Anguko la CHADEMA lipo njiani

Anguko la CHADEMA lipo njiani

Wana JF.
Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema). Kimejipa jina hilo maudhui makuu katika jina hilo, ni mawili tu.

Demokrasia na Maendeleo.

Demokrasia kwa maana ya fursa kwa mwanachama na kiongozi wake asiyeweza kuipata katika chama kingine chochote kile nchini, fursa ya kushiriki katika maamuzi muhimu ya chama.

Maendeleo kwa kila Mtanzania, yanayotokana na mgawanyika sawa wa rasilimali za taifa hili.

Leo chama hicho kinapata mamilioni kwa ajili ya maendeleo ya chama kupitia ruzuku ya Serikali, lakini mamilioni yote hayo hatuoni yanavyoendeleza wanachama wake, achilia mbali chama chenyewe hicho.

Watanzania wapenda amani wameishakuwa makini na Chadema kwamba chama hicho ni hatari kwa ustawi wa jamii.

Viongozi wanaounda Baraza Kuu na Kamati Kuu, ni wale waliokosa uvumilivu ndani ya vyama vya siasa walivyokuwamo mwanzo, wengi wao wakiwa wametokea CCM baada ya matamanio yao ya kupata madaraka waliyoyataka kukosekana huko, akiwamo DK. Slaa mwenyewe.

Ni wazi siku si nyingi anguko la Chadema tutaliona miongoni mwa hao watapatikana kina Yuda Iskarioti waliokata tamaa, na hilo ndiyo litakuwa anguko la Chadema.

Kwa hiyo ulikuwa unataka watoke mbinguni kusiko kuwa na vyama?
 
Watu wenye akili zetu tunapoandika kuwaasa Watanzania wenzetu wajiepushe na chama hicho, tukiwasihi watuamini kwamba hicho kinachoitwa Demokrasia na Maendeleo ndani ya hicho chama ni ghilba na hadaa tu inayolenga kuwanufahisha baadhi ya waliomo, wanakuwa na moyo migumu kama kina Tomaso wa enzi za Yesu.

kwahiyo unataka wajiunge chama gani? unaposema tatizo toa na solution.
 
Mleta uzi ana matatizo. Ruzuku ya CCM chama cha magamba inafanya nini???? Sikumbuki ni lini niliona maelezo kuhusu matumizi ya ruzuku ya CCM au chama chochote cha siasa mbona ameishupalia CHADEMA?. Tafadhali mleta uzi tuonyesha matumizi ya ruzuku wanazopata vyama vingine vya siasa kablba hujainyooshea kidole CDM
 
Aisee SSM kila mkilala ni chadema tu!! Haki ya nani kweli inawapa tabu na post zenyewe hazina kichwa wala mguu ni kigugumizi tu!! Sasa ona wanavyokuchambua hapa!! Waite wenzio waje wakusaidie kama yule wakili wenu katika rufaa ya Mnyika alisema naomba niende kuomba wakili mwingine wa kusaidia maana hii ngumu!! Chezea vichwa vya CDM weye!! Spike Lee!! umejionea mwenyewe.

wewe kama si mmachame basi kibosho sindo washika dau
 
Watu wenye akili zetu tunapoandika kuwaasa Watanzania wenzetu wajiepushe na chama hicho, tukiwasihi watuamini kwamba hicho kinachoitwa Demokrasia na Maendeleo ndani ya hicho chama ni ghilba na hadaa tu inayolenga kuwanufahisha baadhi ya waliomo, wanakuwa na moyo migumu kama kina Tomaso wa enzi za Yesu.
Umeshonyesha utabiri wako vizuri na unalozungumzia ni jambo ambalo linaweza kutokea kama vile vile ambavyo jambo hilo linavyoweza kutokea kwa CCM.
Wakati CUF ikiwa tishio wengi wa wana CCM waliamini ya kuwa kuidhoofisha CUF kutawapa fursa ya kupumua lakini matokeo yamekuwa kinyume.Leo hii hakuna ngangari wala jino kwa jino ila ni hoja ambazo zinaonekana kuwa tishio kubwa zaidi.
Leo mamlaka ya Rais ya kuteua majaji yamehojiwa kwa hoja na taasisi hiyo imevuliwa nguo na washauri wa Rais wanaonekana wanaonekana hawamshauri vizuri mkuu.
Spika wa bunge anapata mpaka kigugumizi wakati anapoona mkono kutoka katika bech la wabunge wa upinzani lakini kubwa zaidi ni kuwa haya yote CCM inayofanya sasa ni woga wa kuondolewa madarakani na kama ulivyosikia deni lataifa limeongezeka na serikali inakopa mpaka bank binafsi ili angalau iwe na cha kuonyesha2015.
Hitimisho,ikianguka CDM kitainuka chama kingine chenye nguvu kubwa na mbinu zaidi ya CDM na hiyo haitakuwa na SIHA kwa CCM.Salama ya CCM ni kujisafisha,kuacha kukumbatia ufisadi na mafisadi na kuhakikisha ugumu wa maisha unapungua kinyume cha hayo ni anguko la CCM na si CDM kwani CDM haipo madarakani kwa hivyo haiwezi kuanguka.
 
Wana JF.
Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema). Kimejipa jina hilo maudhui makuu katika jina hilo, ni mawili tu.

Demokrasia na Maendeleo.

Demokrasia kwa maana ya fursa kwa mwanachama na kiongozi wake asiyeweza kuipata katika chama kingine chochote kile nchini, fursa ya kushiriki katika maamuzi muhimu ya chama.

Maendeleo kwa kila Mtanzania, yanayotokana na mgawanyika sawa wa rasilimali za taifa hili.

Leo chama hicho kinapata mamilioni kwa ajili ya maendeleo ya chama kupitia ruzuku ya Serikali, lakini mamilioni yote hayo hatuoni yanavyoendeleza wanachama wake, achilia mbali chama chenyewe hicho.

Watanzania wapenda amani wameishakuwa makini na Chadema kwamba chama hicho ni hatari kwa ustawi wa jamii.

Viongozi wanaounda Baraza Kuu na Kamati Kuu, ni wale waliokosa uvumilivu ndani ya vyama vya siasa walivyokuwamo mwanzo, wengi wao wakiwa wametokea CCM baada ya matamanio yao ya kupata madaraka waliyoyataka kukosekana huko, akiwamo DK. Slaa mwenyewe.

Ni wazi siku si nyingi anguko la Chadema tutaliona miongoni mwa hao watapatikana kina Yuda Iskarioti waliokata tamaa, na hilo ndiyo litakuwa anguko la Chadema.

Umetumwa na lowasa? Umetumwa na nape? Umetuma na huyo anayetumia jina la mtu? Umetumwana na kinana wenu ambaye yuko kimya baada ya tuuma za pembe za ndovu? Umetumwana na jk? Umetumwa na nani? Ebu kuwa wazi basi umetumwa na nani ndugu?
 
si uanzishe chama chako tu kama unaona Chadema hakuna demokrasia? Katiba inakurusu kuanzusha chama chako ambacho wewe mwenyewe unaona kitakuwa na demokrasia sio unatokwa mapovu na mishipa kwa chama walichoanzisha wenzako na wanakiona kina demokrasia,leo hii sijui umegombana na mkeo huko unakurupuka tu anguko la chadema lipo njiani na anguko la kwako lipo wapi?
 
......
Viongozi wanaounda Baraza Kuu na Kamati Kuu, ni wale waliokosa uvumilivu ndani ya vyama vya siasa walivyokuwamo mwanzo, wengi wao wakiwa wametokea CCM baada ya matamanio yao ya kupata madaraka waliyoyataka kukosekana huko, akiwamo DK. Slaa mwenyewe.....

Nakupongeza kwa pointi zako murua. Mchango wangu kwenye mada yako ni huu:

Huo ugonjwa wa kukosa uvumilivu kwenye chama upo kwenye kila chama cha siasa hapa Tanzania, sio Chadema tu. Steven Wassira alikuwa CCM, alipoona maslahi yake yanalegalega akahamia NCCR, then Chadema, halafu akarudi CCM ambako naona maslahi yake yanaenda vizuri. Jiulize, jina la Tyson alilopewa Wassira lilitokana na nini? Labda nikukumbushe historia ya watu wa namna hiyo, ambao walihamahama vyama kutafuta maslahi manono, pale ambapo hawakuridhika na vyama walivyopo!
  1. Danhi Makanga>>CCM>>UDP>>CCM
  2. Daniel Nsanzugwanko>>CCM>>Chadema>>CCM
  3. Sambwee Shitambala>>CCM>>Chadema>>CCM
  4. Richard Hizza (Tambwe)>>CUF>>CCM
  5. Augustine Mrema>>CCM>>NCCR>>TLP
  6. Thomas Ngawaiya>>CCM>>TLP>>CCM
  7. Thomas Nyimbo>>CCM>>Chadema>>CCM
  8. Njelu Kasaka (G 55)>>CCM>>CUF>>CCM
  9. John Guninita>>CCM>>Upinzani (sina uhakika kama alienda NCCR/Chadema)>>CCM
  10. John Magale Shibuda>>CCM>Chadema>>???

Wengi wa waliorudi CCM wamepewa ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa na wengne kama akina Shitambala wameshinda viti vya NEC. Ni mkakati wa Yusufu Makamba wa muda mrefu sana. Lengo la kuwapa vyeo hawa akina 'hamahama' ni kuua upinzani ili ibakie CCM pekee. Ni sana na kukausha bwawa ili ukamate samaki, badala ya kuwavua kwa chambo na nyavu ama ndoano!
Orodha ya wasaka tonge ni ndefu sana. Kimsingi wanasiasa wa Tanzania wanasaka maslahi yao kwanza, maslahi ya waliowachagua yanakuja baadaye sana. Hi ipo kila chama. Hata leo, usione Nape na Nchemba wanapiga kelele majukwaani, CCM ikiwakera kidogo utashangaa wanaingia kwenye operesheni PEREGE/KAMBALE n.k.
Nawasilisha
 
haakuna liSilokua na mwishomndugu mtoa maDA.....HATA CCM ITAKUFA'''''''''''''hivi cccm adui yake mkubwa ni chadema;;; baada ya kuiombea rushwa,umaskin ufe,maradhi yafe, ujinga ufe mmekazana na chadema
 
jaman hawa vijana wachumia tumbo..mtakufa kibudu kwa tamaa zenu na ulafi uliyopitilza... Vijisent vya mafisadi vinawafanya mtape tape kama kunguru asiefugika.. Mtaanguka nyie mafisadi na chama chenu nyinyiem na masalia yenu.. Funguka akili na ujipange upya nyie vijana njaa..
 
Watu wenye akili zetu tunapoandika kuwaasa Watanzania wenzetu wajiepushe na chama hicho, tukiwasihi watuamini kwamba hicho kinachoitwa Demokrasia na Maendeleo ndani ya hicho chama ni ghilba na hadaa tu inayolenga kuwanufahisha baadhi ya waliomo, wanakuwa na moyo migumu kama kina Tomaso wa enzi za Yesu.
UKiangalia tarehe uliyojiunga humu yaonyesha ni mmoja ya wale mliotumwa na wassira na mwigulu baada ya kikao chenu ....uwa napata tabu sana kukutana na watu wanaofikiria kwa kutumia tumboo
 
jaman hawa vijana wachumia tumbo..mtakufa kibudu kwa tamaa zenu na ulafi uliyopitilza... Vijisent vya mafisadi vinawafanya mtape tape kama kunguru asiefugika.. Mtaanguka nyie mafisadi na chama chenu nyinyiem na masalia yenu.. Funguka akili na ujipange upya nyie vijana njaa..
 
dua la kuku halimpati mwewe, halafu, wewe ni (a) mmoja wa wachache wanaofaidi rasilmali za nchi hii au (b)unataka wafaidi rasilmali wakuone wakugawie kidogo? kama ni (a) hongera na kama ni (b), angalia sana ndugu, watakutumia kisha kukudump, hawajuagi kumthamini mtu hao
 
Mkuu chama,
Nasoma hoja nzito za Spike Lee, kaongea ukweli mtupu.
 
Last edited by a moderator:
Mbona watu wazito kuelewa Kama Zito!huyo Zito hatofukuzwa na mtu atajifukuza mwenyewe na shibuda wake muda wao ukifika wataondoka Mbona maandishi yapo ukutani,akili zakupambambanua ham nazo.........

Mbowe na Dr Slaa wanajua gharama ya kumfukuza Zitto; kama Juliana anatiwa hatiani unawezaje kymwacha Zitto?! Kwann pia Juliana asingejifukuzisha mwenyewe? Zitto ana influence kubwa sana kwa wananchi na wanachama wengi wa cdm; hawezi kufukuzwa kirahisi na cdm kubaki salama licha ya kuwa na tuhuma nyingi dhidi yake;
 
Kutumika vibaya ni kubaya sana, hivi huko Lumumba hamuoni kuwa huu upuuzi wenu wa kipuuzi watanzania walishaupuuza?
 
Nakupongeza kwa pointi zako murua. Mchango wangu kwenye mada yako ni huu:

Huo ugonjwa wa kukosa uvumilivu kwenye chama upo kwenye kila chama cha siasa hapa Tanzania, sio Chadema tu. Steven Wassira alikuwa CCM, alipoona maslahi yake yanalegalega akahamia NCCR, then Chadema, halafu akarudi CCM ambako naona maslahi yake yanaenda vizuri. Jiulize, jina la Tyson alilopewa Wassira lilitokana na nini? Labda nikukumbushe historia ya watu wa namna hiyo, ambao walihamahama vyama kutafuta maslahi manono, pale ambapo hawakuridhika na vyama walivyopo!
  1. Danhi Makanga>>CCM>>UDP>>CCM
  2. Daniel Nsanzugwanko>>CCM>>Chadema>>CCM
  3. Sambwee Shitambala>>CCM>>Chadema>>CCM
  4. Richard Hizza (Tambwe)>>CUF>>CCM
  5. Augustine Mrema>>CCM>>NCCR>>TLP
  6. Thomas Ngawaiya>>CCM>>TLP>>CCM
  7. Thomas Nyimbo>>CCM>>Chadema>>CCM
  8. Njelu Kasaka (G 55)>>CCM>>CUF>>CCM
  9. John Guninita>>CCM>>Upinzani (sina uhakika kama alienda NCCR/Chadema)>>CCM
  10. John Magale Shibuda>>CCM>Chadema>>???

Wengi wa waliorudi CCM wamepewa ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa na wengne kama akina Shitambala wameshinda viti vya NEC. Ni mkakati wa Yusufu Makamba wa muda mrefu sana. Lengo la kuwapa vyeo hawa akina 'hamahama' ni kuua upinzani ili ibakie CCM pekee. Ni sana na kukausha bwawa ili ukamate samaki, badala ya kuwavua kwa chambo na nyavu ama ndoano!
Orodha ya wasaka tonge ni ndefu sana. Kimsingi wanasiasa wa Tanzania wanasaka maslahi yao kwanza, maslahi ya waliowachagua yanakuja baadaye sana. Hi ipo kila chama. Hata leo, usione Nape na Nchemba wanapiga kelele majukwaani, CCM ikiwakera kidogo utashangaa wanaingia kwenye operesheni PEREGE/KAMBALE n.k.
Nawasilisha

11. Dr Wilbroad Slaa >> CCM>>CHADEMa
12. Lamwai >>CCM>>NCCR Mageuzi>>CCM
13. Seif Sharif Hamad>> CCM>>CUF>>CCMCUF
14 Kafulira >>chadema>>nccr mageuzi>> next > chauma
15. ZZK >>Chadema>> next >>chauma or CCM
 
Back
Top Bottom