Angalia namna Lowassa anavyojichanganya na kuonyesha mapungufu yake mengi

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nakumbuka fika kuwa katika mikutano yake wakati hata bado hajakinunua chadema, ukawa na watannzania baadhi wasiojielewa lowassa alikuwa kila anaponukuliwa anasema nanukuu " mimi sitaki mtu masikini na siamini kama kuna mtu masikini tanzania " mwisho wa kunukuu. kwa wale mtakaobisha tafuteni kauli zake hizi kupitia kwa watu waliokuwepo katika hiyo mikutano yake na kauli hii hii pia aliitumia wakati akitangaza nia kupitia chama kikubwa, kizuri, bora na kitakatifu tanzania, africa na duniani kwa ujumla cha CCM.

Ili kuonyesha huyu mzee anavyofilisika kichwani leo tena akiwa huko kwa watu wanaopenda umbea sana kuliko wowote nchini Tanzania mkoani Mbeya lowassa alisema nanukuu " nikiwa rais nitaunda serikali rafiki na masikini kwani natambua tuna marafiki wengi " mwisho wa kumnukuu. je kauli zake zinafanana? kwanini haeleweki? ila sishangai kwani yawezekana wengi wenu msiweze kugundua hili pengine kutokana na kutekwa na mihemko ya siasa za panya road za wapinzani wa nchi hii CHADEMA / UKAWA.

Jambo jingine ambalo linanichanganya kwa huyu mgombea mwenye ndoto za alinacha lowassa ni kitendo chake cha kutumia udhaifu wa kiuchumi wa makundi fulani ya watanzania kama ndiyo mtaji wake wa kisiasa. kwa mfano kokote ambko lowassa ataenda kuhutubia lazima atasema maneno au kauli hii " nikiwa rais nitahakikisha maisha bora kwa mama ntilie, boda boda na wamachinga ". hivi ni kweli matatizo ya nchi hii ni ya watu au makundi hayo ya watu? nimewahi mno kufuatilia siasa za wenzetu waliotutangulia katika siasa tena za kidemokrasia kwa muda mrefu na hapa kwa ulaya nachukua mfano wa nchi ya marekani ambapo nakumbuka wakati wa kampeni za urais obama wa democrat na john mcain wa republican muda wote wa kampeni zao walikuwa wanagusia tu " sensitive and very touching issues " zinazowahusu na zitakazowafaidisha wamarekani kiujumla vivyo vivyo kwa majirani zetu wa kenya hata wao wakati wa akina uhuru na odinga na wao hawakuwa mbali sana kama akina obama na mcain wakati wa kampeni zao ila kwa hapa Tanzania naona lowassa anataka kuleta mtindo wa siasa uitwao " monduli politics " ambazo zimejaa sana sera za kucheza na akili za watu wasiojua kufikiri na ambao wapo tayari kupelekwa pelekwa kama ng'ombe wakiwa malishoni.

Ewe mgombea wangu rais mtarajiwa dr. John Pombe Magufuli naomba utakapoanza kampeni zako hebu tuonyeshe kuwa kweli wewe ni phd holder na utakayoyasema yaakisi hiyo elimu yako kubwa na binafsi nakuaminia na utafanikiwa mno. watanzania tunakutegemea sana magufuli na tuna imani na wewe na chama chako pia.

Tuvumiliane tu kwa sasa.
 
Elimu yangu ni ndogo sana lakini cyo kiasi cha kushindwa kupembua jambo jema na baya. Kwanza kabisa ndugu yangu umewakosea sana watu wa Mbeya kwa kuwaita wanapenda sana umbeya kuliko mtu yoyote au eneo lolote hapa duniani,hapa umenifanya nikuone mtu wa mihemuko na mahaba ya kisiasa. Tayari umejinasibu kuwa upo upande gani ktk siasa. Watanzania wanajua nn watakwenda kukifanya kwenye sanduku la kura,hatuna haja ya kudharauliana,kutukanana,tushindane kwa hoja na cyo kejeli. Humpendi Lowasa tupe hoja zenye mashiko ili tuamini kuwa unayemuita Rais wako Magufuli kuwa ni zaidi ya Lowasa. Lakin ukija na kejeli,mihemuko na mahaba ya kisiasa hakuna atakaye kuelewa hata km ni msomi vp. Siasa cyo ugomvi,lakin kwako inaonekana siasa ni ugomvi na kejeli.
 
Anajifungamanisha na masikini kabla na siku zote lowasa amekuwa akichangia vikoba na kwa nchi yetu, ni yeye na reginald mengi waliowafikia masikini kwa vile ambavyo Mungu amewapa.
 
Juu ni Mbeya chini ni Dar Lowassa kavunja rekodi,trh 17 atakwenda Unguja kuvuruga ngome ya Ccm ili October SS Hamad aanze kusherehekea saa 8 mchana.Pemba hakuna aja ya kampeni ile ni ngome nzito ya Cuf tokea kipindi cha Mwalimu Jk.
 
Ni bora kuwa na imani na magugufeli kuliko kuwa na imani na chama chawala maana maguu fully naye ni team Eddo..
 
Elimu yangu ni ndogo sana lakini cyo kiasi cha kushindwa kupembua jambo jema na baya. Kwanza kabisa ndugu yangu umewakosea sana watu wa Mbeya kwa kuwaita wanapenda sana umbeya kuliko mtu yoyote au eneo lolote hapa duniani,hapa umenifanya nikuone mtu wa mihemuko na mahaba ya kisiasa. Tayari umejinasibu kuwa upo upande gani ktk siasa. Watanzania wanajua nn watakwenda kukifanya kwenye sanduku la kura,hatuna haja ya kudharauliana,kutukanana,tushindane kwa hoja na cyo kejeli. Humpendi Lowasa tupe hoja zenye mashiko ili tuamini kuwa unayemuita Rais wako Magufuli kuwa ni zaidi ya Lowasa. Lakin ukija na kejeli,mihemuko na mahaba ya kisiasa hakuna atakaye kuelewa hata km ni msomi vp. Siasa cyo ugomvi,lakin kwako inaonekana siasa ni ugomvi na kejeli.

Well said boss! I have nothing more & nothing less, Be blessed. Kweli lugha za matusi na kudharauliana hazifai, kushindana/kuongea kwa hoja ndiyo jambo Jena.
 
Hao ndo wapo kwenye system ss wanahaha hizo kauli wslizificha wp ole wenu maana damu yenu i juu ya watanzania wengi wanaotaabika na ninyi wachache mnaojineemesha
 
Well said boss! I have nothing more & nothing less, Be blessed. Kweli lugha za matusi na kudharauliana hazifai, kushindana/kuongea kwa hoja ndiyo jambo Jena.

Unajua Mkuu,tatizo la walio wengi wanadhani siasa ni matusi na ugomvi. Na ndiyo kitu ambacho kimejengeka sana ktk siasa za Tanzania. Nielimishe,tetea hoja yako ili nikubaliane na wewe. Lakin tukianza kutukanana hapa hata haisaidii,na pia zaidi ya yote wengi wetu humu hatufahamiani majina halisi,hujui natokea wapi? Kwahiyo ukinitukana ni sawa na kukitukana kivuli. Na pia jiulize swali,ukinitukana kuna mzgo umenifungia ntashindwa kuubeba. Penye ukweli tuseme ukweli,penye uwongo tukiri uwongo. Hv ni nani aliye msafi ndani ya ccm na kumuita mwenziye fisadi? Ni nani aliyemsafi ndani ya Ukawa na kumuita mwenziye Fisadi? Binadamu wote ni wadhaifu ila kuna kuzidiana. Mm mtazamo wangu ni kuipumzisha ccm tuangalie upande mwingine hata km itakuwa ccm B,unachotakiwa kufanya ni kuniekeza kwa hoja kwann nisiipigie kura Ukawa? Lakn ukitukana haisaidii hata chembe. Asante Mkuu
 
cleverbright

mbona unatoka sana mapofu vidoleni? Tuache watanzania tuamue wenyewe raisi tunayemtaka
 
Last edited by a moderator:
Ila kihuhaki tunataka mtu c sera make kila chama KInasera nzr sana ,xaxa shida,nan wakutekeleza ,mtu kwanza
 
Back
Top Bottom