Andy Swebe ambassodor katutoka

Wayne

JF-Expert Member
May 27, 2009
659
201
Mwanamuziki Andy Swebe a.k.a Ambassodar aliyepata kuvuma sana na kundi la MK GROUP enzi zile akipiga gitaa la base, leo asubuhi amefariki dunia baada ya kubanwa na pumu. Msiba upo Kijitonyama.
MUNGU ailaze roho ya marehemu mahala pema... Amin

Source:Wanandugu
 
...Oh! My God! May God rest his soul in peace~AMEN. Andisye, thanks for the memories bro.
 
RIP Andy Swebe! Poleni ndugu ,jamaa na marafiki na mashabiki wote wa muziki wa dance!
 
Andy alikuwa mtoto wa Upanga aliyekuwa kwenye Muziki wa Dansi by then, basi wale vijana wenzake wa enzi zile wakamwita Ambassodor(balozi) kwa maana alikuwa anawakilisha vijana wenzake wa upanga kwenye muziki huo.
Wakafuata wengine wengi akiwemo mdogo wake Mpeli naye alikuwa napiga base

Tutakukumbuka Brother...
 
RIP Andy niliwahi kuhudhuria dansi la MK Group bandari grill New Africa hotel several times alikuwa akiungurumisha besi gitaa nilimfananisha sana na Ilunga Banza Mchafu....sote tuko njia moja hiyo hiyo!
 
May all beings attain enlightenment.

Maskani Harlem imezizima.
 
RIP Ambasador Andy.Huyu nilikuwa namfanansisha na yule nguli wa Base gitaa Nguma Lokito wa Jamhuri ya Congo.Kuna baadhi ya nyimba base gitta la Ambasador Andy lilisikaka vyema eg Maumivu makali na Yaliyopita si Ndwele.

Ambassodor Andy wasalimie Asia Darwesh,Rahma Shally na Joseph Mulenga.
 
Ngongo, umenikumbusha " Maumivu Mkali''......................kabla jua halijacha..................
 
RIP Andy Swebe
 
Attachments

  • IMG_2380.JPG
    IMG_2380.JPG
    189.8 KB · Views: 102
RIP Ambasador Andy.Huyu nilikuwa namfanansisha na yule nguli wa Base gitaa Nguma Lokito wa Jamhuri ya Congo.Kuna baadhi ya nyimba base gitta la Ambasador Andy lilisikaka vyema eg Maumivu makali na Yaliyopita si Ndwele.

Ambassodor Andy wasalimie Asia Darwesh,Rahma Shally na Joseph Mulenga.
Haujakosea mkuu wangu....Huyu bwana hakika ndo alikuwa Ngouma Lokito wa Tanzania,jamaa alikuwa mtaalamu kweli kwenye gitaa la besi......Binafsi sikuona kama alikuwa na mpinzani katika hilo gitaa zito kwa wanamuziki wa enzi zake,labda kwa mbali Bakari 'Beka' Semhando na Joseph Watuguru ndo walikuwa wanamkaribia.......Ndo hivyo tena,kizuri hakidumu....

Hakika tutamkumbuka Balozi Andy Swebe kwa umahiri wake katika upigaji gitaa zito la besi katika bendi zote alizopitia kama vile bendi za Orch. Makassy, MK Group, Afriso Ngoma, MK Group, Kilimanjaro Connection(ya Kanku Kelly), African Beats(ya Mafumu Bilal 'Bombenga'), African Revolution(wakati huo wakitumia mtindo wa chumvi chumvi 'utalamba) na baadae The Almas Band......

Kwa hakika tutakukumbuka Andy,wewe umetangulia,sisi tunafuata.....

Upumzike kwa amani Balozi wetu Andy Brown Swebe...
 
Poleni..na Mwenyezi Mungu amrehemu....ndio tunapoteza amali zetu katika muziki wa nyumbani.....coz hakuna mbana pua ajuae kucheza hata chombo kimoja cha Muziki
 
Rest In Peace bro Andy!...
umetuachia kumbukumbu za kudumu maishani,
..thanks for the time, for being among us!

  • Thanks
Reactions: BAK

Similar Discussions

Back
Top Bottom