Anguko la January Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anguko la January Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jazzie, Apr 24, 2012.

 1. Jazzie

  Jazzie Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Acts 13:36 – “For when David had served God's purpose in his own generation, he fell asleep; he was buried with his fathers and his body decayed

  Ni ukweli usiopingika kwamba kila kizazi kinahitaji kiongozi wake. Hiyo ni kwa sababu kila kizazi kina matatizo yake, maono yake, na matakwa yake. Ni ukweli usiopingika kwamba kizazi cha Tanzania leo hii kina kiu ya kiongozi wake.

  Kwa muda ilionekana kama vile kuna vijana wawili – January Makamba and Zitto Kabwe, ambao walikuwa tayari kubeba jukumu la kusimama kama nyota ya uongozi wa kizazi kipya. Kili mmoja wetu anajua kilichojiri Bungeni hivi karibuni, hasa uamuzi wa January Makamba kupingana na hatua aliyoingoza Zitto Kabwe ya kudai uwajibikaji serikalini.

  Ni dhahiri, ingawa wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti, kwamba January amejiweka katika wakati mgumu kisiasa, hasa mbele ya vijana waliomtegemea.

  Kwa muda January Makamba aliweza kung’ara katika anga za siasa Tanzania kwa sababu ya uwezo wa kupambanua mambo. Lakini kilichotokea Bungeni kimedhihirisha kitu kimoja – uwezo wa January kupambanua mambo na kutoa kauli “zilizoenda shule” peke yake hakumfanyi mtu kuwa kiongozi na shujaa wa kizazi chake. Kuna wakati na mazingira yanamtaka kiongozi kudhihirisha mawazo na moyo wake ulipo.

  Pale Bungeni, wakati huo ulitokea na bahati mbaya sana January akaugopa wakati huo.

  Pale mjengoni, January Makamba alidhihirisha kwamba mawazo yake na moyo wake yako mbali kama Mashariki iliyo mbali na Magharibi. Na ndio maana dhana ya “unafiki” inamzonga January. Katika utetezi wake, January Makamba aliandika hiki hapa chini:

  "I can disagree with Zittokabwe on methods to reach the same objectives, and we are still brothers"

  Mpaka leo sijasikia chochote toka kwa January kuhusu njia mbadala (tofauti na njia aliyopendekeza Zitto Kabwe) ya kuleta uwajibikaji serikalini. Kwa mantiki hiyo, hiyo kauli yake hapo juu ilikuwa ni jitihada tu ya kuzima zengwe na jinamizi la kisiasa linalomkabili.

  What a waste.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi sijawahi kumweka kwenye list ya viongozi watarajiwa wa nchi hii
   
 3. s

  sambamba Senior Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtoto wa nyani hawez kuwa mbwa atabak nyani2 january km dngi yake kwan dngi yake alvyokuwa mkuu wa mkoa wa Dar alikuwa mkali finally akaja jinyea nyea ndo km huyu nduza mwanae.
   
 4. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unafiki wa kichama umemteka Januari
   
 5. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Kwenye long term serving leaders hayumo ila kwenye ccm yupo, mark my word! Siku si nyingi atakuwa juu lakini 2015up no!
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  january was my first choice tena mbele ya ZITTO
  ILA KWA SASA NAONA NAFUU UWE NA WATU KAMA SOFIA SIMBA kuliko kuwa na JANUARI

  JANUARI kajiaribia sana na kwa kifupi kajimaliza sitokaa nimwamini tena

  big up zitto
   
 7. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 607
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Huyu kijana sijawahi kuona umuhimu wake wala uhazina wake kwa taifa; kwangu mimi yeye ni sawa tu na Nape na William Malecela- wapo kulinda mzimu CCM kwa vile wazazi wao walipita huko- they cant forget honey and milk they have enjoyed since were born.
   
 8. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mie labda mnisaidie wana JF, maana hawa wote wenye majina makubwa (kutoka kwa baba zao) huwa nawachukia siamini kwamba wanapata mafanikio kwa kuwa ni wachapakazi. Mwenye ushaidi kunibadilisha mawazo haya niliyonayo please come forward, zawadi nono itatolewa
   
 9. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,357
  Likes Received: 6,539
  Trophy Points: 280
  hivi kuna ulazima gani wa watoto nao kuwa viongozi kama baba zao..hapo ndipo ninapopata kichefuchefu..kwani hakuna wengine wa kuongoza..tumejaa tele lakini kubaniana na kupeana nafasi kwa vilaza ndio kunaendelea..
   
 10. c

  cr9 Senior Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  the thing is ukiyakumbatia matapishi na yenyewe yakawa mengi nawe unabadilika kuwa sehemu ya hayo matapishi.
  hawa jamaa lazima waelewe wananchi wanawaangalia kila step wanayoifanya iwe bungeni au nje ya bunge na siku moja watahitajika kuwajibika juu ya kauli zao zote.

  Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania.
   
 11. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,770
  Trophy Points: 280
  a coward is a liar. january ni muoga.
   
 13. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Anguko kwani alikuwa juu?mi ndivyo alivyo tuu
   
 14. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  January aliwagwaya viongozi wa ccm! Hatufai vijana ni kiongozi mwoga na si jasiri!
   
 15. R

  Rweza Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naye anaogopa maana anajua akinyanganywa kadi tukirudi jimboni hana chake mbele ya M4C yenye kasi ya kimbunga.
   
 16. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Na mara baaday ya kuona kuwa ameingia cho cha kike siku ile, hakuwa tene na nguvu ya kwenda kusoma majumuisho ya kamati yake badala yake akamrushia yule mama wa singida.

  Waliambiwa na V. Nyerere kuwa tegeme utapata nini ukiruka sarakasi huku umevaa taulo!!!! hao ndo majibu yake, na bado!!!
   
 17. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Bumbuli hawana mtu hapo!
   
 18. g

  guta Senior Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Akisaini unadhani atapatawapi uwaziri baraza likivunjwa?
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mwenzenu hana hata muda nanyi, ndiyo kwanza anasema wabongo wanachonga sana bila kujua wanaloongea, na wao viongozi wenye kujua hawaongei kuwajuza wabongo katika style ya "aliyelala usimuamshe..."

  The nerve...
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  huyo kijana anatamani uwaziri nishati na madini mnafiki tu.
   
Loading...