mbaya sana January akaugopa wakati huo.

Pale mjengoni, January Makamba alidhihirisha kwamba mawazo yake na moyo wake yako mbali kama Mashariki iliyo mbali na Magharibi. Na ndio maana dhana ya “unafiki” inamzonga January. Katika utetezi wake, January Makamba aliandika hiki hapa chini:

"I can disagree with Zittokabwe on methods to reach the same objectives, and we are still brothers"

Mpaka leo sijasikia chochote toka kwa January kuhusu njia mbadala (tofauti na njia aliyopendekeza Zitto Kabwe) ya kuleta uwajibikaji serikalini. Kwa mantiki hiyo, hiyo kauli yake hapo juu ilikuwa ni jitihada tu ya kuzima zengwe na jinamizi la kisiasa linalomkabili.

What a waste.
Unajua tatizo ni ufinyu wa upembuzi wa mambo kwa wabunge wa CCM (Baadhi) kwani kwa sasa CCM haiwezi kuamua nani awe mbunge, uthibitisho tunao, we angalia kuanzia kwa shibuda na Arumeru! Kwa mwanasiasa mjaja alitakiwa amsapoti Zitto ili kujiwekea ngome bungeni, kwa sasa hata mi nikienda mfano kwa January na kusema ni fisadi anasapoti mafisadi wananchi watanielewa na nitawapa ushahidi wa sahihi za wabunge, ila vijana kama Njombe ni mjaja sana maana hao waliotia sahihi wamejijengea jina kubwa miongoni mwa wapiga kura
 
Je, ana tofauti gani na wabunge wenzake wa CCM ambao katika jambo kama hili na nyakati kama hizi, wana achana na siasa za vyama na kuweka maslahi ya taifa mbele? Unasema kwamba 'if he was in opposition he would say a lot and that i should believe you'. Naomba nikueleze tu kwamba maana ya opposition ni hii: "The action of opposing something that you disapprove or disagree with"; Je kwa mtazamo wako, January agrees and approves of what Zitto and other 70 or so Wabunge from various political parties, disapprove and disagree with? January ametuangusha vijana ambao tulikuwa tunamwamini sana. Sisi vijana mitaani ambao tumekuwa tunamtetea tunajificha wapi sasa. Angalau basi ange abstain kama wengine wengi walivyofanya kwani he had nothing to loose. But him being actively involved means anashindwa kutofautisha kati ya activity and productivity katika siasa za ushindani.
Pengine wenzangu wagumu sana kumsoma mtu..Huyo January mtamlaumu sana lakini he is very smart japokuwa ndio Unafiki wenyewe. Ana malengo yake na hatajali anamkanyaga nani ktk safari hiyo.

Kumbukeni kulikuwa na Issue mbili hapa. Moja ni shinikizo lao wenyewe CCM na kundi la EL kuwataka mawaziri wajiuzuru baada ya hotuba ya CAG, na waziri mkuu aliposuasua Zitto akaingia na hoja nyingine mpya (ya pili) ya kumwajhibisha Waziri mkuu ambayo Makamba na kundi lake hawakulitazamia na wala hawakuiafiki. wao walitaka tu mawaziri wajiuzuru ili wapate mwanya wa kupandikiza watu wao.

Hivyo Makamba alipingana na wazo la kumwajibisha Waziri mkuu akitegemea kikao chao watawawajibisha mawaziri waliokuwa tayari wamewaweka ktk list ya kundolewa, ndipo alipoandika madudu yake kujisifia kwamba wao wataifanya kazi kweli na sio hizi siasa za spinning za Chadema na Zitto kumtaka waziri mkuu ajiuzuru.

Sasa walipokaa kikao chao na kuyaweka majina 8 ya mawaziri walifikiri wameshinda maana hata Pinda mwenyewe aliogopa kupoteza nafasi yake akakubaliana nao. Kumbe JK alikuwa na picha tofauti kabisa maana anajua fika kwamba hii haikuwa kuwaondoa viongozi mafisadi bali mawaziri wa kambi yake na hivyo kuwapa nafasi mawaziri wapya wa kambi ya EL. JK anaweza kuwa mjinga lakini sii mjinga hivyo, hasa yanapokuja mambo ya kimujini na uswahili. Akawatoa nishai hivyo Makamba kabakia uchi wa nyama, kuimeza kauli yake anashindwa kakimbilia Norway kujipumzisha kwanza.

Hili liwe fundisho kwenu kwamba wapo viongozi wanafanya siasa kwa maslahi, Makamba sii kama mnavyomfiiria he is ambitious. First to be a minister na aliona mwanya hapa wa kufikia ndoto yake wakati akicheza na vichwa vya kina Zitto na vijana wengine kuelekea Urais sijui mwaka gani. UTU uzima jamani DAWA, tunawasoma vijana na tunaelewa makusudio yao hasa wanaporuka dirishani badala ya kupitia mlango mkubwa..
 
When you speak badly of someone, make sure you put down the reasons why you do so.
 
Huyu bwana mdogo ameonyesha tabia za kizee sana ya fear for unknown tofauti na watu wa hirimu yake. Kipimo cha Zitto kimewaengua wabunge wengi tuliokuwa tunadhani ni wazalendo kumbe ovyo!!! chini ya m/kiti January Makamba. Ameonyesha wazi hana lengo la kuwatumikia waTZ bali maslahi binafsi
 
Tumsubiri arudi toka Stavanger Norway tar 28 a-tweet hoja hizi kama alivyo tweet hio anayoita 'publicity stunt'. Shame on him
 
yule sio kiongozi ni kibaraka tu,kapewa shavu familia yao isife njaaa wezii haooo
 
Huyu kijana sijawahi kuona umuhimu wake wala uhazina wake kwa taifa; kwangu mimi yeye ni sawa tu na Nape na William Malecela- wapo kulinda mzimu CCM kwa vile wazazi wao walipita huko- they cant forget honey and milk they have enjoyed since were born.

Ni kosa kubwa sana tena ni zarau ya hali ya juu kumlinganisha Januari na Zitoo na mbaya kama atahusishwa na nafasi ya juu ya uongozi aidha wa kichama au hata Kiserikali.Historia yake ya shule na mifumo ya utendaji kazi wake haioneshi kama anaweza kuwa hata katibu tarafa.Ajabu amekuwa mwenyekiti wa kamati tena kamati mama ya kukuza uchumi na kusaidia maendeleo ya Taifa. Huu ni mzaha wa hali ya juu.Duniani kote nishati na madini ndio msingi wa uchumi.Soma Historia za chumi kubwa duniani ukianza na Marekani, Ujerumani, Uingereza na kwingine hakuna hata mmoja aliyefanikiwa nje ya matumuzi bora ya nishati na madini. Kwetu sisi wanaleta mzaha.Kuna haja ya kujifunza kutoka kwa Chelsea.Haya mambo yanawezekana.
 
Back
Top Bottom