Andrew Nyerere on Mwalimu humble children!

Andrew Nyerere on Mwalimu humble children!

I have learned alot from the first-last page,kiukwel JF ni shule ya kutosha.
 
Asante JF nimeweza kupata walau moja mbili za familia ya Nyerere. Kumbe watoto wengi wa nyerere wameshiriki kwenye majeshi ya nchi yetu,Safi sana. Hii inaonyesha hawakuwa mayai mayai kama wa mfalme aliyepo sasa.

R.I.P John Nyerere, the retired Jet Fighter Pilot.
 
WanaJf,

NI vizuri tukawafahamu watoto wote wa Mwalimu Nyerere, wako wapi, wanafanya nini na wanaishije. Ninatuma ombi hili maalumu ili tuweze kuwajua hawa watu kwa sababu ndiyo familia ya pekee ndani ya nchi yetu inayoheshimika zaidi kutokana na kazi za baba yao.

Mimi kwa kweli siwajui ila kidogo sana namfahamu Makongoro wakati akiwa Mbunge wetu hapa Arusha na kipindi hicho nilikuwa bado mdogo.

Nina hamu sana sana ya kuwajua hawa watu wanafanya nini na ni kwa nini hawajihusishi na siasa na kutafuta vyeo, na nataka kujua shule walizosoma. Je, walisoma International school? Halafu napenda kujua kama walipelekwa ng'ambo kusoma na elimu zao zikoje.

Tupende tusipende familia ya Mwalimu Nyerere mdiyo familia Humble na ya kuheshimika kuliko familia yoyote hapa Tanzania.

 
Ni familia pekee ninayoiheshimu kuliko familia kupe zilizopo sasa za viongozi wakubwa Tanzania.
 
Hii familia mwalimu aliipa malezi ya kweli
Huwezi kuwafananisha na watoto wa Prof au wa ruksa au nyoka wa makengeza au yule wa Betna (Mil 10 za mboga)
Hiki kizazi cha mwalimu ni kizazi cha dhahabu

Hakika umenena,familia hii imetukuka. Huwezi ilinganisha na familia za wafalume wa sasa wanaozaa na kulea mafisadi, wapenda madaraka na anasa za kutisha. Hawana uchungu na nchi na watu wake waliotopea katika ufukara na dhiki ili hali inchi imetamalaki kwa lasilimali zenye utajili mkubwa.Kuitwa baba wa Taifa si mchezo , ni pamoja na kuyashinda ya dunia Mungu azidi kubariki kizazi na vizazi vyake.
 
makongoro
john
madaraka
leticia
andrew
rose
kabula
george
queen
mwana
rizmoko
magulu machemba
litundu lisuuuu
manyika john
kababwe nyepesi
 
Mmoja ndo katutoka jana. John Guido Nyerere alikuww mtoto wa nne kwa mwalimu nyererr na mwalimu maria. Alikuwa fighter pilot. Tutamzika butiama jumatano mei 13. Tayari tumeshawasili butiama kumsindikiza kamanda john.

John alikuwa mcheza karate na mpiga gitaa. Alikuwa na wimbo wake maarufu wa 'amina dole tupu'
 
Jana usiku kupitia mmoja wa wanafamilia kwa jina Endrew ambae ni Member humu aliwaataarifu wana JF kwa kuondokewa na ndugu yao John Nyerere ambae ni mtoto wa nne Kuzaliwa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katai ya watoto nane.
 
Mmoja ndo katutoka jana. John Guido Nyerere alikuww mtoto wa nne kwa mwalimu nyererr na mwalimu maria. Alikuwa fighter pilot. Tutamzika butiama jumatano mei 13. Tayari tumeshawasili butiama kumsindikiza kamanda john.
Kaka Manyerere Jackton mpe pole sana Yericko Nyerere na watoto wengine wa mwalimu. Najua mpo naye hapo Butiama.
 
Last edited by a moderator:
Kuna yule alimuomba mwalimu pesa ya shati kwa ajili ya sikukuu mwalimu akamjibu asubiria mshahara utoke ni nani?
 
John alikuwa mcheza karate na mpiga gitaa. Alikuwa na wimbo wake maarufu wa 'amina dole tupu'
Wasaidie Watanzania wa kizazi cha late 80s na sasa kujua watoto wafamilia ya Mwalimu...ni muhimu sana najua una uwezo huo kiatu hicho kinakutosha kulik mtu yoyote yule...manake kwa ukubwa wa Endrew ...I hope wewe ni mdogo..Wapatie ufahamu Watanzania si vyema kukaa na taarifa ..kama hizi ambazo dada huyu wa kizazi cha dotcom ameomba kupitia thread hii.Kwa kupatikana taarifa hizo humu kutaweka kumbukumbu na kutumika kujibu maswali yoyote yapatikanayo humu.

Japo kuna maandiko lakini uenda andiko lako likawa ni moja ya andiko zuri na la mafunzo mengi ukizingatia unaufahamu nje na ndani...mlivyolelewa kiasi kuwa mnaweza kula kwa mama Ntilie japo mmekulia kuta za Ikulu.Tena ingekuwa vyema ukatuandikia japo kijiwasifu kidogo cha marehemu John Nyerere ukatupia humu watu wakajifunza kuona maisha ya baadhi ya watoto wa Mwalimu mlivyo lelewa pia kwa fursa hiyo utuandike maisha ya watoto wa Mwalimu kwa ujumla.

Ukweli kwa tuliko pita kwa sasa watu wanaanza kuvutika na jinsi maisha ya watoto wa Mwalimu yalivyo reflect maisha ya kawaida ya mtoto yoyote yule wa kitanzania, maana yake ni maisha simple yasiyo na mawaa wala ukuu na kuishi kwa fursa ya nguvu aiyoijenga Baba..bali kutegemea na weredi wa akili ya mtoto mwenyewe na ufahamu wake.

Ni ombi na ukiona ikikupendeza basi anza na marehemu kisha uje utupe kwa ujumla ya watoto wote kwa faida ya vizazi vya kesho.Nimepita kwenye blog ya ndugu yako madaraka sijapata kuona sehemu yoyote yenye ufafanuzi anaomba binti huyu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom