Ama kwa hakika hakuna kulipo salama!
Kasikika Mwabukusi:
1. Kudogosha taarifa ya Polepole kuwa mifumo INEC na NIDA kusomana ni jambo la kawaida. Sina hakika alisahau kuwa kwa mujibu wa Polepole kulikuwa na mfumo wa tatu uliotajwa pale. Haikuwa siri, kulikuwa na mfumo wa CCM uliotajwa pamoja na miwili ile. Pia kuwa hoja haikuwa mifumo hiyo kuunganishwa tu, bali ilikuwa ni suala la kujirisha na ambacho kimekuwa kikiendelea kwenye utatu wa muunganiko huo usiokuwa na afya kuhusiana na chaguzi zote kuanzia 2014/15!
Je Mwabukusi alikuwa kaghafilika tu au kuwa alitokea kwa waandishi wa habari kwa bahati mbaya na labda bila tahadhari au hata maandalizi ya kutosha?
2. Katokea tena jana akisifia ziara na mapokezi mazuri waliyopata chamwino, na kuwa amekubaliana na anamwunga mkono mheshimiwa bila kuwa wazi vilivyo ni kwenye nini hasa.
Huu uungwaji mkono kwa mfano, je:
a) Ni kwenye Lissu kuendelea kuwa gerezani hadi baada ya uchaguzi?
b) Ni kwenye mitano mingine?
c) Ni kwenye waliopotea wakiwamo kina Mdude kwamba status quo kuendelea?
d) Ni kwenye uchaguzi kuendelea bila reforms?
e) Ni kwenye kusikilizwa tu bila tafsiri ya lolote litatokea lini? Yaani kwenye mali kauli tu?
nk.
Siyo siri impendeze Mwabukusi kutoa ufafanuzi kwa maana wengine tulishaumwa sana na nyoka. Hapa ikizingatiwa hata mwamba kabla ya kwenda kunywa chai ikulu alionekana kuwa mwanetu!
Walisikika pia baadhi ya wanaharakati ya Sauti ya watanzaniakumbagaza mno Polepole kuliko hata ma CCM. Kuwa eti hajasema lolote la maana. Kwamba yote aliyosema hadi sasa si mali kitu na kuwa yalijulikana na lawama nyingi lawama dhidi yake kuhusiana na awamu ya tano utadhani Polepole alikuwa rais, makamu, au hata waziri kwenye awamu hiyo!
Kwamba kwa hao ndugu Polepole hafai kabisa kuliko hata waandamizi waliokuwa vinara zaidi yake kwenye serikali hiyo. Looh! Kwamba yao hayo si machozi ya mamba kweli?
Mtu unajiuliza "Polepole si kaomba msamaha? Zaidi sana, kwani vita si tunapigana na agenda za leo? Au wao wamefanya lipi wapi lenye impact?" Ama kwa hakika haieleweki wanaharakati hao wanataka, au hawataki nini.
Kwa angalizo la Polepole kuhusiana na wahuni, tunayo haja ya kuangaliana vyema usoni, mdomoni, matendo na hata madhila tunayopata na hasa kutoka kwa yule kiherehere kwenye mapambano. Bila kusahau pana wenzetu wa kufanana na wale nguli wa pale ACT Wazawa ambao panga pangua, wao huwa hawakamatwi kabisa! Kwamba ni design ile ile ya mwamba na kina Mdude. Kuwa kwenye hoja moja au msala mmoja, kipondo cha mbwa Koko na kukamatwa ni kwa akina Mdude, ila mwamba yeye, aah aah!
Ama kweli wahuni si watu wazuri na hasa walioko kwetu, hao ni wabaya zaidi kuliko wale wa wazi wazi upande ule mwingine.
Ikumbukwe imeandikwa: "umdhaniaye siye, ndiye." Muhimu kuona haikuandikwa umdhaniaye ndiye siye!
Ninawasilisha!