Anguko la CHADEMA lipo njiani

Anguko la CHADEMA lipo njiani

Hivi hili anguko@litatokana na kuwafukuza wasaliti au?

Wana JF.
Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema). Kimejipa jina hilo maudhui makuu katika jina hilo, ni mawili tu.

Demokrasia na Maendeleo.

Demokrasia kwa maana ya fursa kwa mwanachama na kiongozi wake asiyeweza kuipata katika chama kingine chochote kile nchini, fursa ya kushiriki katika maamuzi muhimu ya chama.

Maendeleo kwa kila Mtanzania, yanayotokana na mgawanyika sawa wa rasilimali za taifa hili.

Leo chama hicho kinapata mamilioni kwa ajili ya maendeleo ya chama kupitia ruzuku ya Serikali, lakini mamilioni yote hayo hatuoni yanavyoendeleza wanachama wake, achilia mbali chama chenyewe hicho.

Watanzania wapenda amani wameishakuwa makini na Chadema kwamba chama hicho ni hatari kwa ustawi wa jamii.

Viongozi wanaounda Baraza Kuu na Kamati Kuu, ni wale waliokosa uvumilivu ndani ya vyama vya siasa walivyokuwamo mwanzo, wengi wao wakiwa wametokea CCM baada ya matamanio yao ya kupata madaraka waliyoyataka kukosekana huko, akiwamo DK. Slaa mwenyewe.

Ni wazi siku si nyingi anguko la Chadema tutaliona miongoni mwa hao watapatikana kina Yuda Iskarioti waliokata tamaa, na hilo ndiyo litakuwa anguko la Chadema.
 
Kufukuzwa masalia ni pigo takatifu huko Lumumba. Mtaweweseka sana mwaka huu.
 
Hivi kumbe bado pana watu wanawaza utawala wa CHAMA KIMOJA!!!!!
 
Watu wenye akili zetu tunapoandika kuwaasa Watanzania wenzetu wajiepushe na chama hicho, tukiwasihi watuamini kwamba hicho kinachoitwa Demokrasia na Maendeleo ndani ya hicho chama ni ghilba na hadaa tu inayolenga kuwanufahisha baadhi ya waliomo, wanakuwa na moyo migumu kama kina Tomaso wa enzi za Yesu.
Imeishakula kwenu mtahangaika sana
 
nafananisha na ile hadith ya fisi kuzani mkono wa banadamu utanguka pale mala pale mala kuhamaki cdm wako ikulu
 
DK.Slaa huyu ndiye tumaini la Chadema. Pamoja na kwamba wanajua hataweza kukanyaga Ikulu kwa sababu Watanzania hawajawa wajinga kiasi hicho. Lakini wanajua wakimtumia vizuri Dk.Slaa ni mtaji wa kuongeza ruzuku, fursa kuu ya kiuchumi ambayo ndiyo lengo kuu la Chadema

Kwa kweli Watanzania wana akili sana, si huoni madini waliwapa wazungu wanaachia wasukuma mashimo, si huoni ndege waliwapa wasouth africa, si huoni hela zao ziko uswisi, si huoni katiba mpaka cdma wawaandamane ndio inaletwa, si huoni waliuza utu wao mwaka 2005 kwa hela zao za EPA, si huoni walivyowakarimu ndio mana wanagawa hela kupitia kagoda, richmond na kadhalika.
 
Una shida weye, yaani hata kama huna point ya kuandika lazima uandike ili mabwana wako wa Lumumba waone uko kazini!?
Haya subiri, kama NGUVU YA UMA huwa inaanguka.
 
Unachosha watu kwa hoja butu, Chadema sio chama cha genge la wahuni, watoa matusi, na kuhujumu chama, hayo huko huko kwa magamba. Sisi CDM tunasema no stone will be left unturned mpaka tumalize wasaliti na wazandiki wote. Hatuangalli sura Chama hakiwezi kujengwa kwa kulea wahuni eti watahama, wahame tena haraka kabla ya panga halijawakumba. Sisi hatutishii kama wenzetu Magamba eti tuwape siku za nn wakati tunawajua. Timua wote wakafie mbali wehu hao wanachafua chama kwa kupewa posho za wali mbuzi.
 
Kufukuzwa masalia ni pigo takatifu huko Lumumba. Mtaweweseka sana mwaka huu.

Watu wametoa ushauri sana hapa la kuachana na mikakati ya kizamani, lakini bado hawasikii! Kila zama na mambo yake!
 
Watu wenye akili zetu tunapoandika kuwaasa Watanzania wenzetu wajiepushe na chama hicho, tukiwasihi watuamini kwamba hicho kinachoitwa Demokrasia na Maendeleo ndani ya hicho chama ni ghilba na hadaa tu inayolenga kuwanufahisha baadhi ya waliomo, wanakuwa na moyo migumu kama kina Tomaso wa enzi za Yesu.

wengine tumekuelewa vizuri sana,tatizo hujasema baada ya kuwashtukia hawa chadema na njama zao je,ni chama gani mbadala kwa manufaa ya watanzania na tanzania yenyewe,mabadiliko tumeumbiwa binadam hivo hatuwezi kuyazuia japo kuyachelewesha inawezekana! Chukua nawe ushauri wangu huu usiweke uzibe,ccm ata kama haitang'olewa na chadema lakini mda ukifika ata TADEA itachukua,ni bora ukakutwa unajiaandaa ili usile hasara kama wale walogeuza hekalu la Bwana sehemu ya uchuuzi/soko, aliyekuwa na njiwa hakumpata hata njiwa wake mmoja!
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha,endeleeni kulea migogoro kwa kivuli cha ccm-kama hamtaumbuka.
 
kuwafukuza wasaliti ndani ya chama hijaanza kwa kina mchange, mtela na shoza. nenda mbali zaidi kwa kuwauliza watu wa arusha kuwa baada ya kuwafukuza viongozi wake (madiwani) watano waliochaguliwa na wananchi (arusha), chama kilibaki na taswira gani mbele ya wana arusha na watanzania kwa ujumla. ukipata jibu linganisha na fukaza fukuza hii na dhana ya vua gwanda ya CCM ili kujiridhisha ni chama kipi kinalinda nidhamu yake na kujenga imani kwa watanzani. wahenga walisema "mwana umleavyo........"
 
Watu wenye akili zetu tunapoandika kuwaasa Watanzania wenzetu wajiepushe na chama hicho, tukiwasihi watuamini kwamba hicho kinachoitwa Demokrasia na Maendeleo ndani ya hicho chama ni ghilba na hadaa tu inayolenga kuwanufahisha baadhi ya waliomo, wanakuwa na moyo migumu kama kina Tomaso wa enzi za Yesu.
Utadhani unaendesha Guta.Mungu akusaidie.
 
ili iweje chadema ikianguka?,,,,,mpate raha ya kuiba........
 
Mawazo haya yanatisha na kukatisha tamaa. Kama ma great thinker tulionao ndiyo hawa, basi ni KAZI KWELI KWELI!! Mimi siyo mwanachama wa Chadema, lakini sipendi chama hicho kife. Nashabikia kipate nguvu ikiwezekana sawa au zaidi ya chama tawala kwa nia ya ku-balance nguvu za maamuzi kwa mustakabali wa nchi yetu. Ni pale kunapokuwa na upinzani wenye nguvu, katiba imara, nguzo tatu za uongozi wa nchi zilizo huru ndipo tunaweza kama nchi kurealize maendeleo. Nchi zote tunazozisifia kwa kuwa na maendeleo zinaheshimu demokrasia na amani ya kweli (Kenya itakuwa mfano nahakika baada ya uchaguzi huu). Kwa hiyo kushabikia chadema kufa ni aibu kubwa.
 
Vijana kuweni makini! Epukeni short cut. Mission mnazopewa ndo makaburi yenu! Kumbuka ukishindwa ku fulfil mission either uuawe ili kutunza siri au utoroke na uish maisha ya digidigi! KIJANA JIAMINI TUMIA JASHO LAKO NDO LENYE BARAKA ZA MAISHA YAKO EEH!
 
Tanzania tanzania peopoplesss pawaaaaaaaaa,Chadema chadema peopl.................naimba tuu nitarejeeea

Eti hapa ulikuwa unataka kumaanisha nini?

Umeandika nini hapo?
 
Back
Top Bottom