Angalizo.....!!!Chukua tahadhari sana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalizo.....!!!Chukua tahadhari sana.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Oct 9, 2010.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Leo nilivyoamka tu nikawasha simu yangu, na mara moja nikapokea message 2 kama ifuatavyo:

  ''Slaa ni mropokaji na mgomvi anayelumbana na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi.Anataka damu imwagike ili mradi ashinde. Tusikubali nchi yetu iwe kama.....
  ....2. Burundi au Congo au Somalia. Hana uwezo wala sifa ya kuwa Rais. Tumuepuke Slaa kama ukoma. Tusidanganyike
  ''.

  Hii msg imeingia kupitia namba hii: +3588976578.

  Nadhani hii msg ni ya uchokozi, unafiki na uchochezi wa hali ya juu. Sina shaka ni vibaraka na makada ya CCM yanatumia vocha za EPA kuandiika na kuzituma hizi message. Mzee wangu nae kapokea same msg with same namba.....So chukua tahadhari ukikutana na msg kama hizi,ni uwongo usiopingika. Nawakilisha.
   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Nimepokea na mimi sms ya aina hii leo asdubuhi, nikajiuliza hivi hata kama ni ushabiki wa siasa watanzania tumefikia hatua hii. Ninaomba number za TCRA ili niweze kui-report hiyo number huko ili waweze kufuatilia mmiliki wake na ikiwezekana wachukue hatua za kisheria.

  Siji kama Gen Shimbo ameiona nafikiri watu wa aina hii ndiyo wanaotaka kumwaga damu. Pia kama kuna mtu ana number ya IG P Mwema au Gen Shimbo ninaomba ili niwaforwadi waweze kuchukua hatua mapema
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Soon ntakuja na jibu zinatoka wapi hizi sms
   
 4. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM ndo itakuwa chanzo cha machafuko nchi hii kuliko watu wengi wanavodhania!
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wameona sms za changis CCM hazitoshi sasa wameanza kutuma ujinga mwingine! Hiyo namba yenyewe imekaa kiajabu ajabu!
   
 6. b

  bojuka Senior Member

  #6
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sms hizo zimeandaliwa na ccm ambapo wanawashawishi wananchi ili wajiingize katika michezo (bahati nasibu ) baada hapo wanawatumia sms ili kuwadanganya na kuleta maneno ya kuhatarisha usalama wa watanzania. watanzania wenzangu tupo katika kipindi kigumu sana yatasemwa mengi kuwachafua wagombea wenye uelekeo wa kushinda nafasi mbalimbali eg; Urais , Ubungena Madiwani.

  TUMEWAGUNDUA HATUDANGANYIKI VIVA DR, SLAA FOR THE PRESIDENT 2010-2015
   
 7. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bobuk unaweza kujua Message center number ya hiyo SMS??
  Hiyo itatusaidia kujua kama zinakuwa originated hapa nchini au la. Hata kama zinatumwa kwa njia ya mtandao Center number itatuwezesha kujua wanatumia server za nchi gani. Kuna wataalamu wa haya mambo humu, tutawaambia CHADEMA namna ya ku-counter hii kitu ikibidi kuwasiliana na hao jamaa ambao server zao zinatumika kuhatarisha amani ya nchi nyingine.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Ilishaletwa tena ya hivi leo asubuhi hapa jamvini, achana nao wazidi kupigia kampeni rais wetu wa awamu ya tano!
   
 9. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Message center ni +255780000030
   
 10. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,356
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Naombeni kuuliza, wote mliopata sms hii mmepata kupitia mtandao gani?
   
 11. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni random, hawajachagua, walichokifanya nadhani wameenda kuziomba aiza, voda, tigo, zantel, na zain, na zingine kwa wale waliojiunga na ccm katika promosheni zao.
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hiyo message inatumia dialling code ya Finland, bila shaka wameweka pandikizi mojawapo huko Ufinland kufanya kazi hiyo. THe next step ni kuitia kashikashi serikali ya Finland kwa kuchochea ghasia nchini. Ngoja niangalie ni nini naweza kufanya againts this and I will be back soon.
   
 13. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna watu wanataka kuandamana kulalamikia zain inatuma meseji za kichochezi, maeneo ya kinondoni akina maama kama wawili wametumiwa na ,paka hapa kuna kundi kubwa lina jadili; nahisi nchi yetu imefika pabaya, JK akikaa Dar kuna jambo lazima afanye, alikaa ikaibuliwa swala la dr slaa kuoa, amekaa tena anaanza kutuma meseji, sidhani kama zaini hawana akili namna hii ila tutaona mwisho wake
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hiyo namba imetengenezwa kuonekana kwamba message zinatumwa kutoka Ufinland, lakini kiuhalisia hiyo message inatumwa kutoka hapo hapo Tanzania. Moja ya makapuni ya simu limejiingiza katika biashara hiyo ya kihuni kwa kutengeneza namba yenye area code inayoonyesha kwamba ni ye nje ya nchi wakati kiuhalisia ni ya humohumo ndani ya nchi. Namba ambazo zimefanya kazi siku ya leo kwa nchi ya Ufinland hadi hivi sasa zimeorodheshwa hapa: 358-897-XXXX Exchange - Reverse Phone Lookup!. Lakini namba hiyo haimo kati ya hizi. Kwa mtizamo huo ni dhahiri kwamba hii ni kazi ya kikundi fulani na kampuni moja wapo ya simu hapo Tanzania ndiyo inayofanya uhuni huu. Kuna haja ya kuzigomea simu zake zote hiyo kampuni mara itakapofahamika.
   
 15. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  halafu ndo wanajifanya kuwatumia JWTZ kuonyesha kwamba kuna watu wanataka kuvuruga amani wakati wao ndo waanzilishi!!:mad:
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Country code ni ya FINLAND!
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata hivyo wajue kuwa watu wameshawastukia. Mimi nawashauri waweke mpita kwapani mechi iishe tusonge mbele. Wanataka kutuletea balaa hawa watu.
   
 18. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #18
  Oct 9, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  God forbid CCM.
   
 19. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu yatafanywa mengi sana ila TUMEFUNGUKA MACHO!!! Pumbafu, nitumieni hiyo message niwalipue..!
   
 20. r

  ramson34 Senior Member

  #20
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamani kwani hamjasikia kile kikundi cha wale wataalamu wa IT toka India chini ya Milaji na Kinana ambao wako nyumba moja hapo Upanga,ndiyo wanaofanya mambo yote hayo..so simple so clear.
   
Loading...