mfano kuna madai bayana kabisa daftari la wapiga kura lilirekebishwa siku tatu kabla ya uchaguzi kwann, maboresho hayo yalifanywa na tume ya uchaguzi kimya kimya, walikuwa wanaficha nini maana si ingewekwa hadharani watu wajiandikishe.
kuna watu walikuwa na shahada zimechanika au majina yao yalikuwepo katika daftari la wapiga kura ila hawakuwa na kitambulisho kutokana na kupoteza au kuibiwa, kisheria wanatakiwa wasaidiwe wajaze fomu maalumu na waruhusiwe kupiga kura, kwann walizuiwa kujaza fomu hiyo na kupiga kura,
moja ya chama cha siasa kilikuwa na majina ya watu ambao watakipigia kura je walijuaje kuwa watawapigia kura hata kama ni wanachama wao,kwani mwanachma wa cdm au ccm au cuf wanalazimika kuvipigia kura vyama vyao, kura ni siri ya mtu na ana haki na hiyari ya kumpigia mtu ambaye hata kama sio wa chama chake,
kulikuwa na madai ya vipigo, utekaji, unyanyasaji na vitisho hivyo navyo unasemaje?
mm sio mwana siasa ila napenda kuchangia mada zenye nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu. kama huna data fanya utafiti upate ukweli halafu utujuze yaliyotokea kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. vinginevyo utadharauliwa na kuhesabiwa si kitu hata mbele za Mungu maana wala rushwa, wachawi, wazinzi, watukanaji, wafiraji, walawiti, waabudu sanamu, waongo wote na wenye dhambi hawataurithi uzima wa milele bali sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto na kiberiti ufunuo 21.8, mathayo 1.21, kumbukumbu 10.17, mathayo 25.41
ukifanya utafiti utatusaidia kupata ukweli watu ambao hatukufika huko ikiwa ni pamoja na kujibu hoja zote bila kumung'unya maneno utakuwa mzalendo na mpenda maendeleo. kama kweli umelipwa buku 7 au kiwango chochote cha fedha kwa kuleta uzi ambao haujakamilika unadhalilisha vijana/watu wa rika lako. nchi inaweza kuendelea na kujengwa na mtu mmoja mwenye hekima ikaliwa na majambazi elfu nyingi. kajipange huenda watu watakuelewa