kunguni wa ulaya
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 4,131
- 6,109
Mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania aliyewahi kujizolea sifa kem kem katika miondoko ya dansi hapa nchini wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica a.k.a Wajela Jela Gwaa, Ndanda Cosovo ‘Kichaa’ amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinasema marehemu alifikishwa hospitalini hapo kupata matibabu ya Vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua siku chache zilizopita lakini alifariki mapema asubuhi ya leo.
Pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wa muziki kwa ujumla kwa msiba huu.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
Amina.
Ndugu, jamaa na marafiki wa Ndandaa wakiendelea na kikao Kinondoni, kujadili mazishi. Baba mdogo wa mwanamuziki huyo, Kardinal Gental ambaye amethibisha kifo chake, amesema baadae watatoa tamko ni wapi Ndandaa atazikwa kati ya Tanzania au nyumbani kwao Congo (DRC).
Ndandaa amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa tangu juzi mchana baada ya kuhamishwa kutoka hospitali ya Mwananyamala.