Anguko la Euro; Je, ni fursa au hasara kwa nchi za kiafrika?

Sheffer95

Senior Member
Mar 16, 2020
197
460
Habari wakuu nawasalimu,

Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa pesa ya ulaya ikipoteza thamani na kuwa sawa na dola ya kimarekani. Huku Urusi wakiendelea kupokea malipo yote kwa pesa yao, na India wakitaka kuanza kufanya miamala yote kwa pesa yao(rupee).

Je, hili linatafsiri gani kwa nchi za kiafrika ambazo toka mgogoro huu wa urusi na Ukraine uanze basi wamepata visingizio vingi hasa baada ya bidhaa na huduma za msingi kupanda.

Je, ni wakati sahihi kwa hizi nchi kurudi kwenye agenda zinazowagusa wananchi moja kwa moja kama kilimo kuwekeza na kuhakikisha wanaweza jitegemea.

Je, nchi za ulaya zinazopambana na kupanda kwa gharama za maisha kwao zitapunguza au kusitisha misaada barani Africa?

Hii hali iliyopo sasa ina faida au hasara gani kwa nchi za kiafrika ambazo 70% zina malimbikizo makubwa ya madeni ya nje.

Ni hayo tu ahsanteni na karibuni kwa mjadala
 
Back
Top Bottom